Nimeamua nitafsiri mawazo ya Elon yamenivuti sana. Soma mpaka mwisho uelewe anachomaanisha kuhusu mtu maskini.
-------------------------------------------------------
Kabla ya yote, elewa kwanza utajiri haimanishi kuwa na pesa nyingi kwenye akaunti ya benki. Hatua ya awali, utajiri ni uwezo wa kutengeneza utajiri.
Kwa mfano, mtu anayeshinda bahati nasibu au kamali. Hata kama anashinda milioni 100 yeye siyo tajiri. Yeye ni maskini mwenye pesa nyingi. Hii ndio sababu asilimia 90 ya watu milionea wa bahati nasibu huwa maskini tena baada ya miaka mitano.
Pia kuna watu matajiri ambao hawana pesa.
Kwa mfano, wajasiriamali wengi wapo tayari kwenye njia ya utajiri hata kama hawana pesa, kwa sababu wanaimarisha mianya ya pesa, na huo ndio utajiri.
Ni vipi tajiri na maskini hutofautiana?
Kwa urahisi tu. Tajiri anaweza kufa na kupona ili awe tajiri, wakati maskini ataua ili awe tajiri.
Kama unamuona kijana ambaye anaamua kufunza, kujifunza vitu vipya, ambaye hujaribu kujiimarisha yeye mwenyenyewe, jua huyo ni mtu tajiri.
Kama unamuona kijana ambaye hufikiri kwamba tatizo ni nchi, ambaye hufikiri kwamba matajiri wote ni wezi, na yeye ni kukosoa tu, jua huyo ni mtu maskini.
Matajiri wanashawishika kwamba wanahitaji taarifa na mafunzo ili kuanza, lakini maskini hufikiri kwamba wengine lazima wawape pesa ili kuanza.
Katika kuhitimisha, ninaposema kwamba binti wangu hataolewa na maskini, siongelei kuhusu pesa. Ninaongelea kuhusu uwezo wa kutengeneza utajiri ndani ya mtu huyo.
Samahani kwa kusema hivi, lakini wahalifu wengi ni maskini. Wanapokuwa mbele ya pesa, wanapoteza ufikiri ndio maana wanafanya ujambazi, wanaiba, wanaua, wanatakatisha pesa nk. Kwao ni neema kwa sababu hawajui ni vipi wangeweza kupata pesa zao wenyewe.
Siku moja, mlinzi wa benki aliokota begi lenye pesa nyingi, alilichukua begi na kulipeleka kwa meneja wa benki.
Watu walimuita mtu huyu mjinga, lakini katika uhalisia mtu huyu alikuwa ni tajiri ambaye hakuwa na pesa.
Mwaka mmoja baadae, benki ilimpa ofa kama mtu wa mapokezi. Miaka mitatu baadae akawa meneja wa wateja. Miaka kumi baadae aliongoza utawala wa kanda wa benki hii. Aliongoza mamia ya waajiriwa na kila mwaka bonasi yake ilizidi kile kiwango ambacho angeweza kuiba.
Utajirini hali ya kufikiri kwanza.
Kwa hiyo, wewe ni tajiri au maskini?