BMW SUV (X3,X5) zinatelekezwa garage

BMW SUV (X3,X5) zinatelekezwa garage

Ndugu umefafanua vizuri sana , Gari zote za ulaya ni bora mno na nirahisi kutengeza japo zina ugharama kidogo kwa sababu spare zake sio nyingi mtaani yaani spare za kukata sio nyingi , hatuna mafundi, hata hao maarufu wengi ni uzoefu tu ila sio kusomea automotive engineering , Mfano nina gari CLS 550 ilikushuka ikagoma kupanda kupeleka kwa mtaani kwa wasomali hapa nilipo nikaambiwa compressor imekufa , kupeleka kwa mtaalam wa kimexico kabadilisha fuse kitu kikapanda dola 200 tu ufundi na fuse , ningemsikiliza msomali litakiwa dola 4000
Huyu fundi mmexico yuko wapi?
 
Tatizo kubwa hapa bongo ni mafundi wanatuharibia magari.

Inaweza kuwa tatizo la umeme kwenye gari, labda sensor fulani au wiring tu, wao wanalitafsiri ni mechanical problem; wanabomoa injini au gearbox hapo ndo habari imekwisha huna gari.

Imeshawahi kunitokea ndo maana nasema haya, niliingizwa hasara ya kununua gear box nyingine kumbe tatizo halikuwa gearbox, niliyoitoa kumbe ilikuwa nzima,

Gari ilikuwa na tatizo la kushtuka na kuzima inapoingia speed ya 80km/h au wakati mwingine inapoingia speed ya 60km/h, inastuka wakati gear inaingia na inazima. Walibomoa gearbox wakairudidhia ndo ikafa mazima gari haisogei hata futi moja.

Nikanunua hiyo gearbox nyingine wakaweka gari ikarudi na tatizo lilelile inazima baada ya kufikia hizo speed.

Hapo nimeshatupa 2m imagine.
Sasa wakaanza kuisingizia injini nikawaambia acheni nikachukua gari yangu nikaenda nayo nyumbani kwa hasira.

Gari ukitembea speed chini ya 60 unaenda nayo popote haizimi.

Nikaanza kuhangaika mwenyewe utundu utundu wa kufunguafungua kidogo ninao na spanner ninazo kwa kazi zangu ninazofanya.na google pia inasaidia sana tusidharau ilimradi rugha iwe inapanda.

Baada ya kupata marekezo sababu zinazoweza kusababisha hiyo hali wakaziorodhesha, nikafata moja baada ya nyingine.

Nikafika kwenye crank shaft sensor hapo ndipo lilipokuwa tatizo, huwezi kuamini matatizo yote na kuhangaika kote ni hapo, kadude kadogo tu kama betri ya remote, hii gari hiyo sensor ipo chini ya injini imefichwa kidogo na bellhousing ilikuwa imejaa tope limeganda, nikaifungu nikaisafisha nikaifunga gari ikawa imepona inabadili gear vizuri haizimiki tena

Mafundi sina hamu nao.

Kula tano mkuu[emoji109]
 
Back
Top Bottom