Boarding Schools 1970s-2000: Kambi za watu katili, wanaopenda masomo, mateso, ukakamavu, walokole na wazinzi

Siku mbili tu tangu nimeripoti ndanda boys high school nikasikiwa natafutwa na jamaa anaitwa mkali man. Huyo alikua ni mbavu moja hatari wa form six na huyo jamaa alikujaga na vyuma vyake vya mazoez akaviweka kwenye rum flan pale kwenye mabweni ya kilimanjaro (kibo).
 
Na wewe Ng'wanapagi umesoma GESECO? Lakini itakuwa juzi juzi hapa!! Enzi zetu ndo ilikuwa taabu tunasoma na Wakara wamekomaa kishenzi!!
 
Mimi nilikuwa mbabe sana mpaka waalimu wenyewe wakija kunipa mpaka wajipange kinoma
 
Na wewe Ng'wanapagi umesoma GESECO? Lakini itakuwa juzi juzi hapa!! Enzi zetu ndo ilikuwa taabu tunasoma na Wakara wamekomaa kishenzi!!
Kaka nimesoma kipindi cha second Master aitwaye Sungusungu, akina mwalimu Shebby (mzee wa moshi), Babu Tangalo. Ilikuwa nuksi sana kaka kilichonisaidia kuishi maisha hayo ni upole, heshima na kujishusha. Shule zote za kanda ya ziwa ikiwemo aliyofundisha raisi Magufuli walikuwa wachumba tu.
 
endelea na simulizi...nakumbuka kuna mtu alifumwa anapiga puli...(goli la mkono)(kupanda mnazi kwa mkono m1) dah...akakabidhiwa ndoo azunguke kila bweni aijaze ile ndoo kwa vile avitoavyo...dah noma!
 
daahhh... hii story inanikumbusha mbali sana..... kwa wale wenzangu wa zamani sijui kama mnazifaham shule za Tukuyu za LUTENGANO NA NDEMBELA........ aiseeeee.. zile shule alikuwa ananisimulia baba yangu mdogo akija likizo ilikuwa ni balaaah. na baba mdogo alikuwa mbabe ana knuckles na anabeba vyuma ilikuwa shida sana. so hapa napata picha ya alichokuwa anasema. mkuu hii utupe kama ilivyo..usiache kitu. mimi nlisoma boarding pia hi habar ya kunyanyasa form one nlikutana nayo.... ila tulinyoooshana sana.
 
Naona umejifanya "Stering wa picha" , wewe ndio ulikuwa mjanja na wenzako wajinga, umehadithia wenzio walivyodhalilishwa huku ukificha yaliyokukuta
 
Ikiendelea nitag
 
Hadithi tamu. Watu mnajua sana fasihi. Ila umesahau kidogo kuonyesha uhalisia wa matukio. 70's na taa za sola duu. Afu ganja ts.100 ktumbua tsh5
Hapa ndipo script inapoingia dosari[emoji1]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…