Blue ticks za whatsapp: Ni kwamba huyo mtu yupo busy sana au ameamua tu kukuonesha dharau za waziwazi?

Blue ticks za whatsapp: Ni kwamba huyo mtu yupo busy sana au ameamua tu kukuonesha dharau za waziwazi?

Naweza nisijibu kwa muda huo kweli ila lazima niijibu hata baadae. Hata mimi sipendi mtu aignore text au call yangu akichelewa sio ishu. Ishu ni kuipuuza.
Mimi hata mtu akinipuuza nafurahi tu.

Ananisaidia kupunguza idadi ya watu ninaowasiliana nao ambao hata wa sasa tu sina muda wa kutosha kuwasiliana nao, na wanaongezeka kila siku.

Uki mind sana blueticks unaweza kukaa na kijiba cha roho mtu hajakujibu, kumbe mwenzako kashakata roho huko.
 
Kuna za ubize na za dharau pia, ila nyingi ni za dharau.

Mtu uko busy kwanini ufungue msg? Ni bora uache itiki ile ya kuonesha msg imefika vitiki viwili lakini mtu na madharau yake unakuta anafungua na hajisikii kukujibu.
Binafsi uwa najisikia vibaya, na ukiniblue tick kwangu lazima nikulipizie no matter vile utapokea
Kwa hiyo ni dharau sio?
 
Kuna baadhi ya jumbe zinahitaji "quick response" na zingine hazina ulazima wa kujibiwa haraka...
Kila mtu ana haki ya kuamua yeye mwenyewe ujumbe gani unahitaji quick response na upi uanweza kusubiri.

Usimpangie mtu mwingine ujumbe gani unahitaji quick response. Wala usiache yeye akupangie wewe hilo.

After all, hujui situation yake ikoje huko aliko. Na yeye hajui yako.
 
Watu tunaotafutwa kwa kiasi kikubwa hatuna tatizo hilo.

Na mtu akichelewa kunijibu, that is his/her loss.

Kwa sababu mara nyingine nasalimia watu nikiwa na mood ya kugawa hela na zawadi ndogo ndogo zisizopungua thamani ya $100 🙂

Au kutoa bonge la idea ya kumfungua macho mtu. Au kumfariji mtu.

Wanaonijua huwa hawakawii kunijibu, wanaokawia kunijibu hawanijui. Nami sina hulka ya kutaka kujulikana au kuombeleza urafiki.
Mhhh
 
Back
Top Bottom