Binti wa miaka 15 mwenye uraibu wa dawa za kulevya

Binti wa miaka 15 mwenye uraibu wa dawa za kulevya

Bongotunacheza

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2018
Posts
1,821
Reaction score
3,980
Familia ya PPM wa Mwanza, inawashukuru wote waliosaidia kusambaza taarifa za binti yao mwenye miaka 15 ambaye alitoroka kituo cha kusaidia kupambana na uraibu (Rehabilitation center) kiitwacho Vision of Hope Initiative kilichopo Njiro-Arusha.

Binti alipelekwa kituoni hapo ili kusaidiwa kupambana na uraibu uliokua unamsumbua lakini alitoroka. Hata hivyo kuna watu walimuona huko Sinza jijini DSM na wakatoa taarifa kwa wazazi ambazo zilisaidia kumpata.

Kwa sasa amepelekwa Kigamboni kwenye kituo kingine cha kumsaidia kupambana na uraibu. Wazazi wake wanawashukuru sana wote waliosaidia kutoa taarifa zilizopelekea kupatikana kwa binti yao.!

Credit: Malisa Facebook page

ILANI: Picha ya mhusika na jina vimeondolewa kumlinda mtoto.
 
SWali gumu na muhimu, ilikuwaje akawa teja, na ni madawa gani hayo.

Jambo la msingi kama hayuko tayari kuacha ni ngumu kumuachisha kwa kweli.. shida ipo kwenye utayari..
Kama hayuko tayari atatoka sober na atarudia
 
Ni mtoto wa kishua kwao Mwanza. Ndio hawa LIKUD anawazungumziaga, watoto wa EMS . English Mediums zina waharibu
 
Back
Top Bottom