Binti wa Dkt. Wilbert Kleruu atoa ya moyoni

haji rashid,
Kwa hiyo ni haya haya ya leo ya Babu Seya kama tunavyosikia?

Nilisikia huko Z´bar pia Karume na wanawake ilikuwa ni sehemu ya sifa zake za kujivunia, leo hii hayasemwi. Jumbe niliwahi kusikia akimfunga mtu Kagera kwa sababu ya mwanamama. Kawawa naye kijogoo akiwinda watoto wa shule kila ziara!

Leo hii ni mashujaa. Labda siku tukiambiwa ukweli wa wanadamu hawa tutaweza kuwapa hukumu wanayostahili.

Ni vibaya kumtakia mwenzako kifo lakini pia Viongozi wanapojiona wana kinga ya yote na wanaagiza watu wapigwe tu yaonyesha udhaifu mkubwa wa akili zao.
 
haji rashid, Ni kweli Kleruu alifanya makosa na hata Mwimindi pia maana kuua si haki, ni kosa. Lakini nimependa maneno ya binti yake juu ya kusamehe. Madaraka Nyerere alimtafuta na kuwa pamoja na mtoto wa Idd Amin na hadi sasa ni marafiki. Mtoto wa Idd Amin alikuja hadi Butiama. Nawe kama familia mkutane mmalize suala hili ili wote MSAMEHE NA KIUSAHAU. Nimeyapenda sana maneno ya binti huyu, ya kiutu uzima hakika!
 
Tukitaka Minakasha kama hii ilete faida kwa wasomaji na wafuatiliaji lazima tuache kuingiza hisia za Kiimani. Maana naona kwa sasa mada imetawaliwa na hisia za Imani. Hata hivyo siko zote mtu akitimiza wajibu wa kazi yake kwa ukamilifu huitwa Dikteita, hasa kwa watu majeuri wasiopenda kufuata sheria. Haya ya kusema alimtaka asilime siku ya Christmass siyo ya kweli ndiyo maana waandishi wengine wanasema hawajapata ushahidi wa kutosha kulidhibitisha hili.
 
kleruu amevuna matokeo ya siasa za Ujamaa na Kujitegemea

Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea hakuielekeza hivyo. Hizo zilikuwa vurugu za Kleruu tu na ndizo zilizosababisha mauti yake.
 

Well said. Ukweli ni kuwa MAREHEMU ALIKUWA CHANZO CHA KIFO CHAKE MWENYEWE. Frankly speaking Mwamwindi alijitahidi sana kumvumilia. Lakini kama bianadamu alifika mwisho wa kuvumilia akaona LIWALO NA LIWE! Hata mtoto mdogo pamoja na kujua hana nguvu anaweza hata kujitahaidi kukuuma anapoona sasa ni too much! Kleruu alitawala kwa mkono wa chuma huku akitumia madaraka yake vibaya hata kwa mambo ya binafsi. Hakuna mwanaume yeyote aliyekamilika anayeweza kukubali kudhalilishwa kiasi kile nyumbani kwake mbele ya mkewe na nduguze halafu atulie kimya. Mwamwindi alifika ukomo wa uvumilivu ndio maana hata baada ya kumuua alimpakia kwenye gari na kuliendesha mwenyewe hadi polisi kukabiliana na mkono wa sheria. Ingekuwa hukumu hii inatolewa leo Mwamwindi angeshinda kwa maana ya mazingira na sababu ya tukio lenyewe!
 

Kuna mzee mmoja huku Iringa nlisikia akisema haya haya alihusisha kifo kile na gombania mwanamke na sio masuala ya kilimo wala shamba...
 
Hii sotry sio ya kweli,tafuteni sababu hasa na mfahamu kilichotokea
Tupe wewe hiyo unayoijua.


"kama jambo halina jibu sahii,jibu lenye busara lipo katikati ya ndio na hapana.NALO NI UKIMYA"_DAN BROWN THE DA VINCI CODE
 

sipo upande wowote wa hii case ila deffence ya provocation haiwez kusimama kwa sababu Said alitoka umbali mrefu kuifuata bunduki na aka ikoki......ule umbali ungemtosha ku cool down his temper, afu ukisoma ile case kleruu alikua na kauli chafu sana
 
Dr. Kleruu alipofika shambani kwa Mwamwindi asubuhi ile kitu cha kwanza akamuuliza "mbona unafanya kazi siku ya Krismasi"?

That right there tells you that Mzee Kleruu alikuwa na psychological problems and was calling for his fate.
We umeamka Jumapili ya Xmass kwenda ku enforce ma policy ya nchi kama Mkuu wa Mkoa, halafu unamwambia mwenzako kwa nini unafanya kazi siku ya Krimasi!

Kwa hiyo tunategemea labda yeye kaja shambani kwa mwenzie kula Krismasi, tatizo kaja na fimbo, akawa anamchoma choma mkulima wakati wa maongezi. So obviously hata yeye hakuja na nia njema ya kula Xmass.
 
Emu tuelezeni ukweli ni upi maana si wengine hata hatuelewi ila KWANI HAMNA SHERIA YA KUMSAFISHA MTU ALIYEPEWA HUKUMU YA KUNYONGWA NA AKANYONGWA ILA ILIKUWa hukumu ya kutengenezwa?kwa huku tunaona sanaa kuwa labda mtu alinyongwa miaka hata kumi kumbe kuna shinikizo la siasa au kiongozi then yule mtu anaachia huru kuwa alinyongwa kwa kuonewa..familia yake inalipwa, na mwili unatolewa pale kwenye makaburi ya wanyongwaji kupelekwa kwa kuzikwa ba nduguze...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…