Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

Your Thread , , Is Pontentially Offensive,you Can Not Generalize In Such A Way.B'se Ladies Who Are Graduate Are Many, And You Have Not Yet Seen Enough Of It To Make Such Generalizations,,. It Also Adds Nothing To The Main Issues That You Raise Which Is Quite Good And Useful, . How We Open Our Pitch Matters.B'se We Can Put Off People Or Get Into An Engagement Before Even Start,. You Have To Appreciate The So Called Individual Difference,,,,,,. Kuwa Msomi Ni Pamoja Na Kukubali Kutokubaliana Na Wenzako,,, Katka Biashara Kama Hana Kipya Kwenye Hayo Makande Alichoongeza (game changer,) Basi , Nami Nasema Ni Lulu Iliyopotea, Lazima Tujifunze Kutokubaliana Na Wengine Bila Jaziba,,,.
 
Mkuu nakuunga mkono na miguu yote kwa pamoja. Ni hivi watu tunaishi bila kujua our purpose on this planet earth, tunaishi bila plans. Mtu anaenda shule kusomea let's iT hiyo hiyo uliosema hapo lakini hana lengo au motive au purpose yoyote baada ya kupata hiyo knowledge ni vipi ataitumia kuleta mabadiliko in our society and to make money for him / herself. Na ndo mana wachache sana ambao hata wakiingia kwenye biashara (baada ya kukosa kazi) wanafanya biashara zilizo opposite kabisa na miaka ya tabu, jasho na damu waliyoitumia kuipata knowledge hiyo chuoni.
Unaweza sema ameamua kuifanya biashara yeye aliyoiona ina fursa but najiuliza kama alikua na lengo hilo tangu mwanzo why hakwenda kusomea kitu kitakachoendana na biashara atayotaka kuja kuifanya instead of kupoteza muda kwny masomo ambayo at last hatakuja kuyatumia!.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani mwandishi wa Millard Ayo aliyeweka habari youtube na mwanzishi wa mada hii mmefanya kosa moja la kuchukua title, nimeangalia interview ile yote na yule dada siyo muuza makande,

Anauza chakula kwa ujumla, sema katika menu yake kuna siku ya makande, na ni aiku moja kwa week, sasa wamechukua hiyo na kuifanya title, ni kosa.

Pia yule kasoma project management, baada ya kukosa ajira si vibaya kuja na hiyo project ya catering siyo kosa, though anafanya out of passion.


Narudia kuna makosa ya uwasilishaji wa hii taarifa, yule ana biashara ya chakula kwa ujumla na anafanya delivery kwa wateja wake.
 
Unaweza ukaajiriwa ila ukawa unalipwa 25 million kwa mwezi,so be careful

Noma
Labda kama unalipwa kwa Euro/USD na inetegemea pia umejiweka vipi kwenye elimu? Sio una digrii ya bongo utake ulipwe 25m hiyo ni ndoto ya asubuhi hata kama HR ni basha wako!
 
hivi inakuaje umesom marketing na ukaamua kujiajiri kwenye biashara yako mwenyewe as market manager

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mi nadhani muda mwingine wazazi wanachangia watoto wao kufanya vitu wasivyovipenda. unaweza kukuta huyo dada toka mwanzo alipendelea kujiajir kwenye upishi lakin kwa sabab wazaz hawakupenda walitaka asome aje kuajiriwa benki wakamlazimisha matokeo yake ndio hayo anafanya kitu anachokipenda kwa elimu yake asingekosa kazi hata benki lakin huko siko anakokupendelea
 
Mtoto wako akikwambia baba sitaki shule nataka niwe mnyanyua zege na kufanya kazi za vibarua utamfanyaje, inabidi umuache eti kisa dunia inamgawanyo kwamba hata kukiwa na enjinia atahitaji vibarua, jibu hapana.

Kweli dunia ina mgawanyo wa watu tofauti ila tunachofanya ni kuelekezana tuwe kwenye ule mgawanyo mzuri kweli kutakuwa na waajiriwa na waliojiajiri ila upaande mmoja ndio unauwanja mkubwa was kutusua kimaisha so lazima tuelekezane huko ila haimaanishi kwamba wote wataenda huko kwasababu hata kwenda yenyewe sio rahisi kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niipi tafsiri yako ya kufeli na kufaulu, au kuelimika kiujumla.

Ni lazima ujiajiri kwenye fani yako ndio uwe umefaulu na kuelimika, he unajua power kiasi gani inahitajika ya kujiajiri kwenye fani yako je most of us from poor family tunayo iyo power.

Mtu umesomea HR ukajiajiri kwenye kufuga kuku iweje uwe umefeli nawakati unatatua tatizo la njaa, ukosefu wa virutubisho, ajira nk kwajamii na kujipatia mapato yako na mapato kwa selikari kivipi uwe ujaelimika.

Mwisho ieleweke misoto ya maisha tunayopitia sio yakitoto na haifanani chakwanza ni unaangalia mapato yako then ndio jamii inafaidika vipi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tafsiri yangu ya kufeli ki elimu ni kushindwa kuona fursa zilizopo katika eneo uliloamua ku invest muda na fedha kwa ajili ya kujifunza.
 
Hv hizi kande anazouza huyo mdada msomi zina tofauti gani na kande zetu za kawaida? embu mtuekee picha za hzo kande au mahal uyo bibie anauza tukatest ladha
 
Yule dada wa kande wa Mwanza namkubali sanaaaa…… anaemponda huyo atakuwa na kichaa +
 
Unawajua wanaomponda?
 
Yule dada anaakili sana alisema per day Ana earn zaidi ya lako mbili sasa unampondaje mwanamke mwenye akili kama yule?
 
Kazi yoyote unayofanya unamfanyia mtu mwingine uwe umeajiriwa au umejiajiri
 
Daah Mkuu umenipa tabu sana kusoma Comment yako. Hope mwalimu wako wa mwandiko alifanya kazi yake vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…