Tumwesige senior
JF-Expert Member
- Jan 28, 2013
- 6,978
- 12,641
Ndo maana mi huwa nasema uchawi hautakuja kuisha
au kichwa changu cha chini ndo kibovu hadi kuelewa hivi.
mbona kama huyo kijana Abdul hana kosa, inaonekana huyo Binti mwenyewe aliipenda sana hiyo michezo na ndio maana hakuwahi kusema kama anaumia zaidi akawa anawadanganya tu kuwa walichelewa shule ili awe anapewa utamu na boda.
huo sio ubakaji ila ni maelewano
Ukimtia binti aliye chini ya umri wa miaka 18 hata kama uliona umemtongoza akakubali au alisikia utamu kesho akarudi tena huo ni ubakaji.au kichwa changu cha chini ndo kibovu hadi kuelewa hivi.
mbona kama huyo kijana Abdul hana kosa, inaonekana huyo Binti mwenyewe aliipenda sana hiyo michezo na ndio maana hakuwahi kusema kama anaumia zaidi akawa anawadanganya tu kuwa walichelewa shule ili awe anapewa utamu na boda.
huo sio ubakaji ila ni maelewano
Serikali yenyewe inateka, inatesa, inafira na kuua raia wake.Mdogo wangu wa darasa la tatu amefanyiwa ukatili wa kuingiliwa mbele na nyuma na mtu ambaye kwa sasa yupo nje kwa dhamana na tunaona dalili ya kutotendewa haki kutoka kwa mamlaka zinazohusika.
Wakati anatokewa na kadhia hiyo alikuwa Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kiponza iliyopo Mbande, alifanyiwa ukatili huo na kijana ambaye ni Bodaboda wa mtaani karibu na eneo la shule.
Tulianza kugundua kuna vitu havipo sawa kutokana na mtoto kuchelewa kurudi nyumbani, alipofika alikuwa anaonesha kuchoka kupita kiasi. Alipoulizwa, alitoa visingizio vya uongo kwamba alikuwa kwenye kundi la wanafunzi "10 bora" wanaobakishwa kwa ajili ya masomo ya ziada na walimu.
Hata hivyo, majibu hayo hayakuturidhisha kwa sababu tulikuwa na mawasiliano ya karibu na walimu, tulipowasiliana nao tukabaini hakukuwa na masomo hayo ya ziada.
Kuna siku tulimbana akasema alikuwa anafanyiwa vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia kama nilivyoeleza hapo juu, akamtaja kijana anayefahamika kwa jina la Abdul.
View attachment 3661842Akasema rafiki yake wa karibu wa darasa la tatu B ndiye aliyekuwa akimshawishi na kumpeleka kwa kijana huyo (Bodaboda), walifanyiwa vitendo hivyo katika jengo ambalo halijakamilika lipo karibu na eneo la shule, huku wimbi la vijana wengine wakilinda usalama nje kisha Boda huyo anampa fedha rafiki yake na kuwatisha kutosema popote.
Hii ni picha ya mtuhumiwa tuliyompiga akiwa Kituo cha Polisi.
Tulienda Shuleni, Mwalimu Mkuu ni Mwanamke, akawakagua akaona kweli inaonekana sehemu zao zimeingiliwa. Tukaripoti Polisi na tukafanikiwa kumkamata mtuhumiwa na mdogo wangu akamtambua.
Alipelekwa Kituo cha Polisi cha Mbande, watoto walioathirika walipewa Fomu ya PF3 na kupelekwa hospitali ambapo vipimo vya madaktari vilithibitisha wamefanyiwa ukatili huo.
Baada ya mtuhumiwa kushikiliwa, baadaye aliachiwa kwa dhamana bila sisi kupewa taarifa, pia hakukuwa na mwendelezo wowote wa kesi mahakamani. Hali hiyo imekuwa hivyo tangu Julai 2026 hadi sasa (Septemba 2026) hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa, mtuhumiwa anaendelea kuwepo uraiani huru, hatujui anawaza nini.
Kutokana na hofu ya usalama wa mtoto, mazingira magumu ya shule, kuogopa mtuhumiwa anaweza kumfanyia jambo baya zaidi, tulichukua hatua ya haraka ya kumhamisha mdogo wangu shule na kumpeleka mkoa mwingine kuendelea na masomo.
Tunaomba mamlaka zinazohusika zichukue hatua, kwani kama sisi tumebaini waliofanyiwa ni wawili, je kuna wangapi ambao hawajabainika? Kwa nini Vyombo vya Usalama vinachukulia poa jambo hilo au kwa kuwa hawajafanyiwa watoto wao? Inaumiza sana hii.
Waziri aingilia ~ Waziri Gwajima aingilia hoja ya Mdau aliyedai mtuhumiwa aliyemfanyia ukatili mtoto anatamba mtaani
Upo sahihi sana!Kwanza kabisa pole mkuu.
Wewe na familia yako poleni sana. Mmefanya vizuri kumuondoa binti hapo lakini kuna kitu naomba niseme.
Mwongozo wa kushughulikia sexual assaults za hivi unataka aliyefanyiwa apelekwe hospital au kituo cha polisi ndani ya siku tatu tangu tukio litokee.
Akiwa hajajisafisha na akiwa kama alivyo.
Ndani ya siku tatu ili kumpa dawa za kumkinga na ukimwi lakini pia ili kuweza kuona sehemu za siri za mhusika zipoje. Mfano kukagua michubuko au damu na ikiwezekana kuchunguza kama kuna shahawa zimebaki.
Hii husaidia hata kipimo cha dna.
Ukipita muda sana ni itaonekana kweli binti kaingiliwa, wataona hakuna bikra na sehemu ya nyuma ipo loose, ila kuhitimisha kwamba aliyefanya ni fulani na siyo fulani itabaki kua changamoto.
Nafikiri hii ndiyo sababu huyo jamaa yupo nje na kesi inakua ngumu kuendelea. Kwa sababu hapo inakua ni mtuhumiwa kukiri, asipokiri, ushahidi wa nguvu unakosekana.
Poleni sana wakuu