Binti kamaliza form 6 na ndoto za kusomea udaktari kwa matokeo ya Division 1 ya 9; Physics C, Chemistry C, Biology C, Maths C, amekosa mkopo

Hata vyuo binafsi hawezi kupata udaktari kwa Division one (point 9) kwa mwaka huu.

Halafu hii dhana ya vyuo binafsi na umma huwa nyinyi mnaipata wapi katika zama hizi za sasa?

Hivi mnaelewa jinsi udahili ulivyo tight kwenye kozi za afya zama hizi?

Yaani unaweza ukawa na division one na bado usipate chuo chochote kwa kozi yoyote ya afya mwaka huu.
Kwa vyuo binafsi anawezapata.. nina rafik ang kamaliza form six mwaka huu na alipata two ya kumi. But kaomba st. Joseph na amepata nafas ya kusoma MD. sema issue kubwa ni Ada. But kwa ufaul wake uwezekano wa kupata nafas ni mkubwa xn. Issue ni Ada tyu
 
Mimi naomba aombe ualimu.Akasome ualimu DUCE.Akasome Bed physics.Atapata mkopo asilimia zote tu.Kama ana ndoto ya udaktari basi aombe private kama St joseph',Udom (MD),Bugando ,Kairuki anaweza kupokelewa kule.Mwenyezi mungu amtangulie.

NB;Aombe Chuo mapema maana kama huna Chuo mkopo watakuwekea wapi?
 
Huyo binti kamaliza mwaka gani form six?

Hiyo division 1.9 form six
Hawezi pata chuo Cha Udaktari Cha Serikali Kama Muhas

Then Allocations za mkopo hazijatolewa kwa mwaka. 2022/2023 sasa unasemaje kakosa mkopo toka helsb

Wewe mama D

Kabla ya kupost habari tumia akili
true
 
Mweee mweee mweee, huku sii kufelishana tuu jamani
Hakuna kufeli wewe so unaona wanapasua madogo kuliko enzi za nyuma....walichofanya wametoa marks nyingi kwa continuous assessment ya mitihani ya shulen.Hivyo dogo akifaulu kule shuleni mtihani wa mwisho anafaulu kwa maana wameupa weight ndogo si kama zamani
 
Mleta mada una uhakika na hii habari yako?
Wanafunzi ndio wako busy mwezi huu wa August kuomba chuo, udahili bado unaendelea, round ya kwanza imetoka, round ya pili ndio wako kwenye mchakato, sasa huyo binti anawezaje kuomba mkopo wakati wa udahili unaendelea?

Bodi ya mikopo bado hawajafungua rasmi dirisha la mikopo kwa wanafunzi wapya, vipi huyo binti keshajua amekosa mkopo?

Mpaka sasa, awamu ya kwanza imetoka, mwanafunzi mwenye ufaulu wa chini kabisa aliyepata kozi ya udaktari ana Division 1 (point 7), huyo binti mwenye Division 1 (Point 9) kapataje?
😂😂😂😂
 
Hizo credit kwenye Mathematics ni fake kwa sababu combination ilikuwa ni PCB na Maths alisoma kama subsidiary ambayo akifaulu huwa ni S na si zaidi ya hapo ila pungufu ya hapo huwa ni F! Usitudanganye hapa!
Siku hizi unawekewa credit km A,B n.k

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimi naomba aombe ualimu.Akasome ualimu DUCE.Akasome Bed physics.Atapata mkopo asilimia zote tu.Kama ana ndoto ya udaktari basi aombe private kama St joseph',Udom (MD),Bugando ,Kairuki anaweza kupokelewa kule.Mwenyezi mungu amtangulie.

NB;Aombe Chuo mapema maana kama huna Chuo mkopo watakuwekea wapi?
Bugando hapatiiiiii

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Habari za jioni wakuu mabibi na mabwana

Huyu binti namfahamu tangu akiwa mtoto. Anatoka kwenye mazingira magumu kuliko ngumu wenyewe.

Hamjui baba yake mzazi, hajawahi kumsikia wala kumuona.

Mazingira ambayo mama yake hawezi kumiliki hata simu ya elfu20, hawezi lipa kodi vyumba2 vya elfu 60 uswahilini kwetu huku, hana uhakika wa kulisha watoto wake milo miwili kwa siku lakini amepambana hadi binti kafika kidato cha sita kwa msaada wa serikali na amepata hayo matokeo hapo.

Alipofaulu kidato cha nne kwenda kidato cha tano mkoani hata nauli wachana na Ile ada ya elfu70 ya Magufuli ilikua shughuli kubwa. Wakati wa kufunga shule ndio ilikua hadi walimu wapige simu kwa namba atakazowapa za ndugu na jamaa ndio arudi njiani. Yaani kwa kifupi amekua kwenye mazingira magumu nyakati zote shuleni na nyumbani

Pamoja na kuwa amesoma shule zetu za serikali tangu chekechea hadi kidato cha sita na matokeo yake ni hayo hapo, amejitahidi kadri ya uwezo wake kwa lengo la kuja kusomea masomo ya utabibu kama udaktari au maana ya lakini leo nimeumia kidogo baada ya kumkuta kajikunyata kwa huzuni baada ya kukosa ufadhili au mkopo wa serikali kwa kozi hizo ambazo ada zake zipo juu

Nimewaza nikaona nije hapa jukwaani kwa wajuzi wa mambo maana najua hapa kuna wazoefu, walimu, wasomi, washauri, wazazi wenye mapenzi mema labda Huyu binti anaweza saidika

Mtoto wa mwenzio no mtoto wako, natanguliza shukrani

Nawasilisha[emoji1666]

Cc Dada Ummy Wizara ya Afya Tanzania
Majibu ya maombi ya mkopo yametoka? Je aliomba mkopo kweli? Kwa jinsi unavyoeleza ni km wewe na yeye hamuujui mchakato wa kuomba mkopo. Kwa sasa mkopo hauangalii unosoma fani gani bali vigezo vya kupewa. Kwa kumsaidia mwambie afike ofisi za Bodi ya Mikopo akajieleze.
 
Kajuaje kama kakosa wakati Loarn Board hawajatoa walipata mkopo?,au aliombq mwaka jana 2021?
 
Majibu ya maombi ya mkopo yametoka? Je aliomba mkopo kweli? Kwa jinsi unavyoeleza ni km wewe na yeye hamuujui mchakato wa kuomba mkopo. Kwa sasa mkopo hauangalii unosoma fani gani bali vigezo vya kupewa. Kwa kumsaidia mwambie afike ofisi za Bodi ya Mikopo akajieleze.

Anaenda kusomea mazao bahari
 
Back
Top Bottom