Binti yangu, Kamwe usikubali kuishi na mwanaume anayekupiga au kukutukana matusi ya nguoni Kamwe!

Binti yangu, Kamwe usikubali kuishi na mwanaume anayekupiga au kukutukana matusi ya nguoni Kamwe!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
BINTI YANGU, KAMWE USIKUBALI KUISHI NA MWANAUME ANAYEKUPIGA AU KUKUTUKANA MATUSI YA NGUONI. KAMWE!

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Sisi watibeli hatupigi Wake zetu, Wala binti zetu hawapigwi Wala kutukanwa MATUSI ya nguoni.

Wala hatutishii kuwapiga, Wala wao hawatishiwi kupigwa. Na katika hayo hakuna kuteleza, hakuna bahati mbaya, hakuna kuzidiwa na hasira.

Tangu mwanzo mwambie mchumbaako kuwa moja ya mambo ambayo hutoruhusu na Wala kuvumilia ni kupigwa hata Kofi moja, Wala kutukanwa matusi yoyote ya nguoni.

Na endapo itatokea mwanaume akafanya hivyo usisite kumchukulia hatua zinazomstahili. Mtendee HAKI. Jicho lako lisiwe na huruma. Kama yeye alivyokosa huruma vivyohivyo nawe mchukulie hatua stahiki.

BINTI yangu, Mimi Baba yako nimeshuhudia mengi, zaidi ninaijua saikolojia ya watu wenye uwezo wa kupiga Wake Zao. Wenye uwezo wa kutukana MATUSI ya nguoni Wake Zao.

Hawana adabu.
Hawawezi kudhibiti hisia zao.
Hawajui nini chakufanya, hawana maamuzi sahihi.
Wanadharau na kukuona wewe ni Kama mnyama au mtoto au mtumwa au sio lolote sio chochote.

Binti yangu, mwanaume akikupiga jiulize huo ujasiri WA kukupiga umetoka wapi? Je ni ukichaa?
Je ni dharau juu yako?
Je ni ukosefu wa adabu?
Je ni ukosefu wa maarifa?

Wewe ni mtu.
Wewe ni mwanamke kama alivyo yeye ni mwanaume.
Hakuna sababu hata moja ya maana, na ya HAKI inayomfanya astahili kukupiga au kukutukana matusi ya nguoni. Hakuna hiyo sababu.

Nilikuambia, binti yangu ili uwe mtu lazima uweze kujitegemea. Lazima ufanye Kazi. Lazima uweze kuyaongoza maisha yako wewe mwenyewe. Sio umtegemee mumeo kwa kila kitu kama mtoto mdogo. Ndio maana utapigwa na kutukanwa matusi ya nguoni kama Mtu aliyedharauliwa, aliyelaanika.

Mwambie, watibeli hawanaga huruma kwa watu wenye dharau za makusudi kabisa. Watibeli hawanaga huruma na waovu wanaofanya uovu kimakusudi wakitegemea kuomba msamaha.

Asije akakudanganya mtu kuwa hutaolewa binti yangu.
Kama kuolewa kwenyewe ni kuolewa na wanaume wasiotenda HAKI ni Bora usiolewe kabisa.
Nilikuambia siku zote utende HAKI.
HAKI ni pamoja na kujiheshimu na kuheshimu wengine.

Usimuinulie sauti mwanaume , mheshimu mwanaume lakini kwa mambo ya HAKI. Kamwe! Kamwe! Kamwe! Usije ukakubali kumheshimu mtu yeyote aliyeamua kuivua heshima yake kwenyewe. Hiyo Sio HAKI.

Wasije wanaume wapumbavu wakakuambia maneno ya kipuuzi kuwa Mungu alituumba Sisi waume tuwatawale hata katika mabaya.
Asije akakuambia mtu yeyote kuwa unatakiwa umtii mumeo hata kwa Mabaya. Nope! Sio kwa Sisi Watibeli.

Mwanaume utamtii kwa mambo mema. Na sio Mabaya.

Mvumilie Mumeo kwa changamoto za maisha kama Hali za kiuchumi, labda kipato kidogo kutokana na riziki kuwa Haba.
Mvumilie Mumeo kwa Maradhi.
Lakini kamwe usimvumilie kwa mambo ya uovu.
Ndoa sio sehemu ya kuvumiliana maovu. Kuvumilia uovu ni kuusapoti uovu.

Makosa yanavumilika lakini sio uhalifu. Makosa yanavumilika lakini sio uovu/dhambi.
Makosa ni Kama wewe upige ugali uunguze, au unyooshe nguo iungue. Uvunje kitu kwa bahati mbaya.
Upoteze pesa kwa bahati mbaya (uzembe).

Sio mtu anakutukana matusi kwa dhamiri kabisa ili akuumize, anamtukana Mama yako, alafu mbaya zaidi sio mara moja yaani ni kila mara.

Mwambie Wala usimuogope, kama pombe akinywa zitamfanya akose akili ya kujizuia akafanya uovu akakupiga au kukutukana mwambie wewe hutohesabu kama ni pombe.

Ni aidha achague Pombe au Wewe.
Usiogope Wala kusita kuvunja ndoa na mwanaume anayepigapiga au kukutukana matusi ya nguoni. Mwanaume asiye HAKI.
Watibeli hatupo hivyo binti yangu.

Hayo yote ayajue mapema kabisa Kipindi cha mwanzoni ili yatakapoenda kinyume asije kusema hukumwambia. Mhakikishie kuwa hutokuwa na huruma.

Nimekufundisha kutenda HAKI. Basi iishi hiyo HAKI.

Acha Baba yako nipumzike sasa.

Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Imeisha hiyo,
Ila Binti usiwe na wewe namba one kutukana alafu hutaki kutukanwa,
Kuwa mstaarabu utapewa ustaarabu pia,
Kudos to my husband 10 years of peaceful marriage, I have never encountered even a slap
 
Kwa nini apigwe na kwa nini atukanwe?
Ukiona kuna ndoa ya namna hiyo Basi ujue zipo sababu za msingi zinazofanya ndoa ya Watu hao iwe katika hali hiyo.

Kumpiga mtu ni kosa kisheria sijui kama unajua jambo Hilo.

Pili, hakuna sababu hata moja ya kumpiga Mkeo/mumeo.
Kama mmeshindwana, hamuelewani peaneni Talaka.
 
Mlee mwanao katika misingi Bora kinyume na hapo
atapigwa tu, na kama anarudia lile analokatazwa atatukanwa tu,

Wanapigwa wanawake wasiojielewa. Watumwa, wajinga, tegemezi, wasiopenda HAKI.

Hao utakuwa na ujasiri wa kuwapiga. Vinginevyo hakuna rangi utaacha kuona.

Wewe huna ziada yoyote ya kumpiga mtu mwingine labda aamue kukuachia tuu
 
Kuna wengine bila makofi hawaendi

Kwa Sisi Watibeli hatuwezi ishi na mtu anayetulazimisha tufanye uhalifu.
Hapo suluhu sio kumpiga, suluhu ni kumuacha tuu.

Uliwahi kuona mtu mwenye akili zake timamu, mtu mzima akawa hivyo yaani bila makofi haendi?

Alafu nawe ati utampiga kwa vile wote mpo sawa
 
Mnatafutaga uadui usiokuwepo
Kamwe adui wa mwanamke hawezi kuwa mwanaume
Mwanamke Kwa mwanaume ni mama, bibi, mke, shangazi, dada n.k

Mwanaume aliyefundwa akafundika kamwe hawezi kumpiga mkewe au mwanamke yeyote.
 
Imeisha hiyo,
Ila Binti usiwe na wewe namba one kutukana alafu hutaki kutukanwa,
Kuwa mstaarabu utapewa ustaarabu pia,
Kudos to my husband 10 years of peaceful marriage, I have never encountered even a slap

Ndio maana nikasema wajue kutenda HAKI.

Mimi hata mwanamke ajue kuongea vipi siwezi mpiga. Zaidi ni kuachana naye tuu.

Ni kwamba hatuendani.
 
Kwa nini apigwe na kwa nini atukanwe?
Ukiona kuna ndoa ya namna hiyo Basi ujue zipo sababu za msingi zinazofanya ndoa ya Watu hao iwe katika hali hiyo.
Kuna watu wana mentality kuwa mwanaume anaweza tu kutoka kazini au mihangaiko yake akaanza tu kumpiga mwanamke bila ya kuwa na sababu,lazima ujiulize huyu mwanamke alifanya nini mpaka akapigwa,cha muhimu ni je hicho kipigo kinastahili kwa kosa alilofanya...?
 
Kwa Sisi Watibeli hatuwezi ishi na mtu anayetulazimisha tufanye uhalifu.
Hapo suluhu sio kumpiga, suluhu ni kumuacha tuu.

Uliwahi kuona mtu mwenye akili zake timamu, mtu mzima akawa hivyo yaani bila makofi haendi?

Alafu nawe ati utampiga kwa vile wote mpo sawa
Wakurya usipompiga anaona humpendi
 
Akimpiga ujue ni sawa na mwanaume kupigana na mwanaume mwenzake usiweke ndani u feminist wako

Kupigana ni kosa kisheria.
Lazima achukuliwe hatua.

Vipi wewe ukipigwa na Mkeo au kumwagiwa maji ya Moto na Mkeo au mafuta, itakuwa Sawa?
 
Back
Top Bottom