TANZIA Bob Makani afariki dunia

TANZIA Bob Makani afariki dunia

R.I.P mzee wetu , ila huyu mzee cdm walimtupa na hawakumpa hata matibabu apart from mchango mkubwa alioutoa kwenye chama


Alipotupwa na CDM wewe kwa upande wako (na wenzio) hamkuona haja kumsaidia ili CDM waone haya? Unatafuta misifa kwenye msiba. masaburi #1
 
Binafsi, nawapa pole ndugu na jamaa wote wa familia ya mpendwa wetu na baba yetu MH. Bob Makani kwa msiba uliotufika. Tunaungana kumwombea kwa mungu, Baba yetu ili ampumzishe mahali pema peponi. La muhimu kwetu tuliobaki ni kuendeleza kwa matendo yale yote aliyotufundisha. Alikuwa imara kusimamia dhamira safi hata kama ni kwa gharama kiasi gani.
 
Warid Kabourou alimsaliti Bob Makani! Sijui anajisikiaje!
 
R.I.P mzee wetu , ila huyu mzee cdm walimtupa na hawakumpa hata matibabu apart from mchango mkubwa alioutoa kwenye chama

Hajawahi kuwa masikini katika maisha yake na watoto wake wamekwenda shule na sidhani kama alihitaji msaada na akanyimwa. Acha hizo bro.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Rip mzee Makani........umetuachia chama kiko vizuri.
 

Bendera ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ikipepea nusu mlingoti katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaa kufuatia kifo cha Mwasisi wa chama hicho, Mahmoud 'Bob' Makani
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu, Mahmoud 'Bob' Makani

Baadhi ya waombolezaji


DAR ES SALAAM, Tanzania

Aliyekuwa Naibu Gavana wa Tanzania na mwasisi wa Chama cha Demokrasia (Chadema) marehemu, Mahmoud Nyange Makani maarufu Bob Makani, anatarajiwa kuzikwa katika kijiji cha Negezi kilichopo mkoani Shinyanga.

Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Hassan Makani amesema kuwa, marehemu Makani ameacha mke na watoto saba na wajukuu wanane na anatarajiwa kuagwa rasmi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kesho.
 
mzee wetu ametutangulia na tunashukuru kwa kazi ulilolifanyia taifa lako. sisi tuliobaki tukaze boot na hawa majambazi maana ndio wanaharibu nchi
 
Mzee ameondoka ktk maisha haya kwa heshima. Atakumbukwa ktk historia ya nchi yetu kwa mapambano ya ukombozi wa pili wa nchi yetu. Pumzika kwa amani mzee wetu Bob Makani.
 
Msiba wa Bob Makani si msiba wa familia yake, si msiba wa CDM pekee bali ni msiba wa wanamageuzi woote, wapenda mabadiliko na watanzania woote.

Allah ampeke pumziko la amani mzee wetu
 
Wekeni eulogy yake kwa maana ya wasifu wake kamili alipokuwa hai, siyo mlolongo wa "RIP" tu.
Swaiba, Mtanzania hana utamaduni wa eulogy!!!

Mi nishafutwa sana na moderators hapa kwa kukandia maswala ya "RIP... Bwana Ametoa Bwana Ametwaa..." haitusaidii chochote katika kujifunza kutoka kwa kazi ya maisha ya marehemu. Nimesema huko juu hizi ni habari za kuhuzunisha lakini Bob Makini ni nani, alifanya nini katika maisha yake? Hakuna mwenye jibu hapa! Kwenye msiba sisi Watanzania hatujui kuyaenzi na kuyaongelea maisha ya marehemu zaidi ya kusema "Sisi tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi" that's it! full bunkum! Mungu alimpenda zaidi mbona hakum keep mbinguni tokea mwanzo kama malaika?
 
R.I.P Bob Makani. Huyu mzee apewe heshima inayostahili katika kuhitimisha safari yake hapa duniani. Makani amefanya mengi sana haswa kuhusu mabadiliko ya kisiasa ya nchi yetu ; tutamkumbuka sana!!!!!i
 
RIP Bob Makani
Hakika huyu mtu alikuwa mzalendo wa nchi hii hakuruhusu kuisuta dhamira yake,alisimamia alichokiamini.Nakumbuka alikuja mwaka 1993 kutangaza chama Iringa akiongozana na waasisi wenzake Mzee Mtei,Marehemu Brown Ngwilelupi na Marehemu Mary kabigi.Alizungumzia sana kuhusu katiba kusimamia zaidi masilahi ya wananchi badala ya viongozi.
 
RIP Mzee Makani.

ulifanya yaliyo bora, utapata yaliyo bora pia. Amen
 
RIP Bob......Msingi uliotuachia tutauhenzi milele!Kapumzike salama Bob....Mbegu mliyoipanda na mzee mtei matunda yake yameanza kuoneka.
 
RIP amekufa bila kuona jinsi CDM inachukua nchi 2015.Poleni wafiwa Mungu yu pamoja nanyi
 
Back
Top Bottom