Binti wa Dkt. Wilbert Kleruu atoa ya moyoni

Binti wa Dkt. Wilbert Kleruu atoa ya moyoni

Mie nilivyosikia, kileruu, alimchukua mke wa huyo Mwamundi, tena akawa anamkejeli mwenye mke wake
Ni sehemu pekee inayofichwa na wanahistoria kuhusu uchafu wa huyu mzee mm personally nilisimuliwa na babu yangu mazuri na mabaya ya huyu anaitwa Kreluu intact alikuwa muonevu na mbabe wa kijinga. Kwa sehemu kama Iringa na wakati ule alijichanganya angeenda kuleta uhuni wake Moshi sio Iringa
 
Kwa maelezo nliyosimuliwa na Marehemu Bibi Yangu Miaka mingi kidogo, Bwana Kreruu alikua mkatili sana, bibi anasema siku ambayo mwamwindi alimpiga risasi taharifa zilivuma kwa haraka maeneo ya Iringa mjini na viunga vyake. Bibi anasema baada ya tu taharifa kuzagaa wakinamama wa kihehe walisogea kwenye vibongonyera (Pembe za Nyumba) wananena (Wanasema au kuomboleza) maneno ya kihehe baada s kunena hayo maneno wanapiga vigeregere.

Bibi anasema kwa wakati huo, ilikua ni kama sherehe kreruu kuuwawa, Mwamwindi kwa jamii ya wahehe alionekana kama Shujaa na Mkombozi dhidi ya udhalimu wa kreruu.

Ubaya ni kwamba Bibi Alifariki, ila nitarejea siku moja kwa wazee Kalenga kuweza kupata historia zaidi ya nini kilichotokea.
Hii historia huwezi ipata Kalenga,kalenga uliza kuhusu mkwawa utaelezwa. Mwamwindi nenda isimani ndo watamueleza vizur. Nimewahi kuishi kalenga kwa miaka 3 hawajui lolote kuhusu hilo
 
Mkuu wa Mkoa wa iringa Dr. Kleruu alidhani kila mtu ni mkristo kwa kumlazimisha Mzee Saidi mwamwindi aache kulima ili asherehekee Krismas matokeo yake ndiyo hayo! mauaji dhidi ya binaadamu wenzetu hayakubaliki! lakini kutumia mamlaka uliyopewa na wananchi kuwadhalilisha raia zako pia haikubaliki!
Uamuzi wa binti wa dr. Kleruu kutaka kujenga mahusiano na familia ya Marehemu Saidi Mwamwindi ni uamuzi wa busara ambao kila mpenda amani atayakaribisha! ila kifo cha Kleruu ni fundisho kwa kila dikteta na kiongozi anaeongoza kimabavu!

Kisa kizima cha mauaji ya Dr. Kleruu gonga hapa: Raia Mwema - Kwa nini mkulima Mwamwindi alimpiga risasi RC Dk. Kleruu? VII
Hii habari ya Krismas ndio naisikia kwako.
 
Dah huyu Kleruu inaonekana Israel alikuwa anamwita asee. Na huyu mzee Mwamwindi nae inaonekana aliamua kujitoa kwaajili ya wenzake.

Kumbe Tanzania kuna historia ambazo sisi kizazi cha .com hatuzifahamu.
 
Historia inatukumbusha na kutufundisha mambo mengi sana.
 
Mkuu wa Mkoa wa iringa Dr. Kleruu alidhani kila mtu ni mkristo kwa kumlazimisha Mzee Saidi mwamwindi aache kulima ili asherehekee Krismas matokeo yake ndiyo hayo! mauaji dhidi ya binaadamu wenzetu hayakubaliki! lakini kutumia mamlaka uliyopewa na wananchi kuwadhalilisha raia zako pia haikubaliki!

Uamuzi wa binti wa Dr. Kleruu kutaka kujenga mahusiano na familia ya Marehemu Saidi Mwamwindi ni uamuzi wa busara ambao kila mpenda amani atayakaribisha! ila kifo cha Kleruu ni fundisho kwa kila dikteta na kiongozi anaeongoza kimabavu!

Kisa kizima cha mauaji ya Dr. Kleruu gonga hapa: Raia Mwema - Kwa nini mkulima Mwamwindi alimpiga risasi RC Dk. Kleruu? VII
Ndio ulivyodanganywa?
Dr. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake - JamiiForums
 
Hii sotry sio ya kweli, tafuteni sababu hasa na mfahamu kilichotokea
Sasa wewe unayebisha ndio utoe ukweli maana huwezi kubishia kitu usichokijua other wise kama huamini una kaa kimya. Lakini kubisha na kuwataka hao hao wanaokuambia watafute ukweli wakati wewe mwenyewe huna huo ukweli ina kuwa haina maana.
 
Mungu amweke Dr Kleruu Mahali anapositahili
... yaani huyo Mungu kila siku anabadilisha mahali anapoweka marehemu? Nachojua akishaweka mtu pahala pake ni mara moja tu na habadilishi. Kleruu alishawekwa anapostahili siku ile ya Desemba 25, 1971 na hatobadilishiwa kikao kamwe!
 
it was very poor judgement kwa upande wa mzee mohamed kwani hata kama alifanya hivyo death penalty was not appropriate. i beleive yeye alipewa full access to the court of law and receive fair justice.
Yes!!! Kesi iliamuliwa kisiasa na kwa hasira!!! Imagine raisi anasign hukumu ya kifo wakati alikuwa mgumu sana kisign!!!! Hasira hasara kwa both sides. Hasira ilimponza Mwamwindi na hasira hiyo hiyo ikahukumu kifo chake!! Very sorry!
 
Kwa miaka sita sasa, tumekua na ma Kleruu wengi mno. On the flip side, akina Maalim Ustaadh Mkulima Mzee Mwamwindi hawapo
 
Kwa miaka sita sasa, tumekua na ma Kleruu wengi mno. On the flip side, akina Maalim Ustaadh Mkulima Mzee Mwamwindi hawapo
Masikini wameamua kukaa kimya tu. Waliamua ku-lay a low profile!!! Na nadhani waliamua vizuri maana hasira dhidi ya baba yao ingewakumba wangeishia pabaya.
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Kwa miaka sita sasa, tumekua na ma Kleruu wengi mno. On the flip side, akina Maalim Ustaadh Mkulima Mzee Mwamwindi hawapo
Wapo na wanaishi block 41 moroco
Wana utata na msimamo fulani,inawezekana
Hiyo ni asili yao

Ova
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Back
Top Bottom