Spea sio adimu ila ni
ghali. Aidha bei ya gari zenyewe nazo sio kubwa kivile ni vile maintenance yake inakua juu kidogo.
Mfano kuna 1 series ya mwaka 2005, nyeupe ina cc 1590 bei yake hadi bandari ya Dar es Salaam ni
2,986 USD (Tsh. 6,930,000). Ingawa bei hii inaweza kushuka hadi around
2700 USD (Tsh. 6,265,000) akiagiza mtu ambae ameagiza mara nyingi na ana offer.
Gharama za ushuru wa TRA kwa hii gari ni
Tsh. 5,864,268.65 (20/1/2021, saa 2:40 asubuhi)
Kwa hiyo jumla ya bei ya gari na ushuru ni 6,265,000 + 5,864,268 ambayo ni
12,129,268/=
Sasa hii ongezea laki nane
(800,000) za kulipia shipping line, wharfage, port charges, clearing agent fee, plate number na kadi ya gari. Hii ni makadirio ila najua haitacheza mbali na hapa na mimi nilitumia less than that. Jumla kuu itakua roughly
13,000,000/=. Sasa ukiangalia hii bei ni more or less the same na bei za IST ya mwaka huo huo baada ya ushuru kupanda.
References:
Bei na specifications za gari nimeziona
hapa
Bei ya ushuru wa TRA nimeiona
hapa pia