Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko ameshuhudia uwashwaji wa mtambo namba tisa katika bwawa la kuzalisha umeme la Julis Nyerere JNHPP ambao umeanza kusambaza umeme megawat 235 katika gridi ya Taifa.
Akishuhudia uwashwaji wa Mtambo huo wa kuzalisha umeme Dkt biteko amesema uzalishaji huo wa megawat 235 utapunguza mgao wa Umeme kwa asilimia 85 na hivyo wananchi wataondokana na kero ya umeme.
"Hata hivyo uzinduzi rasmi wa mitambo miwili, mtambo namba nane na mtambo namba tisa utafanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mwezi ujao wa tatu ambapo mitambo yote hiyo miwili itakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme megawati 470" amesema Dkt Biteko
Pia soma:
-
Dkt. Biteko: Nataka niwahakikishie tutawapa umeme Watanzania