Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,966
- 11,218
Mbona Atlanta iko chini ya Mwafrika and so is Philly, and so are so many other well performing cities in these USs.
Hata hivyo swali la "kwa nini katika bara zima kusini mwa jangwa la sahara hali za maendeleo zinafanana".. well yapo majibu mengi.. ya kihistoria hasa.
Karibu nchi zote jangwa la sahara zina historia moja vile vile; zote zilijikuta zinatoka katika jamii ya kale na kusalimishwa chini ya utawala wa kikoloni ambao lengo lake lilikuwa ni kujenga nchi za watawala. Hivyo, kwa muda mrefu sehemu hii ya Afrika Kusini ilitumika kujenga chumi za huko ng'ambo huku makoloni yakitumika kwa ajili ya lengo hilo na maendeleo yoyote ya wakati wa mkoloni yalikuwa si katika kuendeleza makoloni ili yajitegemee bali yalikuwa yajitegemee kuendeleza nchi mama tawala.
Na hili kufanikisha hili wakoloni walitumia mbinu zilie za kuua hisia yoyote ya uhuru na kujitegemea na kumtukuza mtu mweupe. Wakati Wafaransa walitimua ile ya assimilation wao Waingereza na wengine walitumia kama ile ya indirect rule na combination mbalimbali. Matokeo yake athari kubwa zaidi ya ukoloni haikuwa katika kutoendeleza maeneo yetu bali ilikuwa katika fikra zetu.
Wakoloni walifanikiwa kutufanya tusijiamini na tushindwe kufikiri nje ya kile walichokijenga ndani yetu. Walifanikiwa kutufanya tuwe tegemezi kwao na hadi leo hii tumeendelea kuwa tegemezi kwa kiasi cha utumwa. Ndio maana Nyerere alipokuja mwanzoni kabisa alijenga hili wazo la "kujitegemea". Lengo lake lilikuwa ni kutuondoa katika utegemezi wa kiakili. Bahati mbaya sana leo hii tumekuwa wategemezi kwa kiasi cha kutisha zaidi kwani wakati wazazi wetu walikuwa na utegemezi kwa kulazimishwa na wakoloni kizazi chetu cha leo kinatengeneza utegemezi wa kupenda wenyewe!
Na hili kwa kudokeza tu unaliona pia kati ya Wamarekani weusi hapa Marekani kwani na wao wameathirika zaidi kiakili baada ya miaka 400 ya Utumwa na unakiona hata Afrika ya Kusini ambako chini ya utawala wa weupe kwa miaka kama 400!
Ndio maana ndugu yangu haya tunayaita mapambano ya kifikra kwani huko kwingine kote tutafika endapo tutaweza kutoka hapa tu!
Hapa ndio kwenye mtiani wenyewe particularly kwenye uongozi tabia zikiweza badiliki juu ujue chini zitafuta with or without compliance.
