Binti amlalamikia mpenzi wake kwa kumvalisha pete ya shilingi elfu 23,000

Binti amlalamikia mpenzi wake kwa kumvalisha pete ya shilingi elfu 23,000

Maisha nidhamani wewe hakuna mtu atapenda awekewe pete mkononi ya 23000seriously mie pete yangu ya uchumba ni ya gharama .

Intake kama mwanaume ambaye hana hela anakusanya kwandugu zake ifike 150000tsh ili amvishe mtu pete nzuri ya hadhi maana anamuheshimu wewe unahela halafu unamdharau mchumba wako kwa kumvisha pete ya 23000tsh seriously ??

Acha madharau na nyie wale wanaompa kichwa huyu sio fresh.
Ataishi single kama akiwa hayupo serious.
 
Acha madharau na nyie wale wanaompa kichwa huyu mdudu sio fresh.
Ataishi single kama akiwa hayupo serious.
Pete ndio upendo?
 
Pete ndio upendo?
Ni heshima n kumuonyesha kwamba pete yenye gharama ndio hadhi yake kwamaana yeye ni wa gharama kwako.

Upendo sio kiunganisho pekee kwenye mapenzi kwa watu wapendanao bali ni heshima,uaminifu ,kujaliana ndio muhimu mtu kama unamjali unampa vitu vya gharama.

Sio vitu visivyo vyagharama bhana msitutishie kama hamtaki kuoa basi humu mliringaga tu mbona tumeolewa tuna mapacha mfululizo kama shule mbegu zenu mmebakiwa nazo
 
MDADA - "Hi Nimevalishwa pete ya uchumba mwezi wa 6. Nilifurahi sana sababu sikutegemea. pete haina hata miezi 2 imeanza kupata kutu. Hata marafiki zangu chuo wameanza kunicheka kuwa nimevalishwa pete fake.

Kuna rafiki wa mchumba wangu nimeongea nae ameniambia pete yangu ni ya elfu 23. Nimejisikia vibaya sana na kujiona sina thamani baada ya miaka yote hiyo ya mahusiano anakuja kunivalisha pete ya elfu 23? Ameshindwaje hata kutafuta pete ya laki?

Ingekuwa tofauti kama angekuwa hana pesa lakini mwanaume ana kazi nzuri tuu na ana pesa. Nimemuuliza kuhusu bei ya pete ameniambia naangalia pete au naangalia ahadi zake kwangu kama zitatimia? Mimi naona pete inaonesha jinsi gani ananipenda na kunithamini. Naona kama hajajipanga hata kunioa.

Sasa amenivalisha pete ya elfu 23 kunilea ataweza kweli? Mimi nimemaliza chuo sahizi na graduation yangu inakuja ila naona yeye anapambana kupanga harusi ikamilike na hawazi hata sherehe yangu ya graduation inayokuja. Nashukuru amenifikiria kunioa si unajua kazi hakuna ukitoka chuo unaenda nyumbani? Bora mimi siendi nyumbani naoelwa ntakuwa na kwangu.

Lakini sasa kwa hii pete naona kama hana mzuka wa kunioa kwa nini anipe pete ya elfu 23?

Mimi sio mwanamke ninaetaka makubwa lakini natamani thamani yangu iwe inachukuliwa kama ilivyo sio kupewa vitu vya bei rahisi.

Kama pete kanunua ya elfu 23? Unafikiri gauni ataweza kunishonea ninalotaka kwa kina kenny the brand? Au ndo nitakodiwa kigauni cha bei chee? Make up jee nitapakwa wapi? Unafikiri hii ni ishara naoneshwa kuwa mwanaume niliyenae sio sahihi? Ni mbahili? Au ni mtu wa kutaka viti fake fake? Nisaidie mawazo yako"

Share na wengine

Update:

Jamaa aibuka kujibu mapigo, ni yule aliyelalamikiwa na mdada kumvisha pete ya shilingi elfu 23,000

JAMAA - "Naandika nikiwa nimetulia lakini naomba nimjibu hapa huyo mchumba aliyedharau pete yangu. Ni kweli nilimnunulia pete ya elfu 23. Lakini sikutaka kumpa pete ya gharama kwa sababu nilikuwa na mipango yangu mingine. Nimeagiza pete zetu za ndoa na pete zake zitakuja pete 2 ya ndoa na ya engagement.

Kwa hayo aliyokuandikia sijui kama naweza kuendelea na shunguli za kumuoa mwanamke kama huyo. Fikiria amemaliza chuo. Ameenda kwao kujiandaa na sherehe zinazokuja. Hajataka hata tukae tufikirie yeye anafanya nini baada ya shule kama ni biashara au tutafute kazi. Mwanamke anawaza vitu vya gharama tuu.

Alivokuwa chuo alikuwa ukimtoa out anataka mwende sehemu za gharama gharama tuu kama sio mahoteli makubwa basi atataka mwende sehemu za bei ghali ili ajipigishe picha apost wiki nzima. Alianza kuja na marafiki zake ukiwarudisha anakununia siku nzima hata mlichopanga kwenda kufanya hamfanyi.

Hapo nimeona anawaza magauni ya mamilioni anasahau kama kuna maisha baada ya hilo gauni la milioni. Anataka akapakwe make up sehemu ambayo hata ukoo wao wote hawawezi kutoa hiyo hela.

Wanaume wenzangu mngekuwa ni nyinyi mna mwanamke wa aina hii mngefanya nini? Nimechoka, Nilikataliwa sana kutembea na vitoto vya chuo mimi nikawa najiwazia natafuta mke acha nitafute mwanamke mdogo mdogo nitamfundisha maisha mwenyewe nakuja kukutana na mtu wa aina hii.

Anataka mambo makubwa ambayo hana uwezo nayo. Alikuwa akitaka kutoka chuo hata kwenda kariakoo anaomba nimpeleke au nimpe hela ya uber. Nadhani siwezi kupanga maisha na mwanamke wa hivi.

Pete nimeshaziagiza zimenigharimu pesa nyingi sana na zimeandikwa tarehe za ndoa na ya engagement imeandikwa tarehe yake ya engagement sijui hata nitazipeleka wapi. Nimechoka kuendeshwa na mtu asiyechangia hata chupi yake mwenyewe"
Kumbe mzee mwenzangu na wew upo insta kwa simulizi. Nimekubamba
 
Watu tumetofautiana , sioni kama pete ni big deal hivo hadi kucomplain eti bei rahisi,kama kweli mnapendana hata ya 10k tu inatosha bana, tatizo wadada tunapenda show off na kutambia marafiki,like hii pete babe wangu alinunua mil 3 hii, mmh for what🤔
 
Sema nini kuvaa lipete linapauka vidoleni bora usinivishe tu ...

Thahabu ina raha yake vidoleni bana, afu inaonesha mwanaume anakuthamini sana[emoji848]
Sio kweli kwamba walivalishwa dhahabu ndio wanathaminiwa sana. Sio kweli hata kidogo. Mimi mke wangu nilimpa pesa nikamwambia nina pesa hiyo kanunue pete ipime vizuri yoyote utakayochagua.

Kaenda kanunua, haikuwa ya dhahabu. Leo tuna miaka 12 kwenye ndoa. Wanaweke wengi wanapenda waonekane wanathaminiwa zaidi kuliko thamani wanayoweza kutoa maisha haya au hata pengine thamani waliyonayo. Hii sio sawa.

Kama ana akili vizuri na anayajua maisha atavaa tu pete yoyote. Kwani akiwa na hela si atanunua nyingine. Kwa nini atake vya gharama ambavyo hana uwezo wa kuvitafuta? Je ni ili ajionyeshe kwa wengine? Maana wanawake wengi wanapenda mwonekano zaidi na status kuliko kuwa wake. Wanataka mapete, mamgauni, masherehe makubwa wanakuwa exited nayo kuliko kuwa wake bora kwa waume zao. Shame!
 
Baada ya kuwaza hayo, naona swala la pete ni tamaduni ya kigeni ambayo tumeichukua toka kwa wenzetu. Nadhani kila kabika lina tamaduni zake ambazo pengine hatuzijui. Ikiwa pia ni pamoja na mavazi, vyakula na mengine mengi yanayohusu sherehe za ndoa.
 
Hahaaa wanawake bana mawazo yao sometimes mmh.....kweli tuishi nao kwa akili
 
Ni heshima n kumuonyesha kwamba pete yenye gharama ndio hadhi yake kwamaana yeye ni wa gharama kwako.

Upendo sio kiunganisho pekee kwenye mapenzi kwa watu wapendanao bali ni heshima,uaminifu ,kujaliana ndio muhimu mtu kama unamjali unampa vitu vya gharama.

Sio vitu visivyo vyagharama bhana msitutishie kama hamtaki kuoa basi humu mliringaga tu mbona tumeolewa tuna mapacha mfululizo kama shule mbegu zenu mmebakiwa nazo
Pete ya gharama Ni ya Nini wakati hata bikira sijakukuta nayo!?
 
Maisha nidhamani wewe hakuna mtu atapenda awekewe pete mkononi ya 23000seriously mie pete yangu ya uchumba ni ya gharama .

Intake kama mwanaume ambaye hana hela anakusanya kwandugu zake ifike 150000tsh ili amvishe mtu pete nzuri ya hadhi maana anamuheshimu wewe unahela halafu unamdharau mchumba wako kwa kumvisha pete ya 23000tsh seriously ??

Acha madharau na nyie wale wanaompa kichwa huyu sio fresh.
Ataishi single kama akiwa hayupo serious.
Dhamani [emoji735]

Thamani[emoji3581]

Hivi unavyoliandika hilo neno ndivyo linavyo tamkwa?! Mnakera nyie vilaza wa shule za kata!
 
Watu tumetofautiana , sioni kama pete ni big deal hivo hadi kucomplain eti bei rahisi,kama kweli mnapendana hata ya 10k tu inatosha bana, tatizo wadada tunapenda show off na kutambia marafiki,like hii pete babe wangu alinunua mil 3 hii, mmh for what[emoji848]
Ni kweli kabisa. Ila kwa story ya jamaa hapo amenyoosha maelezo kuwa alikuwa anakuja kumpatia pete nyingine huko mbeleni. Labda angefanya kumhoji taratibu na kwa upole kuwa mbona ametumia pete ya madini dhaifu ambayo yanaweza kumdhuru.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Dhamani [emoji735]

Thamani[emoji3581]

Hivi unavyoliandika hilo neno ndivyo linavyo tamkwa?! Mnakera nyie vilaza wa shule za kata!
Acha dharau mtaachwa na hiyo mikojo yenu muwe mnakojolea malaya tu haya na mashoga .
Kwani siumeelewa
 
Mimi ninavyoona kijana na huyo binti ni watu wawili tofauti. Hata mkifunga ndoa haitadumu. Ni vema kila mtu atafute mwenza wanaoendana.

Binafsi yangu kuliko kunivalisha lipete linalopauka la 23,000 ni heri ukaninunulie pete ya silver unapata nzuri kabisaa gram 3 kwa 45,000 tu.
 
Pete ya gharama Ni ya Nini wakati hata bikira sijakukuta nayo!?
Kwani vanessa rotimi alimkuta bikra??
Cheki hiyo pete amemuonesha ni wa thamani na anampenda ukimpenda mtu wako unamthamini .
Lulu je majizo kamkuta bikra ila umeona anavyompa vitu vya gharama.
Ni upendo nyie humu niwachungu bakini n mikojo yenu
 
Sio kweli kwamba walivalishwa dhahabu ndio wanathaminiwa sana. Sio kweli hata kidogo. Mimi mke wangu nilimpa pesa nikamwambia nina pesa hiyo kanunue pete ipime vizuri yoyote utakayochagua.

Kaenda kanunua, haikuwa ya dhahabu. Leo tuna miaka 12 kwenye ndoa. Wanaweke wengi wanapenda waonekane wanathaminiwa zaidi kuliko thamani wanayoweza kutoa maisha haya au hata pengine thamani waliyonayo. Hii sio sawa.

Kama ana akili vizuri na anayajua maisha atavaa tu pete yoyote. Kwani akiwa na hela si atanunua nyingine. Kwa nini atake vya gharama ambavyo hana uwezo wa kuvitafuta? Je ni ili ajionyeshe kwa wengine? Maana wanawake wengi wanapenda mwonekano zaidi na status kuliko kuwa wake. Wanataka mapete, mamgauni, masherehe makubwa wanakuwa exited nayo kuliko kuwa wake bora kwa waume zao. Shame!
Harusi yangu haikuwa kubwa sikuvaa gauni la harusi lililozidi laki tatu na wala ukumbi haukuwepo ilikuwa kawaida hivi tumeenda sehemu nzuri tu tukaagiza mabufee manne matano nawatu wapo kumi na tano tu marafiki ndugu wazazi/mzazi basi .
Sendoff haikuwepo mahari tu ndio ilitolewa basi waleo nipo na baba J basi.
 
Mi nilimvalisha ya buku jero, nilinunua Mwenge kwa muuza urembo. Alifurahi sana, kwani aliamini amepata mpenzi wa kweli atakayefanya naye maisha.

Hakuhitaji thamani ya pesa kwenye Pete. Alihitaji thamani ya pendo langu kwenye maisha yetu
Mimi mbona sikumvalisha? Nilimtia mimba kama sign of engagement
 
Pete ya bati jamani si bora asingemvisha pete tu. Angejikaga akapata tetanus akafa angemuoa nani. Mwanaume angempa ukweli mwanamke basi
 
Back
Top Bottom