Iko hivi mkuu mimi ni Mkristo, Biblia imetuagiza tuishi maisha yaliyo safi, lakini vilevile tumeagizwa kumtolea Mungu fungu la kumi,sadaka, shukurani, kuwasaidia wajane,yatima na wasiojiweza.Sasa km unapata pesa halafu hutoi sadaka hapo unakuwa umefungua mlango wa shetani kukuibia pesa yako.
Sasa Shetani anaibaje pesa? Ni hivi:-
1.Kwanza,Anakuletea matatizo yanayohitaji matumizi ya pesa km magonjwa,kesi,na matatizo mengine ya kifamilia ili tu utumie pesa na kwa mazingira ya kichawi hiyo pesa huenda kwao.
2.Pili Kumpa mtu mawazo ya kutumia pesa ovyoovyo kwa starehe mfano kubeti( kamali),Ulevi,Kupenda wanawake, na starehe zote zinazotumia pesa.
Elewa kwamba shetani hufanya kazi na fikra au mawazo yetu.Hivyo yeye hutuma pigo(Astral or psychic attack) ambayo huja kuamuru mtu afanye tendo fulani ili kutokana na hilo tendo basi kutokee hasara fulani.Halafu ukishaharibikiwa ndo unarudishiwa ufahamu na akili yako ya kawaida. Hapo ndipo majuto hufuata.
3.Kufanya matumizi yasiyo ya msingi.Unaweza pata pesa halafu ghafla ukasahau kufanya mambo ya msingi uliyokuwa umepanga na kujikuta unanunua visivyo na maana,kufumba na kufumbua pesa yote imeisha.
4.Kupoteza pesa.Unaweza shangaa ghafla pesa huzioni na hujui umepotezaje
5.Pia kupitia kuzulimiwa na watu. Unaweza kuta pesa nyingi unayopata unaishia kudhulumiwa na watu.
Hivyo pesa hii inayopotea kwasababu tajwa hapo juu huenda kimiujiza katika mabenki ya kuzimu na Shetani kuzigawa tena kwa watu wanaokuwa tayari kutimiza masharti. Mwisho wa siku humuacha mtu akiwa bila pesa,au akiwa na pesa kidogo isiyokidhi mahitaji yake ya msingi.
Njia pekee ya kumzuia Shetani asiibe pesa yako ni kutoa sadaka km Mungu alivyoagiza na pindi shetani akijaribu kuiba pesa yako anakutana na ulinzi wa Mungu.Maana katika Biblia Mungu kaagiza kuwa tukimtolea sadaka atalinda afya zetu,mali,zetu, watoto na hata wajakazi wetu dhidi ya yule mwovu( Ibirisi).
Bado una swali?