moyafricatz
JF-Expert Member
- Nov 27, 2015
- 2,904
- 4,902
MDADA - "Hi Nimevalishwa pete ya uchumba mwezi wa 6. Nilifurahi sana sababu sikutegemea. pete haina hata miezi 2 imeanza kupata kutu. Hata marafiki zangu chuo wameanza kunicheka kuwa nimevalishwa pete fake.
Kuna rafiki wa mchumba wangu nimeongea nae ameniambia pete yangu ni ya elfu 23. Nimejisikia vibaya sana na kujiona sina thamani baada ya miaka yote hiyo ya mahusiano anakuja kunivalisha pete ya elfu 23? Ameshindwaje hata kutafuta pete ya laki?
Ingekuwa tofauti kama angekuwa hana pesa lakini mwanaume ana kazi nzuri tuu na ana pesa. Nimemuuliza kuhusu bei ya pete ameniambia naangalia pete au naangalia ahadi zake kwangu kama zitatimia? Mimi naona pete inaonesha jinsi gani ananipenda na kunithamini. Naona kama hajajipanga hata kunioa.
Sasa amenivalisha pete ya elfu 23 kunilea ataweza kweli? Mimi nimemaliza chuo sahizi na graduation yangu inakuja ila naona yeye anapambana kupanga harusi ikamilike na hawazi hata sherehe yangu ya graduation inayokuja. Nashukuru amenifikiria kunioa si unajua kazi hakuna ukitoka chuo unaenda nyumbani? Bora mimi siendi nyumbani naoelwa ntakuwa na kwangu.
Lakini sasa kwa hii pete naona kama hana mzuka wa kunioa kwa nini anipe pete ya elfu 23?
Mimi sio mwanamke ninaetaka makubwa lakini natamani thamani yangu iwe inachukuliwa kama ilivyo sio kupewa vitu vya bei rahisi.
Kama pete kanunua ya elfu 23? Unafikiri gauni ataweza kunishonea ninalotaka kwa kina kenny the brand? Au ndo nitakodiwa kigauni cha bei chee? Make up jee nitapakwa wapi? Unafikiri hii ni ishara naoneshwa kuwa mwanaume niliyenae sio sahihi? Ni mbahili? Au ni mtu wa kutaka viti fake fake? Nisaidie mawazo yako"
Share na wengine
Update:
Jamaa aibuka kujibu mapigo, ni yule aliyelalamikiwa na mdada kumvisha pete ya shilingi elfu 23,000
JAMAA - "Naandika nikiwa nimetulia lakini naomba nimjibu hapa huyo mchumba aliyedharau pete yangu. Ni kweli nilimnunulia pete ya elfu 23. Lakini sikutaka kumpa pete ya gharama kwa sababu nilikuwa na mipango yangu mingine. Nimeagiza pete zetu za ndoa na pete zake zitakuja pete 2 ya ndoa na ya engagement.
Kwa hayo aliyokuandikia sijui kama naweza kuendelea na shunguli za kumuoa mwanamke kama huyo. Fikiria amemaliza chuo. Ameenda kwao kujiandaa na sherehe zinazokuja. Hajataka hata tukae tufikirie yeye anafanya nini baada ya shule kama ni biashara au tutafute kazi. Mwanamke anawaza vitu vya gharama tuu.
Alivokuwa chuo alikuwa ukimtoa out anataka mwende sehemu za gharama gharama tuu kama sio mahoteli makubwa basi atataka mwende sehemu za bei ghali ili ajipigishe picha apost wiki nzima. Alianza kuja na marafiki zake ukiwarudisha anakununia siku nzima hata mlichopanga kwenda kufanya hamfanyi.
Hapo nimeona anawaza magauni ya mamilioni anasahau kama kuna maisha baada ya hilo gauni la milioni. Anataka akapakwe make up sehemu ambayo hata ukoo wao wote hawawezi kutoa hiyo hela.
Wanaume wenzangu mngekuwa ni nyinyi mna mwanamke wa aina hii mngefanya nini? Nimechoka, Nilikataliwa sana kutembea na vitoto vya chuo mimi nikawa najiwazia natafuta mke acha nitafute mwanamke mdogo mdogo nitamfundisha maisha mwenyewe nakuja kukutana na mtu wa aina hii.
Anataka mambo makubwa ambayo hana uwezo nayo. Alikuwa akitaka kutoka chuo hata kwenda kariakoo anaomba nimpeleke au nimpe hela ya uber. Nadhani siwezi kupanga maisha na mwanamke wa hivi.
Pete nimeshaziagiza zimenigharimu pesa nyingi sana na zimeandikwa tarehe za ndoa na ya engagement imeandikwa tarehe yake ya engagement sijui hata nitazipeleka wapi. Nimechoka kuendeshwa na mtu asiyechangia hata chupi yake mwenyewe"