Binti wa umri wa miaka tisa amuuguza Bibi yake kwa zaidi ya miaka Mitatu

Binti wa umri wa miaka tisa amuuguza Bibi yake kwa zaidi ya miaka Mitatu

Tuache upuuzi ktk ishu kama hizi. Wakulaumiwa hapo ni watoto wa huyo mama.
....Kweli. Lakini na hao wauguzi wa hiyo wodi aliyomo mama mgonjwa wanastahili adhabu!
Miaka Mitatu wanaona mtoto wa miaka 9. Na kwa maana hiyo toka akiwa na miaka 6 tu, anamtunza mama yake wanaangalia tu bila angalau hata kuwaita Usitawi wa Jamii ???[emoji45][emoji45]
 
Mungu Awasaidie, inatia huzuni..

Anyway kwa usalama na uhakika
Mwandishi wenu nani?
Chombo gani cha habari?
Weka video hapa watu tuchangie kinachowezekana.
Hii habari nimeiona kwenye page ya Florah Lauwo ya Nitete aisee kuna mambo kule. Kama ww mzima na huna unachosumbuliwa nacho mshukuru sana Mungu. Afya ni mtaji, ile page ina mazito na magumu. Huwa nachangia kidogo kidogo napopata.
 
Ila maisha haya aisee, acha tu. Watu tunavyohangaika na kutamani kupata watoto wanaojielewa na wenye uwezo kama huyu.....dah. tuna watoto wamefika hadi kidato cha nne lkn kujieleza km hivyo hawawezi. Yaani unampotezea binti km huyu?!!!!!

Kila siku huwa namuwaza mama yangu na kuishia kusikitika kwa kutokuwa na uwezo wa kutosha wa kumfanyia makubwa ili nae aonje raha ya kuzaa......naishia kuongea nae tu kumpatia faraja na kupata baraka zake huku nikijitahidi kumtembelea mara kwa mara. Watoto 5 wote wanamkimbia mama yao?!!! Napata hasira sana.

Huyu binti ni tunu kabisa ya taifa.......namuona mtendaji mmoja mzuri kabisa wa kuliinua taifa. Km atakuwa mwalimu, basi wanafunzi wataelewa kweli kweli! Namuomba M/Mungu ambariki sana huyu binti!

Poleni mama zetu; mnatuzaa na kutulea kwa tabu, tukikua tunawakimbia huku tukikuleteeni wajukuu muscles km mlivyotulea sisi!!
 
Ndivyo wazazi wanavyoishia, hebu mwenye chochote atume, sasa litatoka jina gani?
 
Kweli inasikitisha lakini nadhani mtoto anabebeshwa mzigo mzito unaemuelemea, namsihi huyo baba wa mtoto aende kumchukua mwanawe akamuendeleze kwa mustakabali wa maisha yake ya baadaye na watoto wa huyo mama watafutwe hata ikibidi na vyombo vya dola ili wachukue jukumu lao mtoto akiendelea na hayo majukumu ambayo yamemzidi umri ataharibikiwa maisha yake.
 
JWTZ hamisheni huyo Askari bwege mhamishieni Mwanza akatunze mama yake kuwa asipotunza na kupeleka mtoto shule mnamtimua kazi

Atakuwa kapata mwanamke nwa kingazija Zanzibar huyo amemfuga .Mkuu wa Majeshi hamisha huyo Askari haraka
Nadhani huyo Askari ni mkwe wa huyo Mama.Mama wa huyo mjukuu amayemuhudumia Bibi alikuwa binti wa huyo Bibi ambaye alishatangulia mbele ya haki.

Hi inathibitishwa na maelezo ya Bibi kuwa anawatoto watano walio hai,wawili kati yao anasikia wako Katoro Geita na Wengine watatu hajui walipo.
 
Back
Top Bottom