Binti amenichanganya mpaka nimeshukia njiani

Miaka ya boarding tena ile ya high school, shule zikifungwa machalii wa Moshi walikuwa wanababaika sana na toto za Dar, basi stendi unakuta mtu anakupa company kuanzia saa nne mpaka basi linakuja mitaa ya saa kumi jioni, atakupeleka ukale lunch, mizigo anaweka kwenye kibanda na analipia, jina umedanganya lakini uniform za shule anazijua. Shule ikifunguliwa unasikia barua ya Sky Eclat, unakumbuka lilikuwa jina langu hili siku ile😀😀😀
 
Mkuu umenichekesha sana.
Kweli uliamua kujitoa mhanga ila haikuwa bahati yako.
Hata hivo sijui uliwaza nini mana angeweza asiwe na jamaa yake na bado akakutosa pia .
Ila pole nadhani umejifunza
 
Hahahahahahaa polee

Nafasi yako ilikuwa ndani ya basi ucheze karata zote ili binti asishuke Iringa uende nae hadi Dar angekuwa keshamuacha jamaa yake. Hehehehee polee.

Nakumbuka nilipokuwa kigori **** mkaka alishuka kwenye daladala kituo sio chake na alinisindikiza hadi nyumbani hehehe. Kote huko sijamjibu hata kimoja alichokuwa ananiongelesha. Nilipokaribia nyumbani nikamwambia skiza nipe namba ya simu ya kazini kwako na anuani ili mimi nikutafute maana enzi hizo geti kali na sikutaka apajue nyumbani. Nikimuacha anisindikize kutoka kituo cha daladala hadi karibu na nyumbani maana kigiza cha saa kumi na mbili jioni kilikuwa kimetanda hivo nilikuwa na woga wa kutembea mwenyewe.
Hahahaha nilikuwa nashangaa wanaume unaanzaje kumfatilia mschana hata humjui tena alinilipia nauli, simjibu chochote aniongeleshacho mie natembea tuu hahahah

Kwenye daladala sasa akishakulipua nauli utaona konda anauliza sheli. ... kimya.... kwa mpemba.... kimya... jamaa anasubiria binti aseme shusha ili naye ashuke.

Siku ingune nilikutana na jamaa wa hivi na nilimuuza maana nilikuwa natoka kawe naenda posta, baada ya kunilipia nauli nikasema leo atakoma maana ukimuangalia usoni anakutazama kwa macho ya kukutongoza tuu.
Kufika mbuyuni konda kuuliza mbuyuni nikasema shusha, yeye akatangulia kusimama na kushuka mie nikajichelewesha nilisimama kisha nilipoona kushuka nikainama na kurudi kukaa. Konda kuuliza mwingine kimyaa.... akaruhusu gari iondoke heheheheh nilichungulia nje jamaa macho yanamtoka maana mda ule kupata usafiri wa posta maeneo yale ni shida.

Poleni ila nilifanya yale kwakuwa ilikuwa utoto tuu hahahaha kweli wanaume mmeumbiwa mateso.

Wakati nasoma sekondari kuna mvulana flani alishanisindikiza toka tumeshuka kwwnye daladala hadi eneo la tuition wakati huo na yeye anasoma tuition ila kwingine. Siku hiyo alinisubiri hadi mie nimetoka tuition na tunarudi tumepanda daladala moja. Akanilipia nauli, sikutaka apajue nyumbani hivyo niliposhuka mwisho wa kituo nikamwambia nipe address ya shule unayosoma na jina tuandikiane barua si unajua home kuna mbwa wakali? Akanielewa ndo nikamtoa kihivyo daah.

Yaani mleta mada nimekuelewa sanaa. Pole kwa yaliyokusibu sio pekeyako ni wanaume wengi tuu huwakuta haya.
ahahaaa we mdada wewe kumshusha mwenzio njiani jamani?
 
Wakuu nimeamini mapenzi yana nguvu kiasi kwamba waweza fanya mambo mengine kwa msukumo usiokua na tija. Juzi hapa nimekuwa nikisafiri kutoka mkoani kwenda Dar, but ndani ya bus kulikua na mrembo machachari mno kiasi kwamba nikajipa moyo kama atafanikiwa kushukia ninaposhukia basi siwezi mlazia damu.

Bahati mbaya akawa ameshuka Iringa, nami mtu mzima nikajitosa nika drop kwa vile nilimuelewa sana. Bus likaondoka, ile najiandaa kumsemesha mara ghafla akaja jamaa kajaa jaa hivi, yaonesha ni jamaa yake maana kwa zile hugs nikajua hapa sina changu, then wakatokomea kusikojulikana.

Basi mtu mzima nikaanza kuhaha pesa ya rum na usafiri wakunifikisha safari yangu ukizingatia nilikua nina interview ya kikazi.

Wanawake bwana, sijui mlinyunyuziwa sumaku ya aina gani!
Hahahahahahahahahaahaahahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaahahahahahahahaha
 
Wakuu nimeamini mapenzi yana nguvu kiasi kwamba waweza fanya mambo mengine kwa msukumo usiokua na tija. Juzi hapa nimekuwa nikisafiri kutoka mkoani kwenda Dar, but ndani ya bus kulikua na mrembo machachari mno kiasi kwamba nikajipa moyo kama atafanikiwa kushukia ninaposhukia basi siwezi mlazia damu.

Bahati mbaya akawa ameshuka Iringa, nami mtu mzima nikajitosa nika drop kwa vile nilimuelewa sana. Bus likaondoka, ile najiandaa kumsemesha mara ghafla akaja jamaa kajaa jaa hivi, yaonesha ni jamaa yake maana kwa zile hugs nikajua hapa sina changu, then wakatokomea kusikojulikana.

Basi mtu mzima nikaanza kuhaha pesa ya rum na usafiri wakunifikisha safari yangu ukizingatia nilikua nina interview ya kikazi.

Wanawake bwana, sijui mlinyunyuziwa sumaku ya aina gani!
Jicho lako linaicha hooooi!
 
Mkuu umenichekesha sana.
Kweli uliamua kujitoa mhanga ila haikuwa bahati yako.
Hata hivo sijui uliwaza nini mana angeweza asiwe na jamaa yake na bado akakutosa pia .
Ila pole nadhani umejifunza
hakika nimejifunza mkuu,kwanza jamaa lake hata haliendani nae,nikamuonea wivu..
 
Ndo nyie mnapenda mpk watu wanahis umelishwa limbwata kumbe ni ubox wako nwenyew
 
Hahahahahahaa polee

Nafasi yako ilikuwa ndani ya basi ucheze karata zote ili binti asishuke Iringa uende nae hadi Dar angekuwa keshamuacha jamaa yake. Hehehehee polee.

Nakumbuka nilipokuwa kigori **** mkaka alishuka kwenye daladala kituo sio chake na alinisindikiza hadi nyumbani hehehe. Kote huko sijamjibu hata kimoja alichokuwa ananiongelesha. Nilipokaribia nyumbani nikamwambia skiza nipe namba ya simu ya kazini kwako na anuani ili mimi nikutafute maana enzi hizo geti kali na sikutaka apajue nyumbani. Nikimuacha anisindikize kutoka kituo cha daladala hadi karibu na nyumbani maana kigiza cha saa kumi na mbili jioni kilikuwa kimetanda hivo nilikuwa na woga wa kutembea mwenyewe.
Hahahaha nilikuwa nashangaa wanaume unaanzaje kumfatilia mschana hata humjui tena alinilipia nauli, simjibu chochote aniongeleshacho mie natembea tuu hahahah

Na nyie ndo walaini sana mkishapewa maneno matam nyie.
 
Wewe
Wakuu nimeamini mapenzi yana nguvu kiasi kwamba waweza fanya mambo mengine kwa msukumo usiokua na tija. Juzi hapa nimekuwa nikisafiri kutoka mkoani kwenda Dar, but ndani ya bus kulikua na mrembo machachari mno kiasi kwamba nikajipa moyo kama atafanikiwa kushukia ninaposhukia basi siwezi mlazia damu.

Bahati mbaya akawa ameshuka Iringa, nami mtu mzima nikajitosa nika drop kwa vile nilimuelewa sana. Bus likaondoka, ile najiandaa kumsemesha mara ghafla akaja jamaa kajaa jaa hivi, yaonesha ni jamaa yake maana kwa zile hugs nikajua hapa sina changu, then wakatokomea kusikojulikana.

Basi mtu mzima nikaanza kuhaha pesa ya rum na usafiri wakunifikisha safari yangu ukizingatia nilikua nina interview ya kikazi.

Wanawake bwana, sijui mlinyunyuziwa sumaku ya aina gani!
Wewe huna experience,ilitakiwa basi liliposimama kula au kuchimba dawa uhakikishe unajua anashukia wapi
 
hahaha mkuu sasa umenichekesha nakufanya nisahau mauzauza yote ya juzi, ila huyo mwana wa mbuyuni atakua aliisoma namba..eeh we mutu mubaya

Hahahahahahaa ilikuwa utoto sasahivi siwezi fanya hivyo
 
Wakuu nimeamini mapenzi yana nguvu kiasi kwamba waweza fanya mambo mengine kwa msukumo usiokua na tija. Juzi hapa nimekuwa nikisafiri kutoka mkoani kwenda Dar, but ndani ya bus kulikua na mrembo machachari mno kiasi kwamba nikajipa moyo kama atafanikiwa kushukia ninaposhukia basi siwezi mlazia damu.

Bahati mbaya akawa ameshuka Iringa, nami mtu mzima nikajitosa nika drop kwa vile nilimuelewa sana. Bus likaondoka, ile najiandaa kumsemesha mara ghafla akaja jamaa kajaa jaa hivi, yaonesha ni jamaa yake maana kwa zile hugs nikajua hapa sina changu, then wakatokomea kusikojulikana.

Basi mtu mzima nikaanza kuhaha pesa ya rum na usafiri wakunifikisha safari yangu ukizingatia nilikua nina interview ya kikazi.

Wanawake bwana, sijui mlinyunyuziwa sumaku ya aina gani!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Ulafi wako umezidi
 
Hahahahahahaa polee

Nafasi yako ilikuwa ndani ya basi ucheze karata zote ili binti asishuke Iringa uende nae hadi Dar angekuwa keshamuacha jamaa yake. Hehehehee polee.

Nakumbuka nilipokuwa kigori **** mkaka alishuka kwenye daladala kituo sio chake na alinisindikiza hadi nyumbani hehehe. Kote huko sijamjibu hata kimoja alichokuwa ananiongelesha. Nilipokaribia nyumbani nikamwambia skiza nipe namba ya simu ya kazini kwako na anuani ili mimi nikutafute maana enzi hizo geti kali na sikutaka apajue nyumbani. Nikimuacha anisindikize kutoka kituo cha daladala hadi karibu na nyumbani maana kigiza cha saa kumi na mbili jioni kilikuwa kimetanda hivo nilikuwa na woga wa kutembea mwenyewe.
Hahahaha nilikuwa nashangaa wanaume unaanzaje kumfatilia mschana hata humjui tena alinilipia nauli, simjibu chochote aniongeleshacho mie natembea tuu hahahah

Kwenye daladala sasa akishakulipua nauli utaona konda anauliza sheli. ... kimya.... kwa mpemba.... kimya... jamaa anasubiria binti aseme shusha ili naye ashuke.

Siku ingune nilikutana na jamaa wa hivi na nilimuuza maana nilikuwa natoka kawe naenda posta, baada ya kunilipia nauli nikasema leo atakoma maana ukimuangalia usoni anakutazama kwa macho ya kukutongoza tuu.
Kufika mbuyuni konda kuuliza mbuyuni nikasema shusha, yeye akatangulia kusimama na kushuka mie nikajichelewesha nilisimama kisha nilipoona kushuka nikainama na kurudi kukaa. Konda kuuliza mwingine kimyaa.... akaruhusu gari iondoke heheheheh nilichungulia nje jamaa macho yanamtoka maana mda ule kupata usafiri wa posta maeneo yale ni shida.

Poleni ila nilifanya yale kwakuwa ilikuwa utoto tuu hahahaha kweli wanaume mmeumbiwa mateso.

Wakati nasoma sekondari kuna mvulana flani alishanisindikiza toka tumeshuka kwwnye daladala hadi eneo la tuition wakati huo na yeye anasoma tuition ila kwingine. Siku hiyo alinisubiri hadi mie nimetoka tuition na tunarudi tumepanda daladala moja. Akanilipia nauli, sikutaka apajue nyumbani hivyo niliposhuka mwisho wa kituo nikamwambia nipe address ya shule unayosoma na jina tuandikiane barua si unajua home kuna mbwa wakali? Akanielewa ndo nikamtoa kihivyo daah.

Yaani mleta mada nimekuelewa sanaa. Pole kwa yaliyokusibu sio pekeyako ni wanaume wengi tuu huwakuta haya.
Wewe kiboko
 
si angepanda bodaboda?
haha apande boda kufukuzia nyumbu wake..teh dunia inamaajabu basi kumbe hata mimi ningekodi boda labda tungewakuta kitonga comfort ila ndio sikua na tembo tena
 
Miaka ya nyuma kidogo nilikuwa natokea morogoro to arusha. Nilikutana na mtoto aseeh ni sheeda. Nilimwelewa kinoma. Alikaa siti ya nyuma nyuma na jamaa fulani hivi alikuwa kauzu balaa.

Mimi nilikaa mbele kidogo. Nikawa namchob ile kinyume nyumee. Nikawa nafikiria namna hata ya kuongea nae niombe namba. Kidogo nikajiongeza ni kaenda walipokaa na huyo jamaa nikamwambia bro samahan unaweza kwenda kukaa siti yangu maana kuna vitu tunazungumza na sister angu hapa kabla sijashuka.

Yule mtoto alishangaa akaguna but hakuongea chochote akacheka. Jamaa akagoma akadai anataka kukaa dirishani. Tulipo fika Liverpool nikamhamisha mama niliyekuwa nimekaa nae akaenda kukaa na jamaa ila aliona aibu kukataa maana nilimtoa chips mbuzii. Jamaa alininunia hadi tunafika arusha.

Nikakaa na mtoto hadi stend. Hivyo haya mambo yapo mkuu
 
Ni ugonjwa wetu sisi wanaume
kama sio mwanaume utamuona mtoa mada ni mtu wa hovyo hovyo lakini mtoa mada ni shuja a kapigana mpaka tone la mwisho
ningekua na hela ningekuchangia nauli
Ttz co kutoa mada, ttz ni jinsi alivyoiwasilisha nikama yuko proud kumbe ujinga tu, ckatai kuwa amemuelewa binti alipaswa ajiulize maswal machache kabla ya kushuka.
Kwanza huyu dada anaweza kuwa single?
Kwan nn asiombe namba kwa ustaarabu tu ili baadae au cku nyingine afanye mawasiliano nae amjui zaid kama yuko single au anamtu?
Okay najua ni ngumu sometimes kupata no ya mtu tena hamjuani bt kama mwanaume lazma uwe na mbinu nyingi za, kumuingia mtu,.
Ttz la wanaume wengi mnapapara ndo maana mnaangukia pua,.
 
si angepanda bodaboda?

Hahahahaa sikutaka hata kuwaza anaweza fanya nini wakati akiona daladala inaondoka na mie sijashuka hahahahah. Ila pia niliwakera abiria wa ndani ya basi wale waliosimama si unajua kwenye daladala mtu akisimama halafu akasikia mtu aliyekaa amesema shusha anaanza kujiandaa kukunja kiuno ili akae. ... hehehe mimi nilisimama hapo hapo kwenye siti watu walijisogeza kama kunipisha nishuke kisha nikainama kama naokota kitu kisha niliposikia konda anauliza mwingine. ... halafu kimyaa nikakaa. Nikasikia dereva amshaa hahahaha watu nusura wasonye.
 
Kwi kwi kwi kwi lol! Umenikumbusha story moja humu miaka ya nyuma. Jamaa aliona mtoto bomba halafu wowowo lake lilikuwa si la kawaida. Jamaa alimfuata mrembo hadi mlandizi. Kufika mlandizi jamaa akasema sasa nitapata nafasi ya kumwaga sera zangu, mara jamaa anakuja na mkoko baada ya dakika chache tu za kufika pale kituoni na kumchukua yule kimwana. Jamaa akabaki kapigwa na mshangao na hivyo aanze kupanga hesabu za kurudi tena jijini Dar kwa bus.

Back
Top Bottom