DOKEZO Boda aliyemuingilia Mwanafunzi wa Darasa la 3 (mbele na nyuma) - Mbande, anatamba mtaani, hatuoni dalili ya haki

DOKEZO Boda aliyemuingilia Mwanafunzi wa Darasa la 3 (mbele na nyuma) - Mbande, anatamba mtaani, hatuoni dalili ya haki

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mdogo wangu wa darasa la tatu amefanyiwa ukatili wa kuingiliwa mbele na nyuma na mtu ambaye kwa sasa yupo nje kwa dhamana na tunaona dalili ya kutotendewa haki kutoka kwa mamlaka zinazohusika.

Wakati anatokewa na kadhia hiyo alikuwa Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kiponza iliyopo Mbande, alifanyiwa ukatili huo na kijana ambaye ni Bodaboda wa mtaani karibu na eneo la shule.

Tulianza kugundua kuna vitu havipo sawa kutokana na mtoto kuchelewa kurudi nyumbani, alipofika alikuwa anaonesha kuchoka kupita kiasi. Alipoulizwa, alitoa visingizio vya uongo kwamba alikuwa kwenye kundi la wanafunzi "10 bora" wanaobakishwa kwa ajili ya masomo ya ziada na walimu.

Hata hivyo, majibu hayo hayakuturidhisha kwa sababu tulikuwa na mawasiliano ya karibu na walimu, tulipowasiliana nao tukabaini hakukuwa na masomo hayo ya ziada.

Kuna siku tulimbana akasema alikuwa anafanyiwa vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia kama nilivyoeleza hapo juu, akamtaja kijana anayefahamika kwa jina la Abdul.
Boda mtuhumiwa.jpeg

Hii ni picha ya mtuhumiwa tuliyompiga akiwa Kituo cha Polisi.​
Akasema rafiki yake wa karibu wa darasa la tatu B ndiye aliyekuwa akimshawishi na kumpeleka kwa kijana huyo (Bodaboda), walifanyiwa vitendo hivyo katika jengo ambalo halijakamilika lipo karibu na eneo la shule, huku wimbi la vijana wengine wakilinda usalama nje kisha Boda huyo anampa fedha rafiki yake na kuwatisha kutosema popote.

Tulienda Shuleni, Mwalimu Mkuu ni Mwanamke, akawakagua akaona kweli inaonekana sehemu zao zimeingiliwa. Tukaripoti Polisi na tukafanikiwa kumkamata mtuhumiwa na mdogo wangu akamtambua.
WhatsApp Image 2026-09-02 at 11.58.08.jpeg

WhatsApp Image 2026-09-02 at 11.58.10.jpeg
Alipelekwa Kituo cha Polisi cha Mbande, watoto walioathirika walipewa Fomu ya PF3 na kupelekwa hospitali ambapo vipimo vya madaktari vilithibitisha wamefanyiwa ukatili huo.

Baada ya mtuhumiwa kushikiliwa, baadaye aliachiwa kwa dhamana bila sisi kupewa taarifa, pia hakukuwa na mwendelezo wowote wa kesi mahakamani. Hali hiyo imekuwa hivyo tangu Julai 2026 hadi sasa (Septemba 2026) hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa, mtuhumiwa anaendelea kuwepo uraiani huru, hatujui anawaza nini.

Kutokana na hofu ya usalama wa mtoto, mazingira magumu ya shule, kuogopa mtuhumiwa anaweza kumfanyia jambo baya zaidi, tulichukua hatua ya haraka ya kumhamisha mdogo wangu shule na kumpeleka mkoa mwingine kuendelea na masomo.

Tunaomba mamlaka zinazohusika zichukue hatua, kwani kama sisi tumebaini waliofanyiwa ni wawili, je kuna wangapi ambao hawajabainika? Kwa nini Vyombo vya Usalama vinachukulia poa jambo hilo au kwa kuwa hawajafanyiwa watoto wao? Inaumiza sana hii.

Waziri aingilia ~ Waziri Gwajima aingilia hoja ya Mdau aliyedai mtuhumiwa aliyemfanyia ukatili mtoto anatamba mtaani

Pia soma ~ Waziri Gwajima: Tuhuma za Bodaboda kumfanyia ukatili Mwanafunzi wa Darasa la 3, Jalada tayari lipo kwa Mwanasheria wa Serikali
 
Duh huko mbande,chamazi mbagala mabinti wengi no
Marinda ndomana wanaanzaga hivyo hivyo
Hii inabidi aione Dkt. Gwajima D

Ova
Mkuu ume mtag gwajima??serikali hii haina maana,mambo hayo wala hawayachukulii kwa uzito usishangae mualifu kua nje

Mwaka 2016 kuna dada mwenye Taasi ya msichana initiative Rebecca Gyumi alifungua kesi dhidi ya serikali kubadilisha sheria ya ndoa kwa watoto,sheria Tanzania inaruhusu binti wa miaka 14 kuolewa,Rebecca akasema miaka 14 ni ubakaji angalau iwe miaka 18..akashinda kesi..

Serikali ikakata rufaa ikashinda...
 
Mkuu nchi yetu bado kuna jamii zimelala fofofo, hazijitambui kabisa. Angalia kesi kama hii mtaa mzima unakaa na kuangalia tu.
Inagikirisha sana, halafu Kuna jamaa wanajiita walinzi wa amani kwenye mitaa aiseee....
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Hii isikie tu kwa mwingine usiombe ifikie kwako, so painful situation, pole sana ndugu. Hii hali ipo maeneo mengi sana na itapelekea watu kufanya jambo lao kwa walengwa kama vyombo vyetu vya ulinzi vikiendelea kuachilia mambo.
Uko nchi gani wewe? Hujui vyombo vya ulinzi vya Bongo ndiyo vinaongoza kwa ulawiti? Halafu hili jina la Abdul lina laana na ulawiti. Abdul wa ki-mama ndiyo kiongozi wa walawiti na Abdul bodaboda ni mlawiti wa watoto.
 
Mkuu ume mtag gwajima??serikali hii haina maana,mambo hayo wala hawayachukulii kwa uzito usishangae mualifu kua nje

Mwaka 2016 kuna dada mwenye Taasi ya msichana initiative Rebecca Gyumi alifungua kesi dhidi ya serikali kubadilisha sheria ya ndoa kwa watoto,sheria Tanzania inaruhusu binti wa miaka 14 kuolewa,Rebecca akasema miaka 14 ni ubakaji angalau iwe miaka 18..akashinda kesi..

Serikali ikakata rufaa ikashinda...
Nimemtag ajuwe huko kumeoza,ilibidi akutane na waziri wa mambo ya ndani
Kama waziri ametumia nguvu kubwa kuonana na wasanii,influencer wacheza vigodoro
Wangefanya program maalum upande huo mbande,chamazi,mbagala sjui rangi sita,buza huko ni full laana

Ova
 
Kwanza kabisa pole mkuu.

Wewe na familia yako poleni sana. Mmefanya vizuri kumuondoa binti hapo lakini kuna kitu naomba niseme.

Mwongozo wa kushughulikia sexual assaults za hivi unataka aliyefanyiwa apelekwe hospital au kituo cha polisi ndani ya siku tatu tangu tukio litokee.

Akiwa hajajisafisha na akiwa kama alivyo.

Ndani ya siku tatu ili kumpa dawa za kumkinga na ukimwi lakini pia ili kuweza kuona sehemu za siri za mhusika zipoje. Mfano kukagua michubuko au damu na ikiwezekana kuchunguza kama kuna shahawa zimebaki.

Hii husaidia hata kipimo cha dna.

Ukipita muda sana ni itaonekana kweli binti kaingiliwa, wataona hakuna bikra na sehemu ya nyuma ipo loose, ila kuhitimisha kwamba aliyefanya ni fulani na siyo fulani itabaki kua changamoto.

Nafikiri hii ndiyo sababu huyo jamaa yupo nje na kesi inakua ngumu kuendelea. Kwa sababu hapo inakua ni mtuhumiwa kukiri, asipokiri, ushahidi wa nguvu unakosekana.

Poleni sana wakuu
 
Back
Top Bottom