Wilderness Voice
JF-Expert Member
- May 19, 2016
- 921
- 1,649
Taja viwanda ambavyo Nyerere alitaifisha. Watu kazi yenu kupindisha historia. Viwanda vyote vya nguo Tanzania vilijengwa wakati wa Nyerere. MUTEX kilikuwa kiwanda kikubwa Africa Mashariki.Nilikuwepo, viwanda vingi nyerere slivikuta vya watu binafsi akavitaifisha.
Alivyojenga yeye wakati wake wote havifiki 30.
Vyote vilikufa, vyake na alivyotaifisha, kabla hajaondoka madarakani.
Msidanganyane bado tupo hai.
Viwanda vya maziwa vilikuwa sehemu zote walikokuwa na ngómbe kwa wingi. Viwanda vya viatu iliitwa Bora. Kiwanda cha betri, Viwanda vya mafuta ya kula vilikuwa karibu mikoa mingi. Viwanda vya ngozi, Viwanda vya nyuzi, viwanda vya usindikaji, na kiwanda cha General cha matairi. Na vingi vinginevyo hivi vyo vilijengwa kwa fedha ya serikali.
Nyerere aliviacha vikiwa vinafanya kazi. Kwa taarifa yako wengine tumeonja matamu ya wakati huo ya Nyerere.
Nakumbuka ulikuwa unaenda Bora kununua viatu. Ukiingia unaletewa kifaa cha kuweka mguu kutambua size yako kisha unaletewa viatu vikiwa katika boksi yake. Yaani ilikuwa kama Ulaya ilivyo.
Kulikuwa na maduka ya serikali kila mkoa na wilaya RTC yaliuza bidhaa kwa bei nafuu. Nyerere aliacha yakifanya kazi. Yote yakauwawa na awamu zilizofuata. Ethiopia hayo maduka bado yapo. Ulaya kuna baadhi ya maduka bado yanamilikiwa na serikali hadi leo.
Wakati wa Nyerere tulisoma bure na kupewa madaftari na kalamu shuleni. Wanafunzi wa sekondari na vyuo walisafirishwa bure na serikali.
Kila mkoa katika miji kulikuwa na park, tuliita bustani. Yaani ilikuwa kama ilivyo Ulaya. Siku hizi mnajenga ovyo kila mahala hakuna hata park. Kulikuwa na hotel za kitalii kila mkoa zimejengwa na serikali. Hata club za serikali. Hizi Ethiopia bado wanazo. Nyerere aliziacha.
Wakati wa Nyerere kulikuwa na bank zinamilikiwa na serikali. Akaziacha. Mkabinafusisha na kuuza zote zingine mkauwa. Alipopiga kelele NBC isiuzwe duuh! Ndo ikawa niagieni. Nchi nyingi kubwa serikali ina bank hata hapa Afrika tu.
Kulikuwa na mabasi ya kila mkoa. Yalimilikiwa na serikali za mkoa. Yote mmeuwa. Niishie hapa ni mengi. Harafu unakuja hapa kuonesha Nyerere ati alitaifisha na kushindwa kuendeleza. Tusidanganyane.
Leo tu serikali inashindwa hata kuendeleza miradi ya mwendo kasi magari yanakufa. Yaani Tanzania ni shida tu.
Tanzania ya Nyerere ilikuwa na utamu wake kwa wale waliokuwepo wakati huo tulienjoy. Hakukuwepo na ufisadi uliokithiri kama leo.