Bishop Josephat Gwajima: Mamlaka ya Rais yadhibitiwe Ili asitoke nje ya mpango na Dira ya nchi ya muda mrefu

Bishop Josephat Gwajima: Mamlaka ya Rais yadhibitiwe Ili asitoke nje ya mpango na Dira ya nchi ya muda mrefu

Alichosema kina mantiki, namimi naongezea, Katiba mpya, sheria kali kwa viongozi, kuondolea kinga walizojiwekea. Mahakama iwe na meno makali, tena uwe Muhimili kamili si kama sasa.

KIla raisi anayekuja anajifanyia yake na kuacha ya aliyepita, sababu ni moja tu. naye anataka chake kwenye miradi mipya. Iliyopita anakuwa alishakula mwenzake. Tukatae Tz kuwa shamba la bibi, kila mtu anachimba atakavyo.
Tuna mifumo hovyo sana, sijui lini tutajitambua tuondokane na haya madudu.
 
Kuna nchi za ajabu sana hii Dunia,

Yaani rais anaweza kuamka tu akaelekeza bandari iuzwe na ikauzwa na watu wakabaki na furaha zao TU kama wendawazimu.

Zamani nilikuwa nikisikia vita na uasi katika nchi mbalimbali nafikiri Hawa watu hawana akili timamu lakini baada ya kuyaona yanayoendelea hakika yanasababishwa kwa 100% na uhovyo hovyo wa viongozi wanaopatikana barani Afrika.
 
Hata ukisikia mtu kaingia msituni hushangai😢😢
 
Anadai Katiba mpya.

Hataki kuwa omba omba bungeni, kwamba kupata barabara ya lami Hadi umpigie magoti Rais au waziri.

Huoni huyo ni kiongozi Bora?
Kwani wakati anagombea ubunge mazingira yalikua tofauti? Na aliwahi kusikika akisema hawezi fanya kazi za kilofa kama ubunge
 
Kwani wakati anagombea ubunge mazingira yalikua tofauti? Na aliwahi kusikika akisema hawezi fanya kazi za kilofa kama ubunge
Ni Kweli alisema hivyo,

Hata Daudi hakuwa na ndoto za ufalme, alikuwa zake porini akichunga mbuzi,

Sasa angekataaje maelekezo ya Nabii Samwel kutaka kumpaka mafuta kuwa mfalme?
 
Ni Kweli alisema hivyo,

Hata Daudi hakuwa na ndoto za ufalme, alikuwa zake porini akichunga mbuzi,

Sasa angekataaje maelekezo ya Nabii Samwel kutaka kumpaka mafuta kuwa mfalme?
Akae kwa kutulia, aache kulia lia, kila zama zina nabii wake
 
Akae kwa kutulia, aache kulia lia, kila zama zina nabii wake
HOJA yake mbona imenyooka kama rula?

Wewe hutaki Katiba mpya na Nchi kuwa na Maono ya muda mrefu na kupunguza mamlaka ya Rais Ili kumuongezea ufanisi kiutendaji?
 
Kuna nchi za ajabu sana hii Dunia,

Yaani rais anaweza kuamka tu akaelekeza bandari iuzwe na ikauzwa na watu wakabaki na furaha zao TU kama wendawazimu.

Zamani nilikuwa nikisikia vita na uasi katika nchi mbalimbali nafikiri Hawa watu hawana akili timamu lakini baada ya kuyaona yanayoendelea hakika yanasababishwa kwa 100% na uhovyo hovyo wa viongozi wanaopatikana barani Afrika.
Yaani Eti ukifa ikiwa kuwa Raise, unaonekana una akili na mipango Bora kuliko Mtu au kundi lolote nchini.

Hii Si sawa,

Mamlaka ya Rais yadhibitiwe. Yaendane na dira ya nchi ya muda mrefu.
 
Sawa kabisa!
Lakini Sina hakika kama Gwaji boy ana mpango wa kugombea Ubunge tena! Ndiyo maana amekuwa na ujasiri wa kuyasema hayo.
Kiongozi Bora,

Ni yule anayetangiliza Maslahi ya Taifa mbele kuliko maslah binafsi.

Na kiongozi huyo ni JOSEPHAT GWAJI MA
 
Kiongozi Bora,

Ni yule anayetangiliza Maslahi ya Taifa mbele kuliko maslah binafsi.

Na kiongozi huyo ni JOSEPHAT GWAJI MA
Ni kiongozi bora! Lakini kwa siasa za nchi yetu ni nani anayemwelewa?
Ni lini msemakweli kwa nchi yuko salama?
 
Ni kiongozi bora! Lakini kwa siasa za nchi yetu ni nani anayemwelewa?
Ni lini msemakweli kwa nchi yuko salama?
Viongozi wa aina ya Gwajima ndio wanasababisha uwepo utulivu kidogo duniani.

Wakiondoka hao, ni vurugu mechi na hapatakalika.
 
Salaam, Shalom!!

Askofu Gwajima ameendelea kusisitiza juu ya umuhimu wa KATIBA mpya kuwa mamlaka ya Rais ni muhimu yadhibitiwe, Rais aingiapo madarakani aikute dira na mipango na vipaumbele vya Taifa vya muda mrefu Ili ajikite hapo.

Amesisitiza kuwa, maono ya Taifa ya muda mrefu yakiwekwa kwenye long term plans itaondoa sintofahamu ya Kila Rais kuja na mipango yake mipya na kuacha alipoishia aliyepita.

Naungana na Askofu Gwajima, maana tumeona Awamu zote Nchi inaongozwa Kwa Maono binafsi ya Rais aliyepo Si maono ya nchi.

Atakuja huyu atasema tunue ndege, mwingine atatumbua majipu, mwingine atasema wezi wasemwe na washughulikiwe Kwa ustaarabu, wale Kwa urefu wa Kamba,mwingine atakuja asema ndege ziuzwe ni HASARA, mwingine atasema kuuza bandari au kuzibinafsisha ni uwendawazimu,akija mwingine anasema Kubinafsisha na kuuza bandari ndio mpango mzima.

Katika hili, naungana na Askofu Gwajima mwenye Maono ya miaka mingi sana mbeleni kulihusu Taifa letu.

Mungu Mbariki Askofu Gwajima,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Source: Global Publishers news.

Amen.
At the End Mtamwelewa Tule Smart Boy Tundu Lissu.

Hata Job Ndugai leo akiwa mkweli atakwambia kabiaa Mamlaka ya Rais ni shipa linalotuletea umaskini
 
Back
Top Bottom