BMW SUV (X3,X5) zinatelekezwa garage

Tatizo ni mafundi

Hizo gari hazina shida, Mafundi wetu ni tatizo, wote waongo na wapigaji
We fundi wa gari anatembea na nyundo ya kupasulia kokoto [emoji23][emoji23][emoji23] tena anajiita fundi wa umeme wa gari
 
Hizo gari ni nzuri ila usiwe na mfuko wa mawazo ilee km mtoto mchanga.
Kuna Ford moja combi wife alipiga msumari anaitaka nikapigizana nae makelele kakomaa nikamwambia chukua.
Kaibeba.
Kavimba nayo
Miezi kadhaa tu ikagima.
Mapenzi yakarudi mume wangu ,mume wangu.
Tukakomaa euro 500+ ikarudi road.
Imepiga kazi tena nikasahau siku naona mama anabadilisha night dress tu
Malovee km yote nikajua kuna shida mahali hapa.
Nikaambiwa chombo imetaga tena ipo garage.
Sikufanya makosa nikaenda chukua picha zote weka tangazo inauzwa.
Bei ya screpa.
Demu kashangaa tu watu hao wamejaa tukakabidhiana hapo hapo garage.
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]Ndo ilee Gari nzimaa lakini haiwaki labda uiwashee motoo
 
Sasa maelezo yote ya nini ndugu? Umeulizwa hayo yote? Ila anyway sijauliza kwa ubaya.
 
Siku nikinunua gari nasoma kwanza user manual yake yote ndio naanza kuliendesha. Kanuni yangu kuu ni kufahamu gari lako kuliko mtu mwingine yeyote kwa sababu linabeba dhamana ya maisha yako unapoliendesha na pia linawakilisha taswira ya jinsi ulivyo.
Ndiyo kabisa. Mafundi wengi wanayabaka magari yao. Service 0 halafu huduma wanataka.
 

Macbook ni kiasi gani dukani.
 
We fundi wa gari anatembea na nyundo ya kupasulia kokoto [emoji23][emoji23][emoji23] tena anajiita fundi wa umeme wa gari
Sa nan kakwambia umfate fundi wa namna hio kama sio huna hela. Au fanya nenda wheny companies kama toyota workshops ukiwakuta wa hovyo nipo pale. Mnaenda kwa mafund wa mchongo hana hata chet cha veta automotive au automobile na unaexpect good service. [emoji706]
 
Nadhani ushauri mzuri ni kununua gari brand new, kuna range ya marehemu Erasto Msuya ilinunuliwa brand new 2013. Baada ya kufariki ile gari aliuziwa tajiri mmoja shabiki wa yanga hapa mjini. Mpaka leo ile gari inadunda mifano ipo mingi. Tatizo sisi watanzania tunanunua luxury car za mitumba. Gari ukinunua brand new huwa kuna kawarranty unakuwa nacho na hata dealers hapa Tanzania wanafanya service kwa bei ya chini. Discovery 4 ni gari ya 2009–2016, lakini leo ndozimejaa mjini. Gari zinazoweza kununuliwa mtumba na kuwa nzuri ni ambazo zinaweza kuendesheka mpaka 1000000 kms. Gari kama landcruiser au Mark II zipo na zinadumu toka enzi zile. Kuna siku nilienda mbeya na kukuta taksi Mark II ina 700000 kms kwenye odometer. Ukienda kilimanjaro utakuta toyota stout mpaka leo zinapiga kazi. Kwa hio hizi gari kama una hela nunua mpya. Maana kuna watu wana hela lakini wamezitelekeza kwa sababu ya usumbufu kila siku kuna kitu kinakufa. Anaona bora alipaki nyumbani. Na anavuta Prado akiacha Discovery kuku watagie mayai.
 
BMW walikuja TZ,mojawapo wa obstacle kubwa waliyoiona ni kwamba TZ hakuna qualified Fundis wa magari yao

So,mojawapo wa strategies yao ni kwamba wata establish official maintenance cornerstones TZ na pia watapenyeza know how yao kwenye magereji TZ watu waelewe.

Hilo ndio tatizo kubwa lililopo TZ hasa kwa magari yote ya watu wa middle class and upper class wealthy people!
 
Mafundi wetu wengi NGUMBARU
 
Mimi ilinitokea kwenye duka la viatu mwaka huu..hiyo siku nilikua namsaidia mshikaji wangu kuhamisha vitu ili vipelekwe mkoani tukasaidiana kubeba pale tukavipelekea ilala kwenye yard ya Aifola(nilivaa bukta,flana iliyokatwa mikono na viatu vya kimasai) na jamaa angu alivaa bukta na flana na yebo yebo [emoji16]. Basi baada ya kutoka pale nikamwambia mwana anisindikize K/Koo nikanunue viatu tukafika kwenye duka moja hivi nikakuta watu kadhaa tukaingia(mimi nina mguu mkubwa navaa 45 hivyo najijua ili nipate kiatu super dukani lazima niwe na mpunga).

Sasa ile tushaingia nikaanza kuangaza huku nikaona mikwaju mitatu matata nikamwita jamaa aje anitolee akawa kama hanisikii nikamfuata nikamshika bega nikamwambia nataka kile na kile jamaa akajibu "oya utaviweza bei yake vile laki na 10 na kile kingine 90",huku ananiangalia vizuri nikamwambia oya mzee nimekwambia lete viatu au hauuzi?

Jamaa ndo akashusha viatu pea 3 pale nikajaribu ziko safi nikatoa keshi 290 kabaki katoa macho na wala sikutaka kubageni.

Hii nchi kuchukuliana poa kupi sana kuanzia muonekano hadi life style mtu anayoishi.
 

Pole sana ndugu,Lakini hatupasi kuchukuliana poa hakuna mtu muhimu zaidi ya mwenzake.

Pili maisha huwa awamu tu ,unaweza ukafanikiwa leo haraka wenzako wakawa bado hawajafanikiwa hatupaswi kuwa dharau huwa ni wakati tu.

Mimi najitahidi sana kuheshimu watu na kutowadharau bila kujali wao wananionaje.
 
Mimi gari langu maswala yote ya umeme nisimamia mwenyewe narekebisha... Raha ya Youtube
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…