Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

Acha kuwaza kitoto,Kila mtu ana njia yake ya kupita,uyo aliepata mapesa mengi ndio njiaaliyoandikiwa na mungu,fanya hesabu kidogoo wunafahamu watu wenye degree walioajiriwa mishahara yao ni sh ngapi na hao wenye masters?Dada anasema anaweza kuuza mpaka sahani 40 kwa siku ambapo kila sahani anauza kwa elfu tano piga hesabu kwa mwezi anakusanya kiasi gani? na piga iyo mara mwaka ana pesa ngapi? alafu tafuta jibu kwa wenye degree na masters walioajiriwa hasa serikalini utapata jibu achana nambo ya Benja
 
Inategemea unauza karanga kwa namna gani. Biashara ni ubunifu. Shule inaweza kukupa maarifa ukauza karanga kisomi zaidi. Ukawa unanua kwa jumla kutoka kwa wakulima ukawa unafanya nice packaging na kutengeneza an efficient distribution channel au business process. Hapa bado tutakuita muuza karanga lakini hauko sawa na yule muuza karanga za mia mia pale stendi. Huyo dada muuza makande si sawa na muuza makande yoyote unayemfahamu. Ana uelewa juu ya concept ya branding na market segmentation. Angalia video ona sehemu kande zinapoandaliwa na packaging inayotumika. Kande zake si za kula kila mtu, zina wateja wa class fulani. MBA yake ipo kazini hapo. Huitaji kufanya rocket science kufanikiwa. Kuongeza tu thamani kwenye kile kidogo kunaweza kukupa mafanikio ya juu. Haya tuje kwa mtu anaitwa Mak Juice/ Mak Chicken. Kipi kinamfanya awe maarufu kuzidi wenye juice bar na wauza chicken hapa Dar? Branding and Packaging plus marketing strategy yake inatumia socialites na celebrities. Huyu ni muuza juice na kuku lakini anauza kuku na juisi kwa namna ya tofatuti. Hii ndo maana halisi ya kuwa mjasiriamali. Lazima ujifunze kuwa wa tofauti .The fact kwamba huyo dada tayari anaongelewa ina maana bi9ashara yake in ina prospects nzuri. Sasa kama huna cha kujifunza ina maana una uelewa mdogo sana wa dunia inaendaje. Tujitahidi kupanua uelewa wetu wa mambo ili tuondokane na hizi aibu ndogo ndogo za kuropoka ropoka kama hatukwenda shule.
 
msomi huyo kunamchongo anauandaa uki ticki,ili atoke na baadaye mbakie kusema alikuwa anauza makande tu hapa
 
Mkuu hawapendi kujifunza hawa watu na kazi kujifanya wajuaji. Huu ujuaji ungekuwa na faida Tanzania ingekuwa mbali kimaendeleo. Ila wengi ni zero brain halafu hawataki kukubali kwamba hawana exposure. Ukiona tu mtu anaropoka ropoka kujifanya anajua kuna mawili, kwamba exposure yake ni ndogo, na mbili hana muda wa kujisomea kujifunza zaidi
 
Naona we ndo umeropoka kama hujaenda shule,kwa mtaji wa shilingi ngapi unaweza kufanya package na branding ya biashara yako kama ulivyosema hapo juu? Mshasema huyo binti ni wa kishua......WATU MKISHAFANIKIWA MNAJUA SANA KURAHISISHA MAMBO.
 
Hongera zake. Aendelee hvi hvi mdogo mdogo mpaka afungue kiwanda kama vile kwenye Food Factory!
 
Tatizo mtaji pia, sio kwamba watu hawapendi kujiajiri

Sent using Jamii Forums mobile app
Unapozungumzia mtaji ni kama shilingi ngapi mkuu? anza na kile ulichonacho "mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe". Tatizo watu wanazunguuka sana na bahasha at the time anakumbuka kufanya biashara unakuta umri umeongezeka na majukumu pia yameongezeka na rafiki zake aliosoma nao wengine wameoa ama wamepiga hatua flani ya maisha na ndipo tunapokuja na kauli ya "TATIZO MTAJI" kwa kuwa kadri umri unavyosogea ndivyo matamanio ya kuwa na mtaji mkubwa yanavyoongezeka yaani mtu anafikiria milioni 5 ama 3 kumbe mtaji hata 300,000 (laki tatu zinatosha kama ukiamua)

Nachotaka kusema hapa maamuzi ya kujiajiri yafanyike ukiwa ungali mdogo kiasi kwamba ukipata laki 200,000 inaweza ikakubadilishia maisha tofauti na mtu anaanza kuja na wazo la kujiajiri tayari amegonga 30 and above years
 
Makande hayo usije ukakuta bei yake sawa na pizza, mtoto wakishua hawezi kuuza bei local sawa na uswahilini

Sent using unknown device
 
ndo Visingizio hivyo? ninacho wapendea Wabongo wenzangu ni hapo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nazani ulivyo fundishwa biashara ni kuuza Magari. vipi angefungua Yard ya kuuza Magari pia ungeongea hivi?

Yeye kaona furusa na bishara bi Biashara hata kama ni ya kuuza paka. kikubwa kuna profiti.

nyie ndo mmemezeswa kwamba biashara ni kuuza Magari na kufungua maduka ya nguo hizo ndo biashara mnazo zijua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ndo mentality za umasikini. kwa mawazo haya wacha tuendelee kuajiriwa na wachina na Wahindi na wazungu.

Unataka afanye kile unacho penda wewe?

sasa kama yeye hiyo ndo Hoby yake unataka aiache kwa sababu hampendi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Piga hesabu kwasiku anapata wateja wangapi halafu zidisha mala 5000, ela anayoingiza kwa siku sidhani kama mwenye hiyo degree akiajiriwa anaweza akalipwa kiasi icho
Ana wateja wake huyo wale wazee wa CRDB ambao 70% ya mishahara yao huishia kwenye mambo ya kuupendelea mwili kuanzia kula, mavazi, usafiri na kupanga nyumba kali

Sent using unknown device
 
Idea yake haiwezi kukufurahisha wewe. vipi angefungua saloon? au vipi angefungua duka La Viatu? ungeongea? make hizo ndo biashara mnazo zijua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…