Biteko: TANESCO inanunua umeme wa Megawati 31 kutoka Uganda na Zambia

Biteko: TANESCO inanunua umeme wa Megawati 31 kutoka Uganda na Zambia

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko bungeni jijini Dodoma, wakati akisoma hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2024/2025 amesema:

Katika mwaka 2023/24 Serikali iliendelea kuchukua hatua za kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa umeme nchini ambapo hadi kufikia Machi 2024, uwezo wa mitambo ya kufua umeme iliyounganishwa katika mfumo wa Gridi ya Taifa ulifikia jumla ya megawati 2,138 ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.2 ikilinganishwa na megawati 1,872.1 za Mei 2023. Katika kiasi hicho megawati 836.3 sawa na asilimia 39.1 ni umeme unaotokana na nguvu ya maji, megawati 1,198.8 sawa na asilimia 56.1 ni gesi asilia, megawati 92.4 sawa na asilimia 4.3 ni mafuta mazito na megawati 10.5 sawa na asilimia 0.5 ni umeme wa tungamotaka (biomass)”- Dkt. Biteko.

Ongezeko la uwezo wa uzalishaji wa umeme limetokana na kuanza kwa uzalishaji wa umeme katika Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere (megawati 2,115) ambapo megawati 235 zimeanza kuzalishwa kupitia mtambo namba 9 pamoja na kukamilika kwa mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo ambao unachangia megawati 26.7 katika Gridi ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi 2024, uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme ambayo haijaungwa katika Gridi ya Taifa ni megawati 33.4 ambazo zinajumuisha mitambo inayomilikiwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) yenye uwezo wa kufua megawati 28.4 na megawati 5 zitokanazo na nguvu ya jua kutoka kwa mzalishaji binafsi.

TANESCO na kununua Umeme
Wizara kupitia TANESCO inanunua umeme wa megawati 31 kati ya hizo megawati 21 kutoka Uganda kwa ajili ya Mkoa wa Kagera na megawati 10 kutoka Zambia kwa ajili ya Mkoa wa Rukwa.

PIA SOMA
- TANESCO: Umeme tunaozalisha ni mwingi mahitaji ni madogo nchi nzima, hakuna mgawo kwa sasa

- Waziri Mkuu Majaliwa: TANESCO imezalisha umeme zaidi ya mahitaji

Mbunge - Vyanzo vyenu vya uhalisia wa upatikanaji umme unaozalishwa vinakinzana

View: https://m.youtube.com/watch?v=4DKSzyqRYRA
 
Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Nishati apigwa shule na profesa Muhongo kuhusu nchi imejitosheleza kwa umeme

1713973336075.png
 
Hiyo mikoa inawezekana ilikuwa mbali na mitambo mikuu ndio maana ikawa ni bora iungwe nje ya nchi.

Sio upungufu.

Ni swala la umbali toka Gridi ya Zambia hadi Rukwa ni mdogo. Ukilinganisha na Gridi ya Tanzania hadi huko Rukwa.

Ni kama vile Watu wa Kagera mpaka na Uganda kwenda Uganda madukani au Takes Rombo kwenda Kenya kuliko kuja Moshi au Arusha kununua vitu

DISTANCE FACTOR
 
Nchi za kiafrica zote zina akili sawa jambo la kushangaza Zambia imekumbwa na sakata la ukame na matokeo ya ukame yamesababisha kuwepo na upungufu mkubwa wa umeme na kusababisha ya mgao kwa watumiaji na mbaya zaidi serikali ya zambia nao wameenda kununua umeme ktk nchi ya msumbiji ili kipunguza makali ya mgao.
 
Hizo 5MW za Solar haitakuwa IPTL nyingine imetengenezwa?. Na bado.
Hata kumtaja tu huyo m-Binafsi ni shida?
 
Kwa mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mara, Mwanza na Shinyanga pia wangenunua kutoka Kenya ili umeme wa uhakika usiokatika upatikane, hadi hapo uzalishaji na usambazaji wa umeme wa uhakika toka vyanzo vya ndani na miundombinu mipya ya usambazaji itapokamilika.
Huo umeme wa Kenya kuuza nje watautoa wapi? Wao wenyewe wanategemea Ethiopia na Uganda. Sasa hao hao Kenya wanasubiri kwa hamu sana kununua umeme toka kwetu mitambo ya Nyerere itakapokuwa tayari na njia za kuupeleka huko itakapokuwa tayari.

Sisi ni uzembe wetu tu, lakini tunavyo vyanzo vingi vya kuzalisha umeme. Ungeniuliza mimi, hata makaa ya mawe ningetumia tu, bila kujali kelele za walioshiba.
 
Alimaanisha kunamikoa mbembezoni mwa inch ambayoaijaungwa nagrade yataifandio inaunganishwa naichihizondowanaotoa uduma ilatukumalizakuungnisha gradeyataifa inchizimahatutaija kununuumemeinje
Tusijikite tu katika kulaumu, wakati hatuelewi au hatuna taarifa kamilifu ya jambo husika.
Wewe hapa umejaribu kuelezea sababu za Rukwa na Kagera kununua umeme toka nje, ambayo ndiyo sababu ya msingi.
 
Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo - Bado Sana Nchi Inahitaji umeme zaidi ya 5,000 Megawatts na ili Tujitosheleze kabisa ni 10,000 megawatts hapo tutakuwa hatuna uhaba wa mahitaji ya umeme kwa shughuli za Kiuchumi na Kijamii

View: https://m.youtube.com/watch?v=fEGzgp3BnBI

Kuna tofauti kubwa sana kati ya nadharia na vitendo kwa nchi masikini kwa sababu ya ukosefu wa maarifa ya kuunganisha.
 
Huo umeme wa Kenya kuuza nje watautoa wapi? Wao wenyewe wanategemea Ethiopia na Uganda. Sasa hao hao Kenya wanasubiri kwa hamu sana kununua umeme toka kwetu mitambo ya Nyerere itakapokuwa tayari na njia za kuupeleka huko itakapokuwa tayari.

Sisi ni uzembe wetu tu, lakini tunavyo vyanzo vingi vya kuzalisha umeme. Ungeniuliza mimi, hata makaa ya mawe ningetumia tu, bila kujali kelele za walioshiba.

View: https://m.youtube.com/watch?v=yYIjdmcBk4w
Our premiere project is the 96km 400kV Kenya - Tanzania Interconnector line from Isinya to Namanga. The project is part of a larger Kenya - Tanzania - Zambia interconnector project that is expected to connect the East African Power Pool to the Southern Africa Power Pool, hence facilitating power trade.
Mawaziri wanaosimamia masuala ya Nishati wa Zambia, Tanzania na Kenya walikutana ambapo Serikali ya Kenya ilionesha nia ya kushiriki katika mchakato wa kuendeleza mradi kwa lengo la kupata fursa ya kununua umeme wa bei nafuu kutoka Zambia.

Hali hii ilibadili upeo wa mradi na kujulikana kama Zambia -Tanzania – Kenya Power Interconnector Project. Mradi huu unahusisha sehemu kuu zifuatazo:

i. Ujenzi wa laini ya msongo wa 400kV yenye uwezo wa kusafirisha MW 400 kutoka kituo cha kupoozea umeme kilichopo Pensulo, Zambia hadi kituo cha kupoozea umeme cha Mwakibete, Mbeya kwa upande wa Tanzania,

ii. Kuimarisha mfumo wa usafirishaji umeme nchini kwa ajili ya kuwezesha kusafirisha umeme unaotosheleza, wenye ubora na uhakika katika maeneo ya kaskazini, kaskazini mashariki na magharibi hadi kufikia Kenya kwa kujenga njia mpya ya kusafirisha umeme kutoka Mbeya hadi Singida katika msongo wa kV 400, na

iii. Ujenzi wa laini ya kusafirisha umeme yenye msongo wa kV 400 kutoka Arusha hadi Nairobi

Aidha, mradi wa ZTK ni mmoja kati ya miradi ambayo kwa siku nyingi imekuwa katika Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta ya Umeme (PSMP) kama miradi mhimili ambayo kuendelezwa kwake kutachangia kuwepo kwa vyanzo vya umeme mbadala kutoka nchi za jirani na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa kero ya upungufu wa umeme ambayo imekuwa ikiikumba nchi yetu mara kwa mara ambayo imesababisha kutoa huduma ya umeme kwa mgawo. Aidha, mradi huu pia utafungua uhusiano wa kibiashara kati ya makampuni ya umeme ya nchi

wanachama kwani mifumo ya usafirishaji umeme imepangwa iwe na uwezo wa kusafirisha umeme pande mbili (bi-directional) kwa ajili ya kununua na kuuza umeme kupitia masoko ya East African Power Pool (EACPP) na Southern African Power Pool (SAPP).

Kuunganisha gridi za umeme za nchi jirani ni moja ya mkakati wa kipaumbele ili kuepuka matatizo ya nchi moja kukosa umeme wakati nchi ya jirani inao umeme wa ziada kama ilivyoainishwa katika Power System Master Plan (PSMP). Aidha, ni moja kati ya malengo ya shirikisho la NEPAD kuona kuwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara zinakuwa na ushirikiano wa karibu katika masuala ya kuinua uchumi ambapo huduma ya umeme wa uhakika inahitajika.

Imetolewa na;

Badra Masoud
Msemaji,
Wizara ya Nishati na Madini
 
Kwa bei gani tunanunua ? Bila kufahamu jibu la hapa ni vigumu kutoa maoni..., Ingawa nashangaa kama tunazima mashine kutokana na kukosa mahitaji alafu tunaenda kununua kwa jirani ili kukidhi mahitaji...

Kama shida ni connection ya hizo sehemu kwenye Grid wanangojea nini ?
 
Kuunganisha gridi za umeme za nchi jirani ni moja ya mkakati wa kipaumbele ili kuepuka matatizo ya nchi moja kukosa umeme wakati nchi ya jirani inao umeme wa ziada kama ilivyoainishwa katika Power System Master Plan (PSMP). Aidha, ni moja kati ya malengo ya shirikisho la NEPAD kuona kuwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara zinakuwa na ushirikiano wa karibu katika masuala ya kuinua uchumi ambapo huduma ya umeme wa uhakika inahitajika.
Mpango wa Southern African Power Pool, upo siku nyingi, na ujenzi wa miundo mbinu ya kuugawa naelewa kuwa ilisha anza kutekelezwa.

Lakini la muhimu zaidi hapa, tusitoke kwenye reli kama taifa. Tujitahidi kadri ya uwezo wetu wote tulio nao, kuendeleza kwa ufanisi zaid vyanzo vyetu vingi tulivyo navyo hapa hapa, bila kujali au kutegemea tununue wapi. Tutanunua tukiwa na shida, vinginevyo tulenge zaidi kuuza huko nje.
 
Kwa bei gani tunanunua ? Bila kufahamu jibu la hapa ni vigumu kutoa maoni..., Ingawa nashangaa kama tunazima mashine kutokana na kukosa mahitaji alafu tunaenda kununua kwa jirani ili kukidhi mahitaji...

Kama shida ni connection ya hizo sehemu kwenye Grid wanangojea nini ?
Nadhani tatizo lao ni kutojieleza vizuri. Kagera miaka yote huwa wananunua umeme toka Uganda. Na Kigoma, nadhani hadi hivi karibuni umeme wao walitegemea jenereta. Rukwa na wao tatizo lilikuwa/liko hivyo hivyo, kwamba miundo mbinu ya kuusambaza hata huu mdogo kwenye gridi yetu ilikuwa haipo.
Wanachopaswa basi kueleza zaidi ni mipango yao ya kuhakikisha miundo mbinu hiyo inakuwepo
Huu umeme wa Rusumo, bila shaka sasa utaondoa au utapunguza utegemezi wa Kagera kwa Uganda.
 
Richmond inakuja wa namna nyingine. Hapa tutaligwa na kitu kizito
 
Mpango wa Southern African Power Pool, upo siku nyingi, na ujenzi wa miundo mbinu ya kuugawa naelewa kuwa ilisha anza kutekelezwa.

Lakini la muhimu zaidi hapa, tusitoke kwenye reli kama taifa. Tujitahidi kadri ya uwezo wetu wote tulio nao, kuendeleza kwa ufanisi zaid vyanzo vyetu vingi tulivyo navyo hapa hapa, bila kujali au kutegemea tununue wapi. Tutanunua tukiwa na shida, vinginevyo tulenge zaidi kuuza huko nje.

Na pale kwenye upungufu tununue umeme toka nchi jirani. Hakuna sababu ya kuwa na mgawo wa Nishati hii muhimu ya umeme ikiwa nishati zingine kama diseli na petroli tunaagiza nje ili uchumi na shughuli za kijamii zisisimame kwanini tunakuwa na choyo kwa nishati ya umeme kutoka nchi jirani.
 
Back
Top Bottom