Kwa akili ya kawaida ni lazima waliofanya haya walikuwa na sababu ya kuhalalisha kuyafanya haya.Tumesikia kuwa gari la Rais Museveni lilipigwa mawe na hata kama Bobi wine hakupiga yeye inawezekana tuhuma zikawaangukia washabiki wake na hii ikiwa ndiyo sababu ya kulipa kisasi kwa nguvu kubwa.
Kwa Tanzania tuna ya kujifunza ingawa kwa sasa ni vigumu kwa watu kuelewa.Tuna la TL kupigwa risasi na watu wasiojulikana,tuna na maandamano ya Chadema na kufa mwanafunzi lakini mimi ninachokiona kikubwa na taarifa nyingi za watu kuteswa wakiwa katika vituo vya Polisi na wengine kupoteza maisha.
Uganda limemkuta mbunge na ameelezea kilichotokea,kwetu inawezekana yanawakuta wengi lakini fursa ya kuelezea haipo.
Kwa ujumla hakuna tofauti kwani kama ni darasa tupo ndani ya darasa moja (mwandishi wa habari aliyekula kipigo kwa kubishana na askari na mwisho akaambiwa amemkwida askari).
Ujumbe wangu-Tujiepushe kukabiliana na askari kwa gharama yoyote,tuwe wanyenyekevu hata kama unahisi unaonewa.