Blog ya ujasirimali imenivutia, nawashauri kuitembelea

Blog ya ujasirimali imenivutia, nawashauri kuitembelea

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
MATERU.jpg

Katika pekuapekua zangu nimekuja kukutana na blog hii ambayo mada zake ni za ujasirimali na zinafunza, kusisimua na kuhamasisha ujasirimali. Sijaona shida kushirikisha maana naona ni mkufunzi mzuri katika kufanya mengi iwe katika nyanja za elimu, afya, viwanda na kilimo vitu ambavyo wengi wetu wanajitahidi lakini pengine hawana nafasi ya kuwashirikisha wengine ili kupata maoni toka kwa wazoefu licha ya wengine kujifunza kutoka kwao.

Blog hii inaonekana kushamiri pia katika kilimo cha kisasa, kitu nilichovutiwa si kulima tu ila produce zifikie kiwango cha kuzindikwa tayari kwa soko hasa madukani, jambo ambalo linawezekana kama viwanda vya kuzindika nyanya, mafuta, vikolezo/viungo nk

Kilimo cha ufuta
Ufuta (2).jpg Ufuta.jpg Mafuta ya Ufuta.jpg
Kwa wajasiriamali wengi wanafahamu kuwa, ufuta ni zao linalotoa mafuta yenye thamani kubwa. Pamoja na matumizi ya kupikia, mafuta ya ufuta yanatumika katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumika kwa wanamichezo na wagonjwa kwa kuchulia misuli. Mafuta ya ufuta hayana aina mbaya ya mafuta na hivyo kuna namna yanatumika katika kupunguza pressure na maradhi yatokanayo na magonjwa ya moyo.

Ufuta unalimwa na kuandaliwa shambani kama ifuatavyo: -

1. Kilo moja ya ufuta ina mbegu zinazofikia 15,000
2. Kilo moja ya ufuta inatosha kupandwa katika eneo la eka moja
3. Katika eneo la futi moja shambani, hupandwa miche minne hadi nane
4. Mistari ya ufuta uliopandwa huwa umbali wa inch 15 had 36 kutegemea aina ya upandaji na ufuta wenyewe.
5. Mavuno ya ufuta kwa kiwango cha chini huwa ni kilo 360.
6. Mauzo ya mafuta ya ufuta hufikia shilingi 6,000/= kwa lita moja

Huwa hakuna tatizo la soko la ufuta Tanzania kwani, mafuta yote ya kula yanayotengenezwa Nchini yanatosheleza kwa asilimia 40 na asilimia karibu 60 ya mafuta ya kula huagizwa kutoka nje ya Tanzania.

Kwa Taarifa zaidi wasiliana na {i'MADS} Institute of Management and Development Studies Iringa. The former Sophist Tanzania College.

CC, kibananhukhu

Anuani ya blog hiyo ni: UjasiriMali na iMADS
 
CHONTO F1.JPG
Nyanya aina ya Anna F 1

Nyanya aina ya Anna F 1 kama inavyoonekana shambani ikiwa imeiva. Miongoni mwa sifa ya nyanya hiyo ni kuwa, ikiivia shambani ina uwezo wa kukaa miezi mitatu bila kuoza. Hata itakapo chumwa au kuvunwa nyanya hiyo ina uwezo wa kukaa nje ya jokofu (fridge) miezi mitatu bila kuonza.

Nyanya hii ni nzuri sana kwa wajasiriamali hasa wa kilimo cha Green House kwani huwa inavunwa miezi nane mfululizo na mche mmoja una uwezo wa kutoa hadi kilo 20. Hii nyanya huwa haiuzwi kwa presha kwani bei ikiwa ndogo inatunzika na inaweza kuuzwa pole pole.

Mbegu zinapatikana kitengo cha ujasiriamali cha i'MADS (Institute of Management and Development Studies - Iringa}.
 
Alizeti.jpg
Kilimo cha Alizeti, Mkombozi wa Bishara ya Kilimo Tanzania. Thubutu Utaweza

1. Alizeti inastawi maeneo mengi Tanzania hususani maeneo yote yanakostawi mahindi. Baadhi ya mikoa inakostawi sana alizeti ni pamoja na Singida, Sumbawanga, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Mtwara, Tanga na Dodoma.

2. Alizeti hupandwa mbegu punje moja moja

3. Mbegu ya alizeti hupandwa kwa kuzamishwa ichi moja chini ya ardhi

4. Umbali wa mbegu hadi mbegu ni futi moja au sentimeta 30, kwa mbegu za kawaida na futi mbili mbegu hadi mbegu kwa mbegu zinazokuwa kubwa na kuzaa alizeti yenye mzingo mkubwa

5. Eka moja huweza kupandwa kiasi cha kilo mbili za alizeti.

6. Eka moja huweza kupandwa kati ya mbegu elfu kumi na tano (15,000) hadi mbegu elfu ishirini na tano (25,000) kutegemeana na aina ya alizeti iliyopandwa.

7. Shamba la alizeti huwa halifukuliwi chini sana kwani hulimwa hadi ichi 8 tu chini ya ardhi
8. Mbegu namba mbili (2) huwa ni kubwa zaidi na mbegu namba tano (5) huwa ni ndogo zaidi. Ukubwa wa namba huwakilisha udogo wa mbegu.
9. Alizeti huweza kuchanganywa na mazao mengine kama vile soya, mahindi, kunde nk
10. Ardhi iliyo hadi ni Ph 5.5 inafaa kwa kilimo cha alizeti
11. Kuhusu mbolea wasiliana nasi lakini Nitrogen hufaa zaidi na potasium.
12. Kuhusu mavuno kwa eka, bei ya alizeti, kiasi cha mafuta kwa kila eka, kiasi cha mashudu kwa kila eka, kuhusu aina za mashine za kukamulia alizeti na bei zake pamoja na gharama zote za kulima hadi kuuza mafuta wasiliana nasi kupitia anuani ya hapo chini.
13. Tunaweza pia kuandika mchanganuo mzima wa Biashara ya kilimo cha alizeti au biashara ya kukamua na kuuza mafuta ya alizeti.
14. Simu: +255 767 11 1173. Kwa Dominick Mkuu kitengo cha Ujasiriamali (i'MADS) – Iringa.

Binafsi naona kiwango cha kufikiria kilimo hasa kwa waliopitia kitabu tukapanda hatua moja juu zaidi si kwa kulima na kuuza produce bali iwe njia ya uanzishaji viwanda vidogovidogo ambavyo baadae vitakua. Vema kufikiria processing ya kupata products za kuuza kwenye vyuo, hospitali, supper markets na hata baadaye to export.
 
Asante mkuu, wengi tunapenda kusindika mazao lakini gharama za mitambo, umeme vinakatisha tamaa. Mfano mashine za kukoboa au kusaga nafaka sio bei sana lakini kuvuta umeme wa phase 3 ni kazi hasa maeneo remote tunakoweza weka store. Matokeo yake wanauza nafaka tu

Napenda sana kulima najua ipo siku nitalima sana tu
 
Asante mkuu, wengi tunapenda kusindika mazao lakini gharama za mitambo, umeme vinakatisha tamaa. Mfano mashine za kukoboa au kusaga nafaka sio bei sana lakini kuvuta umeme wa phase 3 ni kazi hasa maeneo remote tunakoweza weka store. Matokeo yake wanauza nafaka tu

Naelewa tatizo hilo sana Mama Joe ila pengine tunafikiria kuanza kwa kiwango kikubwa mno. Labda kunza kwa kusogeza produce nyumbani pako ambako huduma za msingi kama umeme, maji na hivyo unapoongeza phace ya tatu kwa umeme pengine gharama zinakuwa nafuu zaidi kuliko unapopeleka ombi la sehemu mpya.

Pengine kujaribu Incoporated kwa kushirikiana ambao mnaaminiana kama wawili au watatu hivi kwa kuchangiana gharama, biashara ikishatengamaa mnaanzisha matawi kadiri ya idadi yenu kisha mambo yakishakaa vizuri mnagawana kila mtu kituo chake. Ni ushauri tu.

Hata hivyo nadhani maeneo ambayo rahisi kupata vitendea kazi kwa wajasrimali wadogo na waanzaji ni Asia ambako wana mitambo midogo ya kuanzia isiyotumia umeme mwingi. Mitambo ya kutoka Ulaya ni ya kibepari ni kwa ajili ya wenye kutumia mbuzi kuwagunga kamba ndefu wale majani ya mbali.
 
Asante mkuu, wengi tunapenda kusindika mazao lakini gharama za mitambo, umeme vinakatisha tamaa. Mfano mashine za kukoboa au kusaga nafaka sio bei sana lakini kuvuta umeme wa phase 3 ni kazi hasa maeneo remote tunakoweza weka store. Matokeo yake wanauza nafaka tu

Unajua kuna njia moja tu ya kuweza kufanya mambo kama haya.., badala ya kila mtu kuanzisha/kuagiza mashine yake na kujaza sokoni products nyingi zinazofanana na kushindana bei..., njia ni kwa wakulima kutengeneza co-ops / unions / ushirika na kutengeneza finished products hii itamsaidia kila mtu..., kwanza watahakikisha quality ni nzuri, pili kila mkulima atakuwa anayo sehemu ya kupeleka bidhaa zake karibu na yeye au ushirika wake watafata mpaka alipo, tatu sababu ya supplying power kubwa wataweza kupata tender kubwa au hata kusafirisha kutoka nje...

Zaidi ya hapo ni kuongeza gharama ambazo mwisho wa siku hata uenda soko usipate
 
Ushauri mzuri mipango hiyo aliianzisha sana Nyerere katika awamu ya kwanza lakini kukakosekana umakini. Kwa mazingira ya leo ambayo kuna nafasi kubwa zaidi katika sekta binafsi, huenda wenye upeo na mtazamo unaolingana wakashirikiana kuwa na ushirikiano kuanzisha kitu kama hicho, hii inawezakana.
 
Mkuuu nadhani kilimo kinamkomboa kila mtu now inabidi sasa tu think big na kuweza kuanzisha viwanda kabisaa kwa ajili ya kukamua mafuta,sio lazima kuanza juu kabisaaa,maana kama mtu akilima basi ana make sure ana sehemu ambayo ni ya uwakika anapeleka mazao yake yakakamuliwe

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Una maono mazuri, sio lazima kila kitu ufanye mwenyewe peke yako, tunakoendelea sasa hivi ni kwenye mfumo wa industrialization, utaratibu ungefanyika kama ifuatavyo:
  1. Mkulima
  2. Viwanda
  3. Soko

Kwa utaratibu huo mfumo wa viwanda utakuwa kwa kiwango kikubwa na hivyo hali itakuwa kama ifuatavyo:
  • Mkulima akishavuna mazao anayapeleka kwe wenye viwanda kwa ajili ya processing
  • Wenye viwanda baada ya processing products wanaziuza madukani, jumuia za mahospitali, shule na madukani
  • Wafanyabiashara nao watawauzia wateja ambao ndio hatima ya mzunguko wa biashara.

Huo ndio utaratibu ambao nchi zilizoendelea ambazo mfumo wa uchuni ni wa industrialization unavyofanyika, hakuna kampuni inayofanya kila kitu vinginevyo process itakuwa low na pengine kusababisha uzalishaji kusimama kwa sababu mbalimbali, maana kama kiwanda imekosa malighali toka kwa wakulima wazoefu kwa sababu iwayo yote iwe hali ya hewa au vinginevyo basi watahakikisha wana-import kuhakikisha mtiririko wa bidhaa unakwenda sambamba kama ilivyokusudiwa.
 
mkuu ccm wameua viwanda vyote na hata sasa ukitaka kuanzisha cha kwako serekali yote itaamia kwako wakuwekee vikwazo,ila akija mzungu kila kitu atapewa bure
_nchi ngumu hii
 
mkuu ccm wameua viwanda vyote na hata sasa ukitaka kuanzisha cha kwako serekali yote itaamia kwako wakuwekee vikwazo,ila akija mzungu kila kitu atapewa bure
_nchi ngumu hii

Nisingekuunga mkono moja kwa mmoja hoja yako sababu viwanda vilivyositishwa na CCM ni vile vya umma, lakini ulimwengu wa viwanda binafsi ni mkubwa sana, tusikatishe tamaa wakati kuna viwanda vingi vinazidi kufumuka kama uyoka, labda hujatembelea sehemu mbalimbali.
 
Asante sana wadau naona mmenifungua macho, nimekuwa nikifikiria kufanya biashara ya kusindika nafaka bidhaa ziwe unga, chakula cha mifugo na lishe kwa watoto na wenye mahitaji maalumu. Ninaishi mjini nimekuwa nikiona malori yakileta mahindi msimu wa kuvuna kisha kusafirisha unga wakati wa kulima. Wenye hizi mashine wanauza pumba bei na wanaruhusu kusaga nafaka tu. Kina mama wanaotaka kusaga lishe yenye mfano karanga, soya au dagaa hawaruhusu. Hapo hata mfugaji mdogo kuomba asage chakula chake haiwezekani. Nimewaza hii ndio inarudisha nyuma wakulima wanaoanza, maeneo makubwa kwa ufugaji ni vijijini au nje ya mji, nafaka tele, lakini mtu ukanunue chakula cha kwako na mifugo mjini ukisafirishe kwa gharama na bidhaa zako uzibebe ukauze mjini kwa gharama pia. Ninataka ku fill hii gap hata kuanzia mashine ndogo za diesel kwa matumizi binafsi kisha kuwauzia wengine.
 
Katika ujasirimali ulichosema ni muhimu kusoma mwenendo wa shughuli zinavyoenda na kuangalia gape iliyopo ambayo unaweza kuiziba. Tuachene na ila ya nani kaanza nini na mimi naiga kuweka kando yake kitu kile kile.

Pengine tatizo tulilonalo ni pale mashine tulizo nazo kufanya kila kitu jambo ambalo pengine wanaokataa ni kutokana na sababu za msingi kuleta madhara kwa baadhi ya vyakula vinavyosagwa. Mfano niliona vijijini wanaposaga mahindi kwa ajili ya chakuna huwa makini na kuhakikisha wanapokuja kusaga kimea kwa ajili ya pombe lazima wasafishe mashine vinginevyo wakisaga unga wa ugali baada ya kimea matokea wengi wetu wanajua ugali hautulii unakuwa ujiuji.

Kinachotakiwa specialization, wanashughulikia vyakula vya wanyama, Wanaoshughulikia vyakula vya binadamu. Bora kupeleka huduma maeneo ya karibu kwa wananchi. Tumekuwa na mazoea mno ya kila kitu kifanyike mijini na hasa miji mikubwa wakati uzalishaji mkubwa uko vijijini. Bora kusafirisha bidhaa zilizo tayari kuliwa ambazo zimeshakuwa processed kuliko kusafirisha mahindi mjini ambako hakuna vinu vya kutosha na wanunuaji waanze kazi ya kutafuta vinu.

Nadhani hii ya kuweka vinu vya kutosha maeneo ya vijijini ambako process za kuandaa unga na kisha kuwa packaged tayari kwa wateja itasaidia kuwaondolea mzigo wa kubeba viroba vya mahindi kwenda kusaga na hivyo kuwafanya wanunue unga na kwenda nao majumbani.
 
Asante nimekuelewa, hata wao wanadai mashine huchafuka na unga unakuwa haufai. Kumbe pia inabidi kuwa na specialization.... Nimejifunza kitu. Nitajaribu kuifanyia kazi hii. Blessings

Nakubaliana kwa asilimia kubwa. Hata Dangote Aliko, Tajiri namba moja Afrika, katika "ten commandments on money" amesisitiza kuwa moja ya kitu cha kumvusha mjasiriamali kirahisi ni shughuli za Processing. Dr. Olomi Pia katika "The Enterprise Map of Tanzania' ametafiti na kusema Uchumi wa Tanzania Umekuwa, Ume - double, na mchongo mkuwa ni wadau wanaofanya production na Processing. La msingi ni kuzalisha kwa kujali afya.
 
Ushauri mzuri mipango hiyo aliianzisha sana Nyerere katika awamu ya kwanza lakini kukakosekana umakini. Kwa mazingira ya leo ambayo kuna nafasi kubwa zaidi katika sekta binafsi, huenda wenye upeo na mtazamo unaolingana wakashirikiana kuwa na ushirikiano kuanzisha kitu kama hicho, hii inawezakana.

Ushirika leo umeanza kubadilika. Mfano mimi ni miongoni mwa washauri katika baadhi ya vyama vya akiba na mikopo. Wanahamasa sana hasa katika nyanja ya jinsi ya kutumia mikopo au mapato. Nina makubaliano na Posta na simu saccos, tazara saccos, NHC Saccos, Auto Mech Saccos na saccos nyingine kama vile PSPF Tumewashauri na wameanza kufanya miradi kwa ngazi ya mwanachama mmoja mmoja na vyama vyenyewe. Saccos moja tumeishauri ina mradi ambao unakaribia kuwapatia faida ya 5 billioni TZA Shillings.

Vyama vingi vya ushirika vya leo, vinasimamiwa na vijana watanzania wazalendo ambao wanafundishika (wapo Trainable). Baadhi ya kazi kubwa sasa hivi zipo katika ubora wa bidhaa na masoko. Masoko mengi yanategemea ubora na uwezo wa kufikisha sokoni kiasi fulani kwa mwaka mzima. Thou, kiasi hicho huwa ni kikubwa kwa aina ya uzalishaji wa Tanzania. Mfano, Nilienda india na kupata soko la maharagwe, lakini wanataka kontena kumi kila mwezi. Hiyo kwa sisi ni kazi kubwa na tumeshindwa kupata wazalishaji.
 
Kuna dalili ya uwezo wako mzuri wa kushirikisha elimu ya ujasirimali kwa umma, na pengine mbinu za kuwafunza uundaji vikundi ni shina la wengi kuweza kusimama na kuhimili vishindo vyenye kuteteresha nguvu za umoja kiuchumi.

Kuhusu soko la maharage huko India, nadhani utafiti uliofanya ni mzuri mno, labda ulikuwa hujajipanga vema pamoja na watu wako kufikia malengo ya walengwa katika biashara hiyo. Hata hivyo uwezo wa kupeleka container moja kila mwezi upo iwapo tu ushirikishwaji wa wengi utafanya na kuwa na source ya nafaka hizo kutoka kwenye vyanzo vijijini ambako kwa mazingira ya sasa ndio wazalishaji wakubwa.

Kwa vile uzalishaji ni wa msimu, hivyo basi ni vema kukawa na ghala la kuhifadhia ingawa kuna gharama zake katika utunzaji wa nafaka. Hiyo itarahizisha export ya container zima kila mwezi huko India. Mkijipanga vizuri na kushirikiana na baadhi ya wadai inawezekana hasa kusaka nafaka hizo kutoka mikoa ya Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa na Katavi.
 
Back
Top Bottom