Kwani kilichokwamisha ujenzi toka enzi za Nyerere miaka ya 70 , Mwinyi, Mkapa, Kikwete kilikuwa ni nini? Na JPM aliwezaje?

..hakuna Raisi wa Tz ambaye hakujenga mradi wa umeme.

..JK alikuja na mkakati wa miradi ya kufua umeme wa gesi.

..Magufuli aliachana na mkakati wa JK akaamua kujenga mradi kufua umeme wa maji.

..Mgao wa umeme ungemalizika mapema zaidi kama Magufuli angetekeleza mradi mdogo au wa kati usiochukua muda mrefu kama mradi wa Stieglers gorge.

NB:

..Tuliambiwa umeme unaozalishwa kwa nguvu ya maji ni wa bei nafuu zaidi. Je, tutegemee serikali kupunguza bei ya umeme?

..Watanzania tupinge jitihada za kutaka kuiuza Tanesco baada ya kuhangaika nayo wenyewe mpaka mgao umekwisha.
 
..serikali ishushe bei ya umeme.
Kwani Mheshimiwa mkubwa kabisa Mandondo c alisema umeme hautoshuka bei !!?
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa !
Mungu wa mbinguni anawaona 🙏🙏🙏
 
Mashine namba 1 hadi 8 wanawasha lini, maana tunataka bei ya umeme ishuke, maji mengi sana hayo, hakuna sababu ya kuyabania
 
Kwa Sasa ni sawa ila tuwe na mbadala (standby) maana haya mabadiliko ya Hali ya hewa hayaeleweki.Ukitokea ukame WA muda mrefu mgao utarudi tena.
 
Kwa Sasa ni sawa ila tuwe na mbadala (standby) maana haya mabadiliko ya Hali ya hewa hayaeleweki.Ukitokea ukame WA muda mrefu mgao utarudi tena.
Hakuna huo ukame in the near future !
Labda ifanyike hujuma tu !
Kataa Wahuni #Polepole !
 
Kwanini wasiwashe mitambo yote ndo waanze mambo ya uzinduzi kwa pamoja.... Hii nchi bana inaendeshwa na siasa za drama sana..
 
Shida ya umeme bado ipo. Hapa nilipo umeme umekata. Na nilidhani tatizo limeisha ndo maana nikatoa “like” kwenye hili bandiko. Nimerudi hapa baada ya umeme kukatika.
 
Shida ya umeme bado ipo. Hapa nilipo umeme umekata. Na nilidhani tatizo limeisha ndo maana nikatoa “like” kwenye hili bandiko. Nimerudi hapa baada ya umeme kukatika.
Hapa nilipo... Ni mji upi, kata ipi.......Mtaa upi....
Mimi niko kijijini Ifakara... Nguzo za umeme bado hazijafika, hivyo bado tunatumia mafuta ya taa.

Wenzetu mliopo mijini mnasemaje juu ya umeme, toka tutangaziwe mwisho wa mgao. Ni siku ya 5 leo, hivyo inatosha kutoa maelezo kama kwa siku hizi Mgao umetokomea.
 
Kwani Mheshimiwa mkubwa kabisa Mandondo c alisema umeme hautoshuka bei !!?
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa !
Mungu wa mbinguni anawaona 🙏🙏🙏

..kwanini usishuke bei wakati gharama za kuzalisha umeme zimepungua?
 
Matatizo ya kukatika ovyo kwa umeme yako pale pale! Actually kwa mwezi wa February ndiyo hali inazidi kuwa mbaya zaidi. Umeme tunajua ulimuwepo siku zote bali miundombinu na infrastructure nzima ya usambazaji has collapsed. Ndiyo maana walianza kusema tatizo ni ukame, mvua zikinyesha tutapata umeme. Mvua zimenyesha na umeme hatukupata. Wameongeza 235MW ambazo ni kubwa kuliko power generation ya bwawa zima la Kidatu, lakini matatizo yako pale pale. Watajaribu to appease watu wa Dar msipige kelele lakini ukweli ni kwamba umeme haupo hadi sijui lini. Kiwanda changu kimekosa umeme for 26 hours now. Uzalishaji umesimama. HALI NI MBAYA SANA SANA!
 
Mkuu ni kweli mgao ni kama umepungua. Ispokuwa kuna wakati wanakata na unarudi baada ya dakika hivi. Kama wanachosema ni kweli na mgao utaisha, ni mategemeo yetu bei itapungua.
 
Serikali yenyewe ina viongozi ambao hawaongei kwa sauti moja.

Wakati Waziri Biteko anasema tatizo linaisha kwa bwawa jipya kuanza kazi, RC wa Dar Chalamila alisema tatizo halitaisha kwa sababu kuna matatizo mengi katika distribution network, hivyo hata baada ya bwawa kuanza kazi kuna changamoto.

So far inaonekana Chalamila alikuwa muwazi zaidi na Biteko analeta siasa zaidi kuliko uhalisia.
 
Hapa nilipo umeme umekata tangu saa 12
 
Umepungua kwa siku ngapi sasa?

Bado nina mashaka….muda utatueleza!

Tutaona hali itakavyokuwa miezi mitatu ijayo, miezi sita ijayo, miezi tisa inayo, na miaka ijayo.

Siku mbili tatu za afueni haziwezi kunisahaulisha kauli zao za huko nyuma.
Mkuu kwa jinsi mgao ulivyokuwa mkali, sidhani hata kama wiki imepita tokea huo mgao umeanza kupungua.

Ni sawa na kuishi kwa njaa muda mrefu halafu ukipata chakula kwa siku tatu mfululizo unaweza ukahisi kwamba baa la njaa limekwisha. Ni saikolojia tu.

Hivyo nakubaliana na wewe kuhusu muda. Maana ni kweli ni siku mbili tatu umeme haujakatika. Na ukikata unarudi hapo hapo. Na hilo siyo jambo zuri bado.
 
Kwa hali nnayoiona kuanzia jumapili kwa hapa Mbeya ni mgao haupo. Umeme upo na umekuwa wa uhakika katika siku mbili tatu hizi

Kazi imefanyika✌
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…