Binti kamaliza form 6 na ndoto za kusomea udaktari kwa matokeo ya Division 1 ya 9; Physics C, Chemistry C, Biology C, Maths C, amekosa mkopo

Sio fake Kwa sasa BAM unaweza kufaulu kwa grade yoyote ile had A unapata ukifaulu na sio kuandikiwa S
Hizo credit kwenye Mathematics ni fake kwa sababu combination ilikuwa ni PCB na Maths alisoma kama subsidiary ambayo akifaulu huwa ni S na si zaidi ya hapo ila pungufu ya hapo huwa ni F! Usitudanganye hapa!
 
1 point 6 anapata,tena PCB
Labda kama course imejaa,kwa maana ufaulu Mwingi Wa 1.3 mpaka 1.5
Aopt Course Nyingine,Mkopo Chap
Hivi huwa mnasoma vizuri kweli mada,ni wapi kasema binti ana 1.6?
 
Acha uongo,mbona allocations za mikopo bado hata deadline haijafika?na pia udaktari ni unapewa mkopo tena 100%

Sijasema uongo, nimepewa maelezo nakaona sielewi heri nije kwenu kwa ushauri
 
Uko sahihi BAM siku hizi unawekewe credit
 
Nadhani kuna kitu hajui kuhusu mikopo, kwanza majina ya mikopo kwa mwaka huu bado hayatolewa, na kwa ufaulu wake mkopo atapata 100% lakini kwa vyuo vya private itabidi aongezee ada ambayo pamoja na kupata mkopo ataongezea kama mil 2.5+, ambayo nadhani hawezi kuimudu.

Mshauri aombe UDOM, awamu ya pili, kama akikosa hapo basi aombe kozi nyingine ambayo anaweza soma, au aende kwenye taasisi nyingine za ufhadhili kama MO foundation.
 
Kwahio BAM ina A ?
Na Je PCB Ukipata AAF na BAM A hapo una point ngapi ? Je wanaweza wakaacha hayo masomo yako principal na wakachukua hili subsidiary na ukawa na point 3 ?

Total Confusion.... Anyway kila zama na vitabu vyake....
 
Hiyo ipo tu lakini kwenye ufaulu wa kombinesheni haihesabiwi. Zinahesabiwa zile za PCB tu. Haiongezi wala kupunguza point zako.
 
Aliye pata division 1 ya PCB anakosaje mkopo? na wakati bado kuna second na third selections zinakuja mwezi September?
 
Amekosa udahili au ufadhili? ninachojua yametoka matokeo ya udahili,round ya pili imeshafunguliwa.aombe tena.ajaribu na vyuo vya private
 
Amekosa udahili au ufadhili? ninachojua yametoka matokeo ya udahili,round ya pili imeshafunguliwa.aombe tena.ajaribu na vyuo vya private
Ada ya private kwa maelezo haya sidhani kama ataweza, mkopo anawezapata lakini ada ya private ni mil 5+, pamoja na kupata mkopo itabidi aongeze ada ambayo hatamudu.
 
Mambo yako tight sana siku hizi..... Div. 1.9 PCB siku hizi sahau kupata kozi za afya,siyo udaktari tuu hata ufamasia,nursing,maabara...

Cha msingi hapo ajaribu kuomba nursing na maabara anaweza kupata..
 
Amekosa udahili au ufadhili? ninachojua yametoka matokeo ya udahili,round ya pili imeshafunguliwa.aombe tena.ajaribu na vyuo vya private
Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…