Biteko: TANESCO inanunua umeme wa Megawati 31 kutoka Uganda na Zambia

Alimaanisha kunamikoa mbembezoni mwa inch ambayoaijaungwa nagrade yataifandio inaunganishwa naichihizondowanaotoa uduma ilatukumalizakuungnisha gradeyataifa inchizimahatutaija kununuumemeinje
Mnaoelewa muwe mnatutafsiria.
 
Uchumi wa nchi za Afrika, ukiondoa Afrika Kusini na zile za Kiarabu (kaskazini) umeshikwa na magabacholi kwa asilimia kubwa. Serikali na taasisi za kidola hufikiria na kuelekeza nguvu nyingi kulinda viongozi huku wakisahau umiliki wa uchumi na teknolojia.

Rushwa kubwa hutokea kwenye sekta za nishati kwa kutengeneza uhaba na maelezo mengi ya kinadharia ambayo viongozi hukaririshwa.

Hata hivyo, changamoto hii yaweza kuondoka tu kwa kujenga uwezo wa ndani wa watu wetu kiuchumi na kiteknolojia (mifano Afrika Kusini na Misri).

Hakuna maendeleo ya kweli kwa kutegemea makandarasi wa nje. Ni bahati mbaya sana kwamba siasa zetu zinajenga viongozi wenye mitazamo finyu kwenye hili.
 
22.04.2024 Tumezima mitambo 4 umeme umezidi.
24.04.2024 Tunaazima umeme Uganda na Zambia.
Hiyo mikoa inayonunuliwa umeme kutoka nje haiko kwenye gridi ya taifa. Kwa hiyo lile ongezeko la umeme kwenye gridi ya taifa haliwezi kuwanufaisha kwa kuwa hawajaunganishwa!
 
kama diseli na petroli tunaagiza nje ili uchumi na shughuli za kijamii zisisimame kwanini tunakuwa na choyo kwa nishati ya umeme kutoka nchi jirani
Hii dhana ya utegemezi wakati uwezo upo huwa hainiingii sana akilini. Sasa tutauza gesi asili Kenya ili watuuzie umeme? Hapana.
Kwanza umeme wa Kenya, kwa mfano ni ghali sana kwa sababu zinazojulikana vizuri. Tuagize umeme kama huo utatusaidia kitu gani kiuchumi.
 
Kama tunao hadi umezidi matumizi huu wa kununua wa kazi gani?
Nadhani ni kwa mjibu wa masharti ya mikataba tuliyoingia nao huko nyuma. Huwezi ukaisitisha kabla ya muda wa mkataba kumalizika la sivyo utashitakiwa kwenye mahakama za kimataifa.
 
Nadhani ni kwa mjibu wa masharti ya mikataba tuliyoingia nao huko nyuma. Huwezi ukaisitisha kabla ya muda wa mkataba kumalizika la sivyo utashitakiwa kwenye mahakama za kimataifa.
Songas mkataba unaisha lini?
Kuna maandlizi yoyote ya serikali kupokea miundombinu na mitambo?
 
Hii dhana ya utegemezi wakati uwezo upo huwa hainiingii sana akilini. Sasa tutauza gesi asili Kenya ili watuuzie umeme? Hapana.

Umeme ni nishati sawa na nishati ya petroli pia dizeli ambayo tunanunua nje kwa kuwa haipatikani nchini.

Vivyo hivyo kwa kuwa nishati ya umeme kwa kipindi hiki na miaka kadhaa mbele hatujitoshelezi inabidi kununua nishati hiyo kufidia pengo la mahitaji ya nishati hiyo hadi hapo tutapofikia uwezo wa kujitosheleza nishati ya umeme toka vyanzo vya ndani.

Nishati ya umeme siyo anasa ni kichocheo cha mapinduzi ya nne ya viwanda, teknolojia na mazingira safi, hivyo serikali isione umeme ni anasa.

Afrika yatakiwa kutumia fursa ya mapinduzi ya nne ya viwanda​

(GMT+08:00) 2016-05-13 09:07:34

Rais Paul Kagame wa Rwanda ametoa mwito kwa bara la Afrika kutumia fursa zinazoletwa na mapinduzi ya nne ya viwanda ili kujifanya kuwa mdau kamili wa mambo ya dunia.

Rais Kagame ametoa mwito huo kwenye ufunguzi wa mkutano wa baraza la uchumi wa dunia kwa Afrika jana mjini Kigali.

Amesema kama teknolojia na masoko ya mitaji yakitumiwa vizuri, yanaweza kulisaidia bara la Afrika kuondokana na changamoto zilizopo sasa.

Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Bw Akinwumi Adesina pia amesema Afrika haina chaguo ila kukumbatia mapinduzi ya nne ya viwanda 4.0, na moja ya vipaumbele katika hilo ni kuhakikisha watu wote wanapata umeme na wanaweza kutumia teknolojia za digitali.

Pamoja na kuwa soko la mitaji limetajwa kuwa na mustakbali mzuri, gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw Benno Ndulu amesema tatizo lililopo ni kwamba benki kubwa zimejikita kwenye nchi chache tu.
 
Umeme ni nishati sawa na nishati ya petroli pia dizeli ambayo tunanunua nje kwa kuwa haipatikani nchini.

Vivyo hivyo kwa kuwa nishati ya umeme kwa kipindi hiki na miaka kadhaa mbele hatujitoshelezi inabidi kununua nishati
Kama kawaida ya siku zote, naona maneno mengi tu... Haya yote hayataleta umeme.

Na isingekuwa kichaa Magufuli, hata hizo 2115 MW za Bwawa la Nyerere tusingekuwa tunaziwazia, pamoja na kuwa mradi huo ulikuwepo toka enzi za Mwalimu.
 
Kama tunao hadi umezidi matumizi huu wa kununua wa kazi gani?
Kimbembe ni kuufikisha kwa mlaji, umeme huko Rufiji unadhani kuufikisha Rukwa au Kagera ni mchezo? wa Kagera kuufikisha Ngara na Rusumo imekuwa shughuli imebidi kutafuta chanzo kingine hukohuko.
 
Haya ni maajabu, yaani vijijini watu hawana umeme bado watu wako gizani alafu serikali inasema umeme umezidi? CCM wanakera sana Watanzania bila kuchukua hatua CCM itatesa hadi vitukuu vyetu
 
Na Kwa taarifa yenu tuu hiyo Mikoa ambayo inapata umeme wa Nje haijawahi kuwa na mgao.

Wakati mnalialia kuhusu mgao sisi tunawachungulia dirishani 😁😁
 
Haya ni maajabu, yaani vijijini watu hawana umeme bado watu wako gizani alafu serikali inasema umeme umezidi? CCM wanakera sana Watanzania bila kuchukua hatua CCM itatesa hadi vitukuu vyetu
Vijiji vipi hivyo ikiwa 97% ya Vijiji vyote Tzn vina umeme?
 
Unaongea kama mjinga
 
Wapi huko Kuna mgao wa umeme?
 
Shida sio wao shida ni akili Yako Ginyu yenye uelewa mdogo.

Kwani kununua umeme Nje ya Nchi imeanza Leo? Iko hivyo Toka uhuru wa Tzn na pia hata sisi tutaanza kuuza huko tukiunganisha grid
 
Shida Iko wapi hapa kwenye maelezo Yako?
 
Kwa hiyo hapa umeandika nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…