Blue ticks za whatsapp: Ni kwamba huyo mtu yupo busy sana au ameamua tu kukuonesha dharau za waziwazi?

Nafanyaje isitokee blue tick? Najaribu ashindwa, napenda mtu asijue kama nimepokea mag yake
 
Wakati mwingine watu huwa wanalazimika 1. kufungua hizo message tu ile whatsapp isiendelee kuipop up hiyo message kwenye notification kila wakati.
2.Wengine wanashindwa kukujibu kwa wakati huko kwa sababu wanajua wakijibu utaendeleza mazungumzo na wana shughuli nyingine. Watu hawa hujibu hiyo message pale tu wanapoona wana muda wa kutosha kuchat hata ukiendeleza mazungumzo.
3. Dharau eidha kwa hoja au mtu anayeitoa. Kama umetuma message yakawaida tu, wakat mwingine mtu anaona hana haja ya kujibu. Au kama wewe huna umuhimu sana ,kwa nini akujibu.
4. Wapiga mizinga. Wale wa babe nikwambie kitu? Au wale wa habari za huko? Huku maisha magumu..... Message za hivi lazima ziishie blue tick.
5. Kwa wenye mahusiano kama mtu anataka muachane kidiplomasia bila vita baridi, anaamua kubluetick tu.
6. Kufungua data na kukuta message nyingi kwenye simu. Wengi hufanya hii. Unawasha data ,unakuta message 3000. Unajikuta unascan zote haraka haraka , halafu unaendelea na kazi. Utajibu moja moja hasa za muhimu zaidi ukiwa free.
SIO MARA ZOTE BLUE TICK INAMAANISHA UMEPUUNZWA!
 
Kuondokana na bluetick tumia whatsapp pori kama GB WhatsApp , au badili mpangilio kwenye simu yako. Kama ambavyo hutaki waone umewablue tick message zao, seti pia usione bluetick kwa message zako. Inakula kotekote!
Alisemaga Jakaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…