Huwezi kusema outright kuwa mungu hayupo kwa vile tu wale wanaoamini kuwa mungu yupo wanashindwa kutoa ushahidi ulio wa kuridhisha na wenye kuhitimisha kuwa kwamba kweli yupo.
Kushindwa kwao kutoa huo ushahidi hakumaanishi kuwa mungu hayupo. Inawezekana kabisa akawa yupo na kwamba tu wao hawajajua yuko wapi na ndiyo maana wanashindwa kutoa ushahidi wa kuridhisha.
Ama inawezekana kweli hayupo. Na kama kweli kitu hakipo basi hakuna anayeweza kutoa ushahidi kuwa kweli kipo.
Kusema outright kwamba hayupo ni kusema kuwa wewe unajua kweli kuwa hayupo.
Sasa kama unajua kuwa hayupo, wewe umejuaje?
Huwezi kusema chochote outright. Hata 1 + 1 = 2 is subject to your acceptance of number theory, which is called a "theory" for a reason. It is not absolute, if it was it wouldn't be called a theory.
Chochote utakachosema kitakwenda kwa ilmu yako uliyonayo wakati huo, na kinaweza kubadilishwa na ilmu mpya.Hii ni kanuni ya msingi kabisa ya usomi. Humility.Uwezo wa kukubali kwamba naweza kuwa sijaona hili muda huu, nikaja kulijua baadaye. Waamini wanajikosesha humility hii kwa kumkubali mungu (at least in the all knowing, all powerful Abrahamic sense).
Na ilmu ya dunia aliyonayo mwanadamu kwa wakati huu hai support uwepo wa mungu.
Ni kazi ya wanaoamini kwamba mungu yupo kuonyesha kwamba yupo, ama sivyo imani yao itabaki kama ngano za mapokeo, zenye mazuri na mabaya yasiyokubali kuhabarishwa na habari za gunduzi mpya.
Kwa msomi yeyote anayejua kwamba uelewa wa binadamu umejengwa katika neurons mbongoni ambazo kama kitu chochote physical zina Planck scale limit na kwa mipaka ya quantum pertubations hatuwezi kuwa absolute, siwezi kuwa absolute hata katika kusema mungu hayupo.
Ninachofanya ni kutoa challenge kwa wanaoamini kwamba mungu yupo ili wanionyeshe wanawezaje kuamini hivyo, hata kwa principles za ku allow for convergence tu ambazo hazishuki huko kwenye kiama cha quantum pertubations na
PlanckScale ambako one is nor wrong, neither right and not could very easily be wrong and right at the same time and space.
Siku nitakayogundua kwamba mawazo yangu yanayoniambia kwamba mungu aliyeumba mbingu na nchi hayupo ni potofu nitakuwa na furaha sana, kwa sababu nitamtulia mungu matatizo yote ya dunia hii, all the poverty, diseases, environmental issues, injustice etc etc yatakuwa ni responsibility yake.
Until then, ni responsibility ya binadamu.