Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Katika pekuapekua zangu nimekuja kukutana na blog hii ambayo mada zake ni za ujasirimali na zinafunza, kusisimua na kuhamasisha ujasirimali. Sijaona shida kushirikisha maana naona ni mkufunzi mzuri katika kufanya mengi iwe katika nyanja za elimu, afya, viwanda na kilimo vitu ambavyo wengi wetu wanajitahidi lakini pengine hawana nafasi ya kuwashirikisha wengine ili kupata maoni toka kwa wazoefu licha ya wengine kujifunza kutoka kwao.
Blog hii inaonekana kushamiri pia katika kilimo cha kisasa, kitu nilichovutiwa si kulima tu ila produce zifikie kiwango cha kuzindikwa tayari kwa soko hasa madukani, jambo ambalo linawezekana kama viwanda vya kuzindika nyanya, mafuta, vikolezo/viungo nk
Kilimo cha ufutaKwa wajasiriamali wengi wanafahamu kuwa, ufuta ni zao linalotoa mafuta yenye thamani kubwa. Pamoja na matumizi ya kupikia, mafuta ya ufuta yanatumika katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumika kwa wanamichezo na wagonjwa kwa kuchulia misuli. Mafuta ya ufuta hayana aina mbaya ya mafuta na hivyo kuna namna yanatumika katika kupunguza pressure na maradhi yatokanayo na magonjwa ya moyo.
Ufuta unalimwa na kuandaliwa shambani kama ifuatavyo: -
1. Kilo moja ya ufuta ina mbegu zinazofikia 15,000
2. Kilo moja ya ufuta inatosha kupandwa katika eneo la eka moja
3. Katika eneo la futi moja shambani, hupandwa miche minne hadi nane
4. Mistari ya ufuta uliopandwa huwa umbali wa inch 15 had 36 kutegemea aina ya upandaji na ufuta wenyewe.
5. Mavuno ya ufuta kwa kiwango cha chini huwa ni kilo 360.
6. Mauzo ya mafuta ya ufuta hufikia shilingi 6,000/= kwa lita moja
Huwa hakuna tatizo la soko la ufuta Tanzania kwani, mafuta yote ya kula yanayotengenezwa Nchini yanatosheleza kwa asilimia 40 na asilimia karibu 60 ya mafuta ya kula huagizwa kutoka nje ya Tanzania.
Kwa Taarifa zaidi wasiliana na {i'MADS} Institute of Management and Development Studies Iringa. The former Sophist Tanzania College.
CC, kibananhukhu
Anuani ya blog hiyo ni: UjasiriMali na iMADS




