Binti wa Dkt. Wilbert Kleruu atoa ya moyoni

Binti wa Dkt. Wilbert Kleruu atoa ya moyoni

Mkuu EMT, kwanza asante kwa hii kitu!, mimi ni interested party nilisoma darasa moja na mtoto wa Kleruu aitwae Edwin pale Ilboru!.
Jamaa was humble and down to earth!.

Mwamwindi na mhindi mmoja ndie watu pekee Nyerere alisaini death warrants zao za Capital punishment kutekelezwa, nasikia katika utekelezaji ilisumbua, baada ya kunyogwa mara ya kwanza, hakunyongeka na kufa, then ilibidi kitu fulani kifanyike ndipo alikufa, mtu akishahukumiwa kunyongwa, ukinyongwa bila kufa unapaswa kuachiliwa, maana utekelezaji wa adhabu ilikuwa ni "kunyongwa"

Nasikia ikatolewa order, sio tuu anyongwe, bali ni "anyongwe mpaka afe!", from then hukumu ya kunyongwa inapaswa kuandika "Anyongwe Mpaka Afe!"

Kiukweli hukumu hii ni "barbaric!" thanks God, we'll do away kwenye katiba mpya!, japo kwenye rasimu bado ipo!.
Pasco.
Pasco original huyu [emoji1666][emoji1666]
 
Kwa maelezo nliyosimuliwa na Marehemu Bibi Yangu Miaka mingi kidogo, Bwana Kreruu alikua mkatili sana, bibi anasema siku ambayo mwamwindi alimpiga risasi taharifa zilivuma kwa haraka maeneo ya Iringa mjini na viunga vyake. Bibi anasema baada ya tu taharifa kuzagaa wakinamama wa kihehe walisogea kwenye vibongonyera (Pembe za Nyumba) wananena (Wanasema au kuomboleza) maneno ya kihehe baada s kunena hayo maneno wanapiga vigeregere.

Bibi anasema kwa wakati huo, ilikua ni kama sherehe kreruu kuuwawa, Mwamwindi kwa jamii ya wahehe alionekana kama Shujaa na Mkombozi dhidi ya udhalimu wa kreruu.

Ubaya ni kwamba Bibi Alifariki, ila nitarejea siku moja kwa wazee Kalenga kuweza kupata historia zaidi ya nini kilichotokea.
Aiseeee [emoji134][emoji134] vipi uliwapata wazee wa kihehe mkuuu??
 
Mkuu Von tosy, nadhani sio jambo zuri hata kidogo kuzungumzia juu ya "unayoona mabaya" ya mtu aliyeishafariki kwa sababu yeye tena hana nafasi ya kuja kujitetea kama angaliweza kufanya hivyo angalikuwa hai na hapo ni kukosa "absolute justice", juu ya yote marehemu anao watu wa karibu naye ambao kwa namna moja waliguswa na pengine wataendelea kuguswa na msiba wa mpendwa wao pale watakaposikia marehemu akitajwa katika njia ya "ubaya", busara inataka tuyaeleze mema yake ili nasi tujifunze na kuhusu mabaya tumuachie Mungu pekee na pia zingatia hakuna mtu mkamilifu.
Ukweli ni kwamba, kama alivyowahi kusema Mzee Ally Hassan Mwinyi, binadamu yeyote hapa duniani maisha yake ni kama hadithi, hivyo binadamu tunatakiwa kuacha hadithi nzuri hapa duniani,short of that ni ngonjera tuu kama za akina Adolf Hitler au Iddi Amini dada...
 
Hivi watu wameanzia wapi hadi kuanza kutukumbusha mambo ya 43 years ago? Can someone tell me how do we go from mourning the victims of MV Nyerere to discussing nineteenth centuary communism?
Kuna aliyekushikia bunduki uje kwenye huu uzi??
 
Ni sehemu pekee inayofichwa na wanahistoria kuhusu uchafu wa huyu mzee mm personally nilisimuliwa na babu yangu mazuri na mabaya ya huyu anaitwa Kreluu intact alikuwa muonevu na mbabe wa kijinga. Kwa sehemu kama Iringa na wakati ule alijichanganya angeenda kuleta uhuni wake Moshi sio Iringa
Kama bado upo humu ndani mkuu hebu tunyoosheee maelezo kuhusu huyu RC, nini hasa lilikuwa tatizo lake hapo Iringa miaka hiyo? Ufuska? Ulevi wa pombe au ulevi wa madaraka?? Hebu funguka ili vijana wa kizazi hiki wajifunze...
 
Hii historia huwezi ipata Kalenga,kalenga uliza kuhusu mkwawa utaelezwa. Mwamwindi nenda isimani ndo watamueleza vizur. Nimewahi kuishi kalenga kwa miaka 3 hawajui lolote kuhusu hilo
Sasa una uhakika gani kwamba akienda Ismani ndiyo ataipata? Mbona wewe hujaipata? Halafu baadae akitokea mzungu akaiweka hii stori vizuri kwenye vitabu tunaanza kulia lia oooh mabeberu waongo oooh siyo kweli.... Yaani full ujinga tuuu....
 
Historia inatukumbusha na kutufundisha mambo mengi sana.
Sisi Waafrika ni full unafiki, yaani kujitokeza na kuweka sahihi historia ya matukio ni shidaaa.... Akijitokeza mzungu kuweka wazi hiyo historia pia ni shidaaa..
 
Sasa wewe unayebisha ndio utoe ukweli maana huwezi kubishia kitu usichokijua other wise kama huamini una kaa kimya. Lakini kubisha na kuwataka hao hao wanaokuambia watafute ukweli wakati wewe mwenyewe huna huo ukweli ina kuwa haina maana.
Ndiyo shida ya wabongo... Sasa subiri atokee mzungu aende huko Ismani na kuhoji na kuandika kitabu kuhusu hicho kisa sasa...
 
Kleruu TTC ni miongoni mwa vyuo bora kabisa vya waalimu wa sayansi kuwahi kujengwa.ilikuwa mwaka wa 1970 msaada toka Denmark
Usitudanganye mkuu, kwabahati nzuri Sana nimekaa hapo Kreluu TTC zaidi ya miezi miwili kwenye ile rest house yao!! Ni chuo Cha kawaida sana kimiundombinu Hadi mazingira hiyo ni 2014, Hata sehemu za michezo ni Kama Shule ya msingi flan tu!! Angalau hata Tarime TTC Wana viwanja vizuri!!

Kwangu Butimba TTC kilichojengwa 1938 kinabaki kuwa chuo Bora kabisa ambacho nimepata nafasi kuvishuhudia!!
 
Usitudanganye mkuu, kwabahati nzuri Sana nimekaa hapo Kreluu TTC zaidi ya miezi miwili kwenye ile rest house yao!! Ni chuo Cha kawaida sana kimiundombinu Hadi mazingira hiyo ni 2014, Hata sehemu za michezo ni Kama Shule ya msingi flan tu!! Angalau hata Tarime TTC Wana viwanja vizuri!!

Kwangu Butimba TTC kilichojengwa 1938 kinabaki kuwa chuo Bora kabisa ambacho nimepata nafasi kuvishuhudia!!
MKUU ACHA MASiHARA KABISA, HUIJUI KLERRUU WEWE, MIMI NIMESOMA SECONDARI HAPO, HIKO CHUO KILIFAA KIWE CHUO KIKUU,MAJENGO YAKE HAYANA TOFAUTI NA YA UDSM...HAPO COET MAANA NIMESOMA HAPO PIA,

UNAFANANISHA NA BUTIMBA HII KAMA SECONDARY?

1621634716853.png


KLERRUU NI HII HAPA CHINI NDIO UFANANISHE NA BUTIMBA? MIMI NIMESOMA SECONDARY YA KLERRUU , LABALATORY TULIKUWA TUNATUMIA ZA HIKI CHUO, NI ZA KISASA, MAJENGO ASILIMIA 90 NI GHOROFA, HADI MABWENI YAO... KIFUPI KINAZIDI VYUO VIKUU VINGI TU

1621635188124.png
1621635201980.png


1621635235992.png


HIZI ZA CHINI NI LABARATORY ZAO, SISI WA SECONDARY TULIKUWA TUNAZITUMIA NI ZA KISASA

1621635448441.png
 
Mkuu wa Mkoa wa iringa Dr. Kleruu alidhani kila mtu ni mkristo kwa kumlazimisha Mzee Saidi mwamwindi aache kulima ili asherehekee Krismas matokeo yake ndiyo hayo! mauaji dhidi ya binaadamu wenzetu hayakubaliki! lakini kutumia mamlaka uliyopewa na wananchi kuwadhalilisha raia zako pia haikubaliki!

Uamuzi wa binti wa Dr. Kleruu kutaka kujenga mahusiano na familia ya Marehemu Saidi Mwamwindi ni uamuzi wa busara ambao kila mpenda amani atayakaribisha! ila kifo cha Kleruu ni fundisho kwa kila dikteta na kiongozi anaeongoza kimabavu!

Kisa kizima cha mauaji ya Dr. Kleruu gonga hapa: Raia Mwema - Kwa nini mkulima Mwamwindi alimpiga risasi RC Dk. Kleruu? VI
Kwa kuiongezea tu, Dr. Kleruu alikuwa anatembea na mke mdogo wa Said Mwamwindi, na jamaa alikuwa anajua na alishawahi kugombana nae Mara kadhaa. Kleruu alikuwa anatumia cheo chake na Mwamwindi kama walivyo wahehe huwa ni watu wa kunyamaza Ila siku hiyo ndio ikawa mwisho wa dharau.

Jamaa alienda zake shambani kwake akiendelea na shughuli ndipo kleruu akamfuata shbani na kuanza kumharass na hayo Mambo kwamba hiyo no sikukuu why analika na Mambo kama hayo.

Hapo Mwamwindi alimwambia subiri nitakuonyesha, na alivyo mjinga, kleruu akabaki anamsubiri, ndipo jamaa alipoenda kuchukua gobole akamuwasha na kumpakia kwenye landrover yake na kumbwaga police central akawaambia askari kachukueni mbwa yenu , jamaa kwenda kucheki kwenye gari wakamkuta RC.

Actually Said Mwamwindi pia alikuwa ni mtu anafahamika sana sababu alikuwa ni mkulima mkubwa pale Iringa.

So kimsingi kifo Cha Kleruu kilifichika haswa lakini kimetokana na personal beef na haswa Kleruu alikuwa na tabia ya kumharass wahehe na kwa Mwamwindi alifikia Hadi kutembea na mke mdogo wa jamaa Ila alinyamaza tu.
 
Tukitaka Minakasha kama hii ilete faida kwa wasomaji na wafuatiliaji lazima tuache kuingiza hisia za Kiimani. Maana naona kwa sasa mada imetawaliwa na hisia za Imani. Hata hivyo siko zote mtu akitimiza wajibu wa kazi yake kwa ukamilifu huitwa Dikteita, hasa kwa watu majeuri wasiopenda kufuata sheria. Haya ya kusema alimtaka asilime siku ya Christmass siyo ya kweli ndiyo maana waandishi wengine wanasema hawajapata ushahidi wa kutosha kulidhibitisha hili.
Naona hujui kitu kuhusu Kleruu. Alikuwa mshenzi sana, but in short Kleruu alikuwa na personal issues kati yake na Mwamwindi. Kumbuka Mwamwindi alikuwa mkulima tajiri na alikuwa na mke mdogo ambae Kleruu alikuwa anatembea nae kwa kutumia cheo chake.

So hata hii ya kumfuata shambani waweza kujiuliza kwa nini RC mzima amfuate shambani mtu na ni sikukuu na yeye ni mkristo angeendelea na sikukuu? What was so special ilimpeleka shbani kwa Saidi?

Kumbuka alishataka kumnyang'anya Yale mashamba ayaingize kwenye villagization wakati yeye Said alikuwa amehangaika kuyafyeka mapori na analima miaka yote .

Kleruu alikuwa na issues na Saidi so alimprovoke although provocation alinitumia kama defense mahakamani ukishindwa kusustain kisheria.

It was too much for him akaona sasa huyu jamaa anamletea dharau. The rest ni story tamu maana alimpakia kwenye landrover nyuma akampeleka central police akawaambia kachukueni mbwa yenu. Jamaa wanaenda wanakuta RC .

It was too much hakukubali Ile dharau, mashamba yachukuliwe na serikali, ingali mapori yapo mengi tu, kwa nini wachukue ya kwake ambayo analima kila mwaka?

Mke mdogo achukuliwe, sasa na jamaa aamua ashinde zake shambani Tena anafuatwa na kejeli, hakuna mhehe atakayekuacha.
 
Back
Top Bottom