Black Americans wanaondoka Tanzania na hizi ndio sababu zao

Waende tu....wamesahau kwamba Tanzania na Afrika kwa ujumla ni mtakuja tu.
 
Tumemzika juzi tu mumeanza kudai ardhi?!eti ardhiii... embu panda ndege urudi kwenu bhana!ardhi hata tusipoilima itatuhifadhi tukiondoka duniani,hatuna haraka nayo kabisa yaani!labda kama ni wabongo wenzetu mliobadili uraia semeni ukweli tuone tuwasaidieje.πŸ˜„
 
Wewe unataka wamiliki ardhi???
Au wewe ndo mmoja wa hao "Black Americans"
Kila mgeni akiruhusiwa kumiliki ardhi itakuwaje??

Kama wewe ni Mtanzania kuwa Mzalendo.
Wafate washarti yaliyowekwa wenye bia njema kwetu sisi Watanzania.
Rwanda ukubwa wake ni sawa na mkoa wa morogoro lakini mgeni anaruhusiwa kumiliki ardhi! Ijekuwa Tanzania ambayo almost 75% ardhi bado ipo tupu? Na ukae ukijua rwanda inaingia zaidi ya mara 30 kwa tanzania

Mi nadhani kuliko kukataa kabisa wageni wasimiliki ardhi ni bora tuwape ardhi kwa masharti maalum ambayo yatakuwa na faida pande zote.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Umewaza vizuri lakini kabla ya kuuliza hili swali???
Yes! Now tunapaswa kuigeuza nchi yetu kuwa nchi ya kipebari tuachane na ujamaa

Mtu yoyote mwenye mtaji akaribishwe kwa kupewa permit na kuuziwa ardhi hta ikibidi kwa masharti maalum

Wenzetu dubai wanajenga hadi visiwa baharini na kuwauzia foreigners wakati sisi huku sehemu kubwa ya ardhi tumeikalia bila kuifanyia chochote

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 

Hao ni wababaishaji tu. Mbona ardhi ipo ya kutosha kupitia TIC au EPZ?
 
Ardhi Ni mali ya Tanzania, nchi haitakufa. Wewe mwenzetu unamiliki ardhi marekani?
Kwa jinsi nchi yetu ilivyo kubwa hta kama kila mtanzania atapewa viwanja 50 bado itabaki ardhi ya kutosha tu! Huko marekani ukitaka ardhi hta wiki ijayo unaipata wenzetu walishaufungua uchumi wao kwa dunia nzima ndio maana kuna kila aina ya watu wanaishi marekani na wanamiliki ardhi.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Watanzania sijui niseme baadhi ama wengi wetu tuna kaubinafsi flani hivi kwa wageni.. badala kuwasemea vizuri kwa serikali iwaangalie na kuwaondolea masharti yanayowashinda.
Wamesahau usemi wa ' mgeni aje mwenyeji aneemeke' kwa mfano mstaafu wa marekani akija kustaafu tanzania atafanya matumizi kwa kutumia hela zake za kigeni na kuchangia pato la taifa.

Saaa watanzania wengi akili mgando hawajiliwaza hilo.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Kisa ni Wamerekani Weusi.... ndiyo wapewe aridhi ya Watanzania kwa kuongoza.. Wanda Kenya huko ndiko wanawahitaji. Wabongo na aridhi ampati kitu. Wameshindwa jirani Kenya itakuwa wao
 
Sasa unataka tujifananishe na Rwanda? Kwa kuwa Rwanda kafanya hivi na sie tufanye vile?
Kila Nchi na mambo yake.

Basi waende huko.

Sent from my SM-J200F using JamiiForums mobile app
 
Upumbavu wa kuwamilikisha ardhi ni hatuwezi kuukubali.
 
Kipi bora? Kuwa na ardhi kubwa isiyo na matumizi au kuwauzia baadhi ya watu waiendeleze na kutengeneza ajira?
Akili gani hizi?
Uuze ardhi kwa wageni?
Kwa njaa za Watanzania si utakuja kukuta nchi nzima wenyeji tumekuwa wapangaji?
 
Hasa mtu unakuja na familia yako hapa unataka ule maKfc, Macdonadi chocolates za Neyyork,Henesey na Jack daniel lazima maisha yawe gharama ukizingatia wengi wao ni watu wa low au middle income warudi tu tunataka wawekezaji wa uhakika siyo youtubers.
 
Kweli kabisa. Dem wa jamaa yangu anasepa kesho

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…