Na; Bob Chacha Wangwe
Mhe. Mbowe na Mhe. Lissu wote ni viongozi wetu. Mchango wao ni mkubwa sana na tunawapenda. Lakini tunaipenda zaidi CHADEMA. Katika kuchagua mmoja kwenye nafasi ya Uenyekiti, tukiamua kabisa kuweka upambe na uchawa pembeni na kuangalia maslahi na ustawi wa CHADEMA na Upinzani kwa ujumla, hebu tujiulize maswali sita (6) yafutayo halafu ni imani yangu yatasaidia kutuonesha anayestahili kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA.
1. Ni yupi kati ya hawa wawili maadui zetu wa kisiasa wanatamani achaguliwe kuwa Mwenyekiti?
2. Nani anaungwa mkono zaidi na Umma?
3. Yupi ambaye akichaguliwa ushindi wake unaweza kuongeza ari na matumaini kwa Watanzania Wazalendo ambao wengi wanaonekana kukata tamaa?
4. Uchaguzi ni kawaida kuacha athari na majeraha kwa chama, ni yupi unadhani ushindi wake unaweza kutuachia athari au majeraha kidogo baada ya Uchaguzi?
5. Ni yupi kati ya hawa, unadhani aina ya watu wanaomuunga mkono ni kwa maslahi yao binafsi na sio maslahi ya CHADEMA?
6. Kwakuwa chama ni Wanachama, kati ya hawa viongozi wetu wawili, nani unadhani akichaguliwa atasaidia kuongeza Wanachama wapya?
Maswali haya sita (6), yatusaidie kufanya maamuzi januari 21, 2025! Kama huna sifa ya kupiga kura, waombe wanaoweza kupiga kura watuchagulie huyo nafsi yako kwa dhati kabisa inakwambia ni sahihi!
Happy new year in advance!
Bob Chacha Wangwe