Bobi Wine alaani Jeshi la polisi nchini Uganda kwa kujaribu kumzuia kwenda katika uchaguzi

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2021
Posts
630
Reaction score
1,262
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi, al maarufu Bobi Wine, ametuma picha ya polisi na jeshi wakionekana nje ya nyumba yake kabla ya kampeni za uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika katika wilaya ya Kayunga.

Rais Yoweri Museveni anatarajiwa kutembelea katika wilaya ya Kayunga kumfanyia kampeni mgombea wa chama tawala anayewania nafasi ya uenyekiti.

Uchaguzi huo mdogo umepangwa kufanyika Alhamisi na chama tawala na upinzani kwa pamoja vinataka kuonyesha uwezo wao katika eneo hilo.

Bobi Wine ameshutumu jeshi na polisi kwa kujaribu kumzuwia kuondoka nyumbani kwake.
Vyombo vya habari nchini Uganda vimeripoti kuwa polisi na jeshi pia wamepelekwa Kayunga kabla ya kampeni za Jumanne.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…