Issue ni image ya chama.
Wakati kina Mukama wanateuliwa majuzi walitoa hotuba nzito nzito, kina Chiligati na Mnauye na Kikwete etc. Common thread ya ujumbe wao ilikuwa wanataka CCM kirudi kuwa "chama cha wanyonge." Wakati wanajenga CCM, tokea TANU, tokea TAA, tokea Uhuru, Watanganyika, weusi walikuwa karibu wote masikini, wote, wakajiita wanyonge. Image ya chama cha wanyonge ndio iliyojenga chama nchi nzima kwa sababu kilionekana chama kinacho akisi picha ya Watanganyika, sasa wanasema wanataka kurudi huko.
Kumbe wanyonge wa CCM ni watu tofauti, hakuna shule ya sekondari Igunga, Tabora inayomtosha mtoto wa mbunge, hakuna shule Tanzania, hakuna sekondari Afrika inayomtosha mtoto wa kiongozi wa CCM, hakuna shule ya kawaida UK, Uswisi n.k. bali mtoto wa mbunge anasoma shule ambayo hata Malia na Sasha, watoto wa Rais wa mabepari wa Marekani hawawezi kusoma, hicho ni chama cha wanyonge?
Chama cha Mapinduzi kinajiuza kama chama cha watu wasiopenda kujilimbikizia mali. Basi angalau wangejilimbikizia mali halali. Mali za wizi. Wanajenga image ya chama kiongo na kinafiki. Mnyonge anaidai nchi umeme wake?