Bishop Josephat Gwajima: Mamlaka ya Rais yadhibitiwe Ili asitoke nje ya mpango na Dira ya nchi ya muda mrefu

Bishop Josephat Gwajima: Mamlaka ya Rais yadhibitiwe Ili asitoke nje ya mpango na Dira ya nchi ya muda mrefu

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

Askofu Gwajima ameendelea kusisitiza juu ya umuhimu wa KATIBA mpya kuwa mamlaka ya Rais ni muhimu yadhibitiwe, Rais aingiapo madarakani aikute dira na mipango na vipaumbele vya Taifa vya muda mrefu Ili ajikite hapo.

Amesisitiza kuwa, maono ya Taifa ya muda mrefu yakiwekwa kwenye long term plans itaondoa sintofahamu ya Kila Rais kuja na mipango yake mipya na kuacha alipoishia aliyepita.

Naungana na Askofu Gwajima, maana tumeona Awamu zote Nchi inaongozwa Kwa Maono binafsi ya Rais aliyepo Si maono ya nchi.

Atakuja huyu atasema tunue ndege, mwingine atatumbua majipu, mwingine atasema wezi wasemwe na washughulikiwe Kwa ustaarabu, wale Kwa urefu wa Kamba,mwingine atakuja asema ndege ziuzwe ni HASARA, mwingine atasema kuuza bandari au kuzibinafsisha ni uwendawazimu,akija mwingine anasema Kubinafsisha na kuuza bandari ndio mpango mzima.

Katika hili, naungana na Askofu Gwajima mwenye Maono ya miaka mingi sana mbeleni kulihusu Taifa letu.

Mungu Mbariki Askofu Gwajima,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Source: Global Publishers news.

Amen.
 
Hivi Gwajima yale ma-grader aliyoahidi kununua kule kawe kashakabidhi?

Alternatively, Hivi huyu Mbunge kafanya chochote Cha kukumbukwa Jimboni mwake toka achaguliwe?
Nje ya mada,

Si Rahisi kufaulu mtihani wowote Kwa majibu Yako, unaulizwa hili, unajibu lile🤔
 
Alichosema kina mantiki, namimi naongezea, Katiba mpya, sheria kali kwa viongozi, kuwaondolea kinga walizojiwekea. Mahakama iwe na meno makali, tena uwe Muhimili kamili si kama sasa.

KIla raisi anayekuja anajifanyia yake na kuacha ya aliyepita, sababu ni moja tu. naye anataka chake kwenye miradi mipya. Iliyopita anakuwa alishakula mwenzake. Tukatae Tz kuwa shamba la bibi, kila mtu anachimba atakavyo.
 
Alichosema kina mantiki, namimi naongezea, Katiba mpya, sheria kali kwa viongozi, kuondolea kinga walizojiwekea. Mahakama iwe na meno makali, tena uwe Muhimili kamili si kama sasa.

KIla raisi anayekuja anajifanyia yake na kuacha ya aliyepita, sababu ni moja tu. naye anataka chake kwenye miradi mipya. Iliyopita anakuwa alishakula mwenzake. Tukatae Tz kuwa shamba la bibi, kila mtu anachimba atakavyo.
Na wasisaini mikataba ya miaka mingi,

Rais wa miaka 5 pekee, anasaini mkataba wa miaka 30.

Mikataba ya muda mrefu isimamiwe na Dira ya muda mrefu ya Taifa yenye maono ya nchi itakayokuwa huru itakayosheheni wabobevu na wazalendo, wasomi nk nk.
 
Na wasisaini mikataba ya miaka mingi,

Rais wa miaka 5 pekee, anasaini mkataba wa miaka 30.

Mikataba ya muda mrefu isimamiwe na Dira ya muda mrefu ya Taifa yenye maono ya nchi itakayokuwa huru itakayosheheni wabobevu na wazalendo, wasomi nk nk.
Tena Raisi aliyeingia kwa Katiba, badala angemaliza ya aliyetangulia. Kwa muda mfupi amesaini mikataba mingi sana, ya muda mrefu.

Halafu kuna wehu wanamsifia, kama alichofanya ni sahihi. Wasichojua mikataba karibu yote kanufaika yeye na familia yake, waache baada ya miaka watajionea.
 
Sisi wakazi wa jimbo la Kawe bado tunakusubiri muheshimiwa sana Mbunge, ahadi zako hazijatimia
Jikite kwenye mada,

Hapa inajadiliwa Katiba mpya na kupunguza mamlaka ya Rais na kuwa na Maono ya miaka mingi ya Taifa.
 
Sawa kabisa!
Lakini Sina hakika kama Gwaji boy ana mpango wa kugombea Ubunge tena! Ndiyo maana amekuwa na ujasiri wa kuyasema hayo.
 
Hautaki tuseme chochote kuhusu mbunge wetu mpendwa?
Anadai Katiba mpya.

Hataki kuwa omba omba bungeni, kwamba kupata barabara ya lami Hadi umpigie magoti Rais au waziri.

Huoni huyo ni kiongozi Bora?
 
Back
Top Bottom