Hapana, siyo ya mtu mweusi peke yake. Hakika ni ya wengine pia. Lakini hao wengine haikuwazuia kupiga hatua za kimaendeleo. Wengi wetu kila siku wanalialia eti historia this, historia that, so what? Yaliyopita yashapita, sasa hivi tunaweza kufanya nini?
Hivi Zakumi ngoja nikuulize swali ambalo kwa maoni yangu ni rahisi tu. Ni kanuni gani ya kisayansi, kimahesabu, kifizikia, kikemia (hivi hayo yote si sayansi, au?) inayohitajika kujenga majengo imara (madarasa) ya shule na kuhakikisha yanakuwa na mahitaji yote yote ya msingi kama ubao, madawati/viti, madirisha, milango n.k.
Mimi nasema hivi, tushindwe kuunda miroketi ya kwenda angani sawa, tushindwe kujenga mibomu ya nyuklia na mi submarine poa, lakini siyo tushindwe hata kutengeneza madawati na vitanda vya hospitali. Khaaaaa!!!!