Bado napata shida sana kuwaamini mafundi wetu, kwani sio gari za ulaya tu kwao tatizo, hata ukitaka kununua Xtrail unakutana na hadithi hizo hizo, yaani gari hapa ni Toyota tuu! lazima tukubali tunahitaji kubadilika na kuachana na mafundi uchwara, fundi ambaye hakubali kubadilika kwendana na teknologia tumkimbie kama ukoma!
mwaka 1998 niliagiza Mercedec 190 C ilipofika nilichekwa sana na mafundi, lakini gari nilitumia zaidi ya miaka kumi bila changamoto kubwa, sasa tatizo liko wapi?
Kwa kweli nimesoma maelezo ya Jitumiraba4 nimemwelewa vizuri sana, na kwa kweli sasa natamani kuagiza Volvo XC 90 ambayo miaka karibia mitatu naiwaza! naomba ushauri hapo pia!