Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Sorry folks...ila waafrika wengi wetu.. sisi tuna matatizo..tunaridhika haraka mno.no wonder akina Mangungo walituuza kwa wajeremani..kwa vipande vya kanzu na mvinyo...
Huwezi kusema huu mkate hovyo kwasababu umekosa amira,kama umekosa amira huo tayari siyo mkate,umeshakosa ingredient muhimu unayoufanya uitwe "mkate" sambamba na hali ya Afrika kwa ujumla,Afrika kama Afrika si Afrika minus History,sijui umenipata?History ni ingredient muhimu sana pale unaposema "Afrika" hivi ama "Afrika" vile....Na ndio maana narudia tena na tena pls revisit history....Waafrika si wajinga.
Nachokubali ni kwamba waafrika si wajinga na waafrika shall overcome provided that there will always be unwavering patriots,the spirit shall live generations to generations,na kama ilivyo kwa jamii nyingi duniani historically,mapinduzi might one day be a solutions provided the spirit is there and the only other ingredient is the right enviroments or situation to ignite a revolution,history can back that up,please revisit.
Hata niki revisit history nitaona kitu hicho hicho tu: ujinga wa Mwafrika. Hivi Mangi unadhani ku sign mkataba bogus wakati hujui kusoma na kuandika ni stroke of genius? Unadhani kuwauza binadamu wenzio in exchange for material goods ni werevu? Unadhani kujilimbikizia kinyume na sheria wakati umezungukwa na watu wenye dhiki isiyo na kifani ni ishara ya akili? Hivi unadhani kucha kutwa kuchagua mijitu ambayo unajua wazi kuwa ni mijizi ni ishara ya kuwa na akili?
Hiyo historia unayotaka nii revisit itakuumbua mwenyewe. Taking a page right out of Companero's playbook ain't gonna help anything.
Nadhani wakuu hapa tuangalie bigger picture. Ukitoa mfano wa Founding fathers wa US miaka 300 iliyopita nadhani hujitendei haki. Yes, US walipitia huko, je ina maana na sisi lazima tupitie huko? why should we reinvent the wheel? Kuna mambo mengi sana tunaweza kujifunza bila kuanza kuhangaika kuanza upya.
Bottom line is: The major task remains with WE THE PEOPLE. Hivi jiulize..leo hii watanzania baba zetu na mama zetu wanakufa njaa kwa magonjwa nk....lakini ni hao hao kesho utakuta wanaimba idumu CCM! baada ya kupewa tshirts mbili..... Effectively tumeshindwa kulink matatizo yetu na prevailing governance failure! Any democracy inahitaji accountability. Yote mtayasema, lakini ukweli ni kwamba Waafrika hatuhitaji mkombozi zaidi yetu sisi wenyewe. Nenda ulaya au America au kwingineko. Bila wananchi kushika hatamu..we are no where near the promised land.
Africa/Tanzania itakombolewa na watu wenyewe. Mpaka watu watakapoamka na kujua wajibu wao kama raia. Hakuna wasomi kutoka Harvard, Oxford au LSE wa uchumi watakaotukomboa. Hao watakomboa familia zao. We simply need ourselves. So we can blame anybody..ccm, Kikwete, Sofia Simba nk....bottomline is those folks will NEVER change kama WANANCHI hawatawalazimisha.
Its high time tuache hizi mediocre excuses za ujinga, umasikini, njaa...kwa maamuzi mabovu ya wananchi ambao ndo sisi. Huu ujinga na njaa havitaisha kwa kauli mufilisi za akina Makamba et al. Zitaisha tuu pale ambapo..tutaweka SOCIAL CONTRACT kati yetu na watawala. Na wala msitegemee kwamba wananchi wote wataenda shule ndipo wafanye uamuzi sahihi. Mi ndo maana nasema tena....waafrika, sad to say..we are simply stupid. Though haina maana kwamba huu ujinga ni permanent. Tukiamua tunaweza kutoka. But so far....we are the ones to blame. Hakuna maendeleo pasipo uwajibikaji. NEVER.
Infact mtu akishasoma na yeye anataka part of the cake..anakaa kimya..the common mwananchi anaendelea kupiga mark time...Ndo maana mimi wasomi wa Afrika siwafagilii kabisa..na wao ni mijinga tuu..maana ikishasoma inakuwa mibinafsi..haina mpango wa common good...ila hapa watakuja kama mbogo..eti wameitwa wajinga..yet hiyo elimu yao inaishia kwenye vitabu vyao huko huko waliko......
Sorry folks...ila waafrika wengi wetu.. sisi tuna matatizo..tunaridhika haraka mno.no wonder akina Mangungo walituuza kwa wajeremani..kwa vipande vya kanzu na mvinyo...
Hata niki revisit history nitaona kitu hicho hicho tu: ujinga wa Mwafrika. Hivi Mangi unadhani ku sign mkataba bogus wakati hujui kusoma na kuandika ni stroke of genius? Unadhani kuwauza binadamu wenzio in exchange for material goods ni werevu? Unadhani kujilimbikizia kinyume na sheria wakati umezungukwa na watu wenye dhiki isiyo na kifani ni ishara ya akili? Hivi unadhani kucha kutwa kuchagua mijitu ambayo unajua wazi kuwa ni mijizi ni ishara ya kuwa na akili?
Hiyo historia unayotaka nii revisit itakuumbua mwenyewe. Taking a page right out of Companero's playbook ain't gonna help anything.
Juli:
Je hiyo historia ya kutawaliwa ni ya mtu mweusi peke yake? Waingereza walitawaliwa. Wachina walitawaliwa. Wakorea walitawaliwa.
Kuna professa mmoja hapa kutoka South Korea. Anasema miaka ya 50, 60 wanawake walikuwa watafuta kuni kama Afrika. Amepoteza ndugu zake kwa TB.
Ukisiliza anayosema unaweza kupata hisia kuwa katika miaka hiyo mtu aliyeishi Kilimanjaro au Zambia alikuwa somehow better.
Hii ni aibu....huyo mtoto akiporonyoka hapo itakuwaje? But man, African women are tough. I just don't know how they make it. Shout out to all the hardworking African women in the motherland
Hapana, siyo ya mtu mweusi peke yake. Hakika ni ya wengine pia. Lakini hao wengine haikuwazuia kupiga hatua za kimaendeleo. Wengi wetu kila siku wanalialia eti historia this, historia that, so what? Yaliyopita yashapita, sasa hivi tunaweza kufanya nini?
Hivi Zakumi ngoja nikuulize swali ambalo kwa maoni yangu ni rahisi tu. Ni kanuni gani ya kisayansi, kimahesabu, kifizikia, kikemia (hivi hayo yote si sayansi, au?) inayohitajika kujenga majengo imara (madarasa) ya shule na kuhakikisha yanakuwa na mahitaji yote yote ya msingi kama ubao, madawati/viti, madirisha, milango n.k.
Mimi nasema hivi, tushindwe kuunda miroketi ya kwenda angani sawa, tushindwe kujenga mibomu ya nyuklia na mi submarine poa, lakini siyo tushindwe hata kutengeneza madawati na vitanda vya hospitali. Khaaaaa!!!!
Hivi kwa wazungu kuna mafisadi? Je nchi zote za wazungu zina mazingira mazuri na watu wake wote wananufaika na utajiri wa nchi hizo? Je nchi hizo zina maskini? Je watu wote kwenye nchi hizo wanafurahia sawa utajiri wa nchi zao?
Mwanakijiji:
Mafisadi wako kila sehemu. Hivyo matatizo yetu ya kimsingi kama maradhi, malazi, ujinga na mengineyo yataendelea kuwepo hata kama nchi itakuwa free kutokana na ufisadi.
Na kuna uwezekano mkubwa kuwa ufisadi unakuwepo kwa sababu tumeshindwa kutatua matatizo ya kimsingi ambayo yanakabili jumuia zetu.
Kwa mfano watu wamesha-observe kuwa sehemu zenye upungufu wa vitu watu wanakuwa walafi sana. Mtanzania ambaye kwa kipato chake hawezi kunye bia kila siku, siku akifika Marekani na kupata kipato ambacho kinamwezesha kunywa Heineken 5 kila siku, basi anaweza kuwa mlevi kupindukia kuliko Mmarekani ambaye ana access ya kunywa bia toka akiwa mtoto.
Jamii inapobadilika kunakuwa behavioral changes ambazo zina positive and negative impacts kwa jamii na kiuchumi. Hivyo mafisadi wa Ulaya na Wa Tanzania wanaweza kufanya kitendo kimoja kwa nchi zao lakini wakawa na impacts tofauti kabisa kwa jamii zao.
Hivi kwa wazungu kuna mafisadi? Je nchi zote za wazungu zina mazingira mazuri na watu wake wote wananufaika na utajiri wa nchi hizo? Je nchi hizo zina maskini? Je watu wote kwenye nchi hizo wanafurahia sawa utajiri wa nchi zao?
Julius.. we ushawahi kusikia mtoto kachoropoka mgongoni mwa mama?
Kwa hivyo, tusijikute tunajiona duni kwa mambo yanayofanywa na wanasiasa wetu na kuamini kuwa "miafrika ndivyo tulivyo". Ukweli wa mambo ni kuwa "binadamu ndivyo tulivyo". Mwanadamu yeyote akipewa nafasi ya kufanya ufisadi na kujinufaisha kwa mgongo wa mwanadamu mwingine atafanya hivyo bila kujali rangi, dini, au eneo la jiografia alipo.
Tofauti yetu kubwa ni jinsi gani tunawashughulia watu wa namna hiyo.
Oh mafisadi wapo. Italia kuna mafisadi kibao lakini Italia huwezi ukailinganisha na nchi yeyote Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.
Nchi zote za wazungu watu wake wote hawanufaiki na utajiri wa nchi hizo. Well, I guess inategemea na unamaanisha nini kunufaika? Welfare, SSI, n.k. zina count?
Kutokuwa kabisa na maskini ni vigumu kwa sababu binadamu kibinafsi tumetofautiana mengi. Kuna wavivu, kuna walafi, kuna wachapa kazi, kuna wenye kupenda kukata kona, kuna wenye mitazamo tofauti, n.k. Mtu mvivu kama hatajishughulisha na kujibidiisha ataishia kuwa maskini.
Na watu wote kwenye nchi hizo hawafurahii sawa utajiri wa nchi zao. Duniani hapa huwezi ukamfurahisha na kumridhisha kila mtu.
Sawa, unachosema pengine kina ukweli lakini ninachoshindwa kuelewa ni kwa nini katika bara zima kusini mwa jangwa la sahara hali za kimaendeleo zinafanana (zote ni nchi za ulimwengu wa tatu). Ina maana wote tuna tabia sawa (ya kutowashughulikia mafisadi)?
Aisee inawezekana imeshawahi kutokea lakini mimi binafsi sijawahi kusikia!