Bishop Josephat Gwajima: Mamlaka ya Rais yadhibitiwe Ili asitoke nje ya mpango na Dira ya nchi ya muda mrefu

Bishop Josephat Gwajima: Mamlaka ya Rais yadhibitiwe Ili asitoke nje ya mpango na Dira ya nchi ya muda mrefu

Mwanangu Tlaatlaah anasemaje kuhusu hilo

Ova
unaelewa ndugu yangu mrangi,

mambo haya yanahitaji utulivu, uelewa na ufahamu mpana na wa kutosha ndipo sasa uweze kujadili vyema na hatimae kua na uwezo wa kubaini na kutofautisha ni kitu gani cha maendeleo chenye ukomo wa muda, na kitu gani cha maendeleo kisicho na ukomo 🐒

utagundua kwamba kama uelewa wenyewe ndio huo,

utaona sasa kumbe,
hata kwenda kwenye uchaguzi kumbadilisha Rais hakuna haja tena, aendelee tu alieko akamilishe mpango wa maendeleo ambao utakua umewekwa ndani ya katiba, right? si ndicho mwataka?

na Rais atakae fuata, hana haja ya kua na ilani wala sera, atakuta tayari kuna mpango wa maendeleo kwenye katiba yeye ni kuchapa kazi tu sindiyo mrangi na ndugu mtoa hoja pamoja na comrade Bishop Gwajima?🐒

vinginevyo mtakua mnabadili katiba kila baada ya mpango wa maendeleo kufikia ukomo 🤣

ni vizuri kutokuchanganya mambo ya ObamaCare na katiba ndrugu zangu....
 
Na wasisaini mikataba ya miaka mingi,

Rais wa miaka 5 pekee, anasaini mkataba wa miaka 30.

Mikataba ya muda mrefu isimamiwe na Dira ya muda mrefu ya Taifa yenye maono ya nchi itakayokuwa huru itakayosheheni wabobevu na wazalendo, wasomi nk nk.
Kama ya loliondo, ngorongoro, Kia, Bandari NK
 
Anadai Katiba mpya.

Hataki kuwa omba omba bungeni, kwamba kupata barabara ya lami Hadi umpigie magoti Rais au waziri.

Huoni huyo ni kiongozi Bora?
Askofu Gwajima anafaa kuwa mkuu wa watu wake Mungu, Tanzania
 
Hivi Gwajima yale ma-grader aliyoahidi kununua kule kawe kashakabidhi?

Alternatively, Hivi huyu Mbunge kafanya chochote Cha kukumbukwa Jimboni mwake toka achaguliwe?

Watu wako serious wew unaleta utoto
 
Alichosema kina mantiki, namimi naongezea, Katiba mpya, sheria kali kwa viongozi, kuondolea kinga walizojiwekea. Mahakama iwe na meno makali, tena uwe Muhimili kamili si kama sasa.

KIla raisi anayekuja anajifanyia yake na kuacha ya aliyepita, sababu ni moja tu. naye anataka chake kwenye miradi mipya. Iliyopita anakuwa alishakula mwenzake. Tukatae Tz kuwa shamba la bibi, kila mtu anachimba atakavyo.

Naunga mkono na nakuunga mkono kwa hoja zako
 
Bunge zima la Marekani hakuna Professor wala PHD
PhD zipo nyingi sana.

Sema tu wao wamepona Ujinga kujitambulisha Majina Yao Kwa ELIMU kama Prof, Dr nk nk

Obama ana PHD tena Toka Harvard university, lakini anajiita Simply, Barrack Obama.
 
Itakuwa ni mara yangu ya kwanza kusikia jambo la maana ktoka kwa huyo mbunge.
Nakubaliana na maoni yake.
 
Hivi Gwajima yale ma-grader aliyoahidi kununua kule kawe kashakabidhi?

Alternatively, Hivi huyu Mbunge kafanya chochote Cha kukumbukwa Jimboni mwake toka achaguliwe?
Watu wanasubiri kwenda kozi Japan na Birmingham 😂😂😂
 
Wasiwe wezi Sasa.
Kenya hiyo mamlaka ilizuia budget ya IKULU na kusema ni ghali mno, wakadai IKULU ipunguze gharama ndipo waipitishe.

Huku tukifikia hapo, itakuwa njema sana.
 
Back
Top Bottom