Kama unajua sayansi vizuri, utakuwa unatambua kuwa, kabla ya research au experiment yoyote kuna hatua ya mwanzo ya kuchambua, ambayo unaelezea unahisi jibu au hitimisho la research litakuwa ni lipi. Kuna nia na madhumuni ya kipengele hicho katika steps za experiment, then ukipata jibu, unaformulate hypothesis na kutest kama inaendana na mawazo na dhamira uliyokuwa unaihisi, ni maajabu kwa great thinker kukataa point akiwa hana points za kuipinga hoja au kuwa na idea yoyote.
Beside,,
Mkuu, mimi sijakulazimisha uamini mimi ninavyojua, kila mtu ana haki ya kuamini ambacho anaona ni right.
Peace!
Sayansi nzuri haisemi inahisi jibu la reserach litakuwa lipi. Kitendo cha kuanza kuhisi jibu la research litakuwa lipi ni kuharibu research. Unaweza kusema domain ya jibu la research inategemewa kuwa wapi (kwa mfano square root ya 16 by definition ni ndogo kuliko 16), lakini ukisema jibu unategemea liwe lipi (4) unaondoa openmindedness. Hata kama una jibu lako unalotegemea huwezi kuliweka formally kwa sababu sayansi hairuhusu mambo ya "gut feeling". Na kama unajua jibu litakuwa lipi unafanya research ili iweje sasa? Unaweza kusema jibu ni 4 ukajikuta uko inaccurate kwa sababu jibu halisi ni +/- 4 !
Angalau sayansi inaruhusu testing your premises, whatever they are. Dini ukitaka ku test unaitwa heathen, pagan, infidel etc.
Kwa kufuatisha mfano wangu wa kihesabu hapo juu, kisayansi ukiulizwa "What is the square root of 16?" hata kama hujui jibu kamili, lakini unajua kwamba square root ya 16 ni ndogo kuliko 16, jibu lolote utakalopewa kitu cha kwanza kufanya ni kulipitisha katika initial test ya number line.
Mtu akikwambia jibu ni 23, utaanza kwa kulipima jibu, je 23 ni kubwa zaidi au ni ndogo zaidi ya 16 katika number line?
Utakuta ni kubwa zaidi. Hivyo haiwezi kuwa square root ya 16.
Ukiambiwa 1, utaona ni ndogo zaidi. Kwa hiyo ina uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa square root ya 16 kwa mujibu wa test yako. Lakini kuna test ya pili. Ili namba kuwa square root ya 16, ni lazima upate 16 ukiizidisha kwa yenyewe. Ukizidisha 1 x1 utapata 1 na hivyo utajua si jibu, jibu lipo kati ya 1 na 16.
Kuhusu habari ya kila mtu kuwa na haki ya kuamini anachotaka, naona hunisomi vizuri. Kwa sababu ungenisoma vizuri ungegundua huna haja ya kurudia nilichokwisha kukisema tayari.
Nimesema ni ruhusa kuamini sio tu mungu, bali hata vibwengo na Santa Claus anayekaa North Pole anayekuja dirishani na kuwawekea watoto zawadi za Krismasi usiku wa kuamkia Krismasi. Ruksa.
Lakini kurudia swali nilikwishawahi kuuliza hapo mwanzo, lililorudiwa na Nyani Ngabu katika uzi huu, unajua tofauti kati ya kuamini na kujua?
Wewe unaamini katika uwepo wa mungu au unajua kwamba mungu yupo?
Huwezi kuamini na kujua kwa wakati mmoja. Unachoamini huwezi kuwa unakijua. Unachokijua huwezi kukiamini. Definition ya kuamini inakataza kujua. Ukishajua kwamba mungu yupo, kusema "naamini mungu yupo" itakuwa cheating kama yule mtu ambaye anajua tiketi gani ya bahati nasibu itashinda halafu aende kuisaka maduka yote mpaka aipate. Huyu hajacheza bahati nasibu, huyu ana uhakika.
Vivyo hivyo, ukiamini kwamba mungu yupo maana yake huna hakika kama yupo.Imani maana yake ni kufanya kitu bila ya kuwa na hakika, kwenda kwa kufikiri tu.
Sasa wewe unaamini kwamba mungu yupo (bila kujua kwa uhakika) ana unajua kwamba mungu yupo (kwa uhakika)?