BLOCK 89 Wasafi FM

BLOCK 89 Wasafi FM

Aisee hawa jamaa bado sana,wana kazi kubwa ya kufanya kama kipindi chao cha kwanza ndo hiki..

Contents ya hii show ni mbovu kupitiliza,wanapiga makelele,hawapeani time,wanataka kuonyesha wanajua,yaani hamna taste yoyote..

Kipindi cha redio ni lazima kiwe na flow nzuri ya segments,kwa bongo XXL ndo the best kwa flow nzuri ya contents..

Sio mbaya wajifunze kwa waliowatangulia na sio kujifanya wanashindana nao kwa kila kitu..

It's never late to learn something new
 
I agree with you
Radio pekee unayoweza kusikiliza hata mwaka mzima bila kubadili station na bila kujihisi unamiss chochote kwasasa ni CLOUDS FM.

Na Television pekee ni EAST AFRICA TV.

Nyingine ni TAKATAKA tu.
 
Radio pekee unayoweza kusikiliza hata mwaka mzima bila kubadili station na bila kujihisi unamiss chochote kwasasa ni CLOUDS FM.

Na Television pekee ni EAST AFRICA TV.

Nyingine ni TAKATAKA tu.

exactly
 
Wanajitahidi lakini ubunifu bado sana. Haiwezekani muwe mnahoji wasanii kila siku! Hii itafikia sehemu itakuwa ovyo kwasababu nyingi ikiwemo mazoea.

Maswali yao mengi yanajirudia/yameshasikiwa sana na wengi sababu wanacopy kutoka media zingine na hasa interviews za playlist ya Lilommy. Ku copy si tatizo kama utaweza kuyapika upya ili kupata majibu ya utofauti na si kitu kile kile.

Huyo jamaa mnayesema ni mkimya anahitaji muda tu lakini ana kitu kikubwa ambacho kitafumka muda muafaka. Madj wao mizuka inapitiliza hadi wanaharibu muziki, over scratching na mtiririko wa muziki si mzuri sana, inaonesha muziki department ya Wasafi inahitaji pia DJ matured kidogo awaelekeze vijana.

Kwa ufupi wanahitaji watu matured kwenye burudani ili kusaidia ku direct kipindi na kuboresha chemistry ya wale watangazaji ambao ni wazuri sana otherwise kitachosha mapema watu wakishazoea ile mandhari ya studio.
 
producer wa hicho kipindi achukue huu ushauri. >>>>> kwanza hawapeani nafasi kwenye kuuliza maswali mgeni akitaka kujibu anakatishwa na swali jingine, very unprofessional! alafu hayo maswali yao hayana ushawishi wa mtu kusikiliza zaidi pia hayamfanyi mgeni kufikiria marambili mbili kwenye kujibu. Maswali yao hayana utafiti ndani yake sometimes wanaweza wakamuuliza mgeni kitu alafu mgeni akawasahihisha kua sio hivyo bali ni hivi.. pia kwenye hayo maswali yao kuna mengine yanamfanya source apatwe na jazba ila basi tu anavumilia, maswali hawayaweki kwa mpangilio from malaini to magumu to malaini. Kipindi kinaendeshwa na mihemko makelele mengi content 0. waache kuigana. Hawaendi na muda inapaswa ikifika saa tano kamili show is over ili watanzania tulale sasa utakuta wanapitiliza kwa vitu visivyoeleweka very unprofessional. Wanapaswa kutenga dakika hata 2 tu za kusoma messages za raia tu sio wanataja social media zao alafu wanamaliza kimya kimya hata kusikia maswali yenye content kutoka kwa raia. Kabla hawajamuita mgeni wafanye research kwanza tena kweli kweli sio kufreestyle tu On air its very unprofessional.

MWISHO uchezeshaji wa jingles ni mbovu sanaaaa, jingles hawazipi nafasi hata sekunde kadhaa kwa sekunde kadhaa. mtu unaburudika na mziki mara utaskia ndani ya sekunde moja jingles 5! very unprofessional wjifunze kwa east africa radio na clouds jamaa kwenye muziki jingels ni moja au mbili tu na zinapikwa kwa wakati maalumu sio hovyo hovyo hadi kumboa msikilizaji.
Since it's their debut in the industry give em an ample time,they gonna do better next time
 
Hamna nayezaliwa anajua kwani wote wanajifunza,ndio maana zamani kulikuwa na akina aboubakar sadiki,majizo,John dilinga nk,wakapotea baadaye wamekuja hawa wa sasa na usishangae wakapotea.Hii dunia kila mtu ana chance endapo akijituma na kuwa mbunifu ,hamna aliyezaliwa anajua kwani wote walipitia stage ya kujifunza,wakajua .
 
Hicho kipindi mim sijakisikia. inabidi nikiongeze kwenye list ya kusikiliza maana mimi huwa nasikiliza radio nyingi.
Magazeti-Magic Fm na Rfa pia Efm
Sport Hq-EFM
Mhana habari-DW
Burudani nahamia Mawingu na EFM
Saa moja usiku michezo nasikiliza kidogo EFM kisha nahamia Uhuru FM coz kuna dogo hivi anamwiga kitenge huwa anachambua vizuri sana michezo.
Saa mbili kamili usiku nahamia magic fm kwenye michezo
Saa tatu kamili usiku nahamia Upendo radio au Wapo redio kuna kipindi nasikilizaga nakipenda sana.
Kukitangazwa mpira nasikiliza radio ya taifa au sibuka fm.
 
Nimekitazama mara 4 hivi, naomba wafanyie kazi mambo haya
1.Mtu imara hafai kuwepo hapo, kipindi aachiwe Jonijoo na Calypsoo, then watafute mtu mwingine wa tatu, hata AALIYAH pia sioni akifit hicho kipindi AALIAH aka LIAH abaki kwenye REFRESH tu ni mzuri sana hapo, kipindi kiwe na mtu tatu tu na dj wao.
2. Watangazaji waachiane nafasi ya kuuliza maswali, wasiulize maswali wakati bado mgeni hajamaliza kujibu swali la mwingine, kuingiliana huko kunafanya kipindi kubore.JONIJOO na CALYPSOO naona atleast ndo wanauliza maswali ya mazito na yanayojielewa.

Naamini kadri wanavyoendelea wataimprove, fanyieni kazi maoni ya wadau wanayoyatoa maana ndo wasikilizaji na wafuatiliaji.
 
Shida nikwamba kila redio inayokuja mpya inataka kushindana na clouds. Wangekuja tuu kivyao wakapiga kazi na watu wawakubali kivyao. Clouds ni leval nyingine. Me naona redio ambayo bado ni mshindani wa clouds kwa sasa mm ni E fm.
 
Radio pekee unayoweza kusikiliza hata mwaka mzima bila kubadili station na bila kujihisi unamiss chochote kwasasa ni CLOUDS FM.

Na Television pekee ni EAST AFRICA TV.

Nyingine ni TAKATAKA tu.
Mkuuu na unga mkono hoja CLOUDS FM imejitosheleza kwa vipind kinomaa
Mimi hua nabadilisha kidogo EAST AFRICA FM ile saa sitaa kusikiliza KIPENGA
then na rudi CLOUDS ...!!
 
producer wa hicho kipindi achukue huu ushauri. >>>>> kwanza hawapeani nafasi kwenye kuuliza maswali mgeni akitaka kujibu anakatishwa na swali jingine, very unprofessional! alafu hayo maswali yao hayana ushawishi wa mtu kusikiliza zaidi pia hayamfanyi mgeni kufikiria marambili mbili kwenye kujibu. Maswali yao hayana utafiti ndani yake sometimes wanaweza wakamuuliza mgeni kitu alafu mgeni akawasahihisha kua sio hivyo bali ni hivi.. pia kwenye hayo maswali yao kuna mengine yanamfanya source apatwe na jazba ila basi tu anavumilia, maswali hawayaweki kwa mpangilio from malaini to magumu to malaini. Kipindi kinaendeshwa na mihemko makelele mengi content 0. waache kuigana. Hawaendi na muda inapaswa ikifika saa tano kamili show is over ili watanzania tulale sasa utakuta wanapitiliza kwa vitu visivyoeleweka very unprofessional. Wanapaswa kutenga dakika hata 2 tu za kusoma messages za raia tu sio wanataja social media zao alafu wanamaliza kimya kimya hata kusikia maswali yenye content kutoka kwa raia. Kabla hawajamuita mgeni wafanye research kwanza tena kweli kweli sio kufreestyle tu On air its very unprofessional.

MWISHO uchezeshaji wa jingles ni mbovu sanaaaa, jingles hawazipi nafasi hata sekunde kadhaa kwa sekunde kadhaa. mtu unaburudika na mziki mara utaskia ndani ya sekunde moja jingles 5! very unprofessional wjifunze kwa east africa radio na clouds jamaa kwenye muziki jingels ni moja au mbili tu na zinapikwa kwa wakati maalumu sio hovyo hovyo hadi kumboa msikilizaji.
Yani hawa jamaa ni kama wanashindana kuongea..Kila mmoja anataka aonekane bingwa wa kuongea..

Utakuta mtu kauliza swali hata halijajibiwa fresh mwingine kadakia na kitu kingine..

Bado hawajawa na chemistry nzuri na hawajajua kukimanage kipindi..Unless nakubali uwezo wa kila presenter pale ukiachia Mtu Imara..Calypso,Jonijoo na Aaliyah nishawaona kwenye vipindi vingine na wanafanya poa..Hope wakitulia watakuwa poa..
 
Kipindi wanapiga kelele hakuna mpangilio wa kuongea kama kibanda umiza Cha mpira
Mtangazaji mmoja kauliza swali kabla mlengwa hajajibu vizuri mtangazaji mwingine kadakia

leo Mr T Touch ametambulisha wimbo mpya, baada ya kupigwa huyo jamaa anayejiita Mtu Imara anamwambia wimbo wake umefanana na wa sheta "hatufanani", aisee touch kaishiwa pozi furaha ya kutambulisha wimbo wake imekata.
 
Hiv watu wanafurahia nini wakivaa milegezo na kuonesha boxer zao?
Tena Hadi kwenye vitu official
 
Back
Top Bottom