Bodaboda atekwa, akatwa mikononi na miguu, afungwa kamba

Bodaboda atekwa, akatwa mikononi na miguu, afungwa kamba

Sishani kama ni wanawake.......dogokuna vitu inabidi Atubu tu na kuweka wazi.

Hicho ni kisasi.

Na wakati mwingine Makosa hayakufanywa na yeye.

Kuna mambo inabidi tufikirie na kuyaepuka.

Dogo huenda anatumikia dhambi ya wazazi wake.

Bibilia inatueleza Mungu hupatiliza Kizazi cha wana wa maovu hadi kizazicha Nne.

Huyo dogo huenda Babu yake au Baba yake alishiriki mambo maovu ya kuua, kutesa na au kupoteza watoto wa wengine.

Sasa kama Ilivyo Karma hilo hutokea ili wazazi nao waumie kama walivyowafanyia wengine.
Kwann umewaza kwa upande uo kwann isiwe ni visa vya mwanamke(mke wa mtu)
 
Aah ila ndo lengo la watekaji.
Ngoja nikuambie. Mimi nilishamwokoa jamaa mmoja aliporwa gari la serikali halafu wakamfunga wire mikono na miguu. Ni hivi: Majambazi wakikufunga kamba wanakaza sana sana. Jamaa alikuwa amefungwa kwa kukaza na damu haitembei kabisa. Angebaki hivyo kwa muda mrefu nadhani sehemu za mkono kuanzia pale alipofungiwa kwenda chini zingeoza kwa kukosa damu.
 
  • Thanks
Reactions: apk

Nimekuelewa mkuu.
Ndugu yetu damu ilikuwa aitembei.
 
Huyu aliporwa pikipiki, walimkodi wakamfunga kitambaa usoni, kamba miguuni na mikononi. Wakamtupa kwenye boma mbali na mji huko dumila.
 
Kweli mkuu. Kosa sio la mwanaume ni Demu wako aliemkubalia unakuta uyo kijana ndo alikuwa nategemewa na familia saiv ndo anaitegemea kwa kila kitu.
acha tuu mkuu inasikitisha sana kwakwelii, mpka hiloo tukio linatokea limechukua mda ina maanisha walidhamiria na walikuwa zaidi ya watatu.
 
Huu mkasa unanikumbusha tukio.

Nimewahi kuvamiwa na vibaka watatu wenye panga.

Walinivamia kwa nyuma wakanipiga ubapa wa panga kichwani nikaanguka chini.

Wamenisogelea wanikate nikawa nikelidaka panga nikiwa hapo hapo chini, nikaling'ang'ania kwa nguvu huku linanikata vidole vya mikono bila kuachia.

Mmoja akawa ananipiga mateke mbavuni, huku mmoja akawa ananisachi alipopata simu akakimbia ndipo nikabaki na wale wawili.

Mfukoni nilikuwa na elfu 30 hawakuweza kuichukua maana nilivaa jeans.

Nilipambana nao nikafanikiwa kunyanyuka nikawapush then nikawakimbia.

Wanaume tunafanya kazi zenye riski sana.

Hivyo tujitahidi kufanya mazoezi ni muhimu.

Siyo lazima gim, unaweza ukapiga push-up hata hamsini na ukaweka mwili fit.

Anza push up 5, kesho ongeza hadi uje kufika 100+.

Mwanaume vaa raba pia ni muhimu, au viatu vya kamba. Inasaidia kwenye kipindi kigumu kama hiki.

Mazoezi muhimu maana yanasaidia kiasi chake.
 
Mwandishi ametia chumvi kwenye kichwa cha habari. Siyo hao wezi walimkata. Alikatwa hospital baada ya kufungwa kamba na kukaa nazo kwa muda mrefu hivyo akaoza.
Alikaa na kamba muda mrefu mpaka akaoza, alikuwa anakula nn huo muda mrefu, mbona hakufa kwa njaa?
 
Sishani kama ni wanawake.......dogokuna vitu inabidi Atubu tu na kuweka wazi.

Hicho ni kisasi.

Na wakati mwingine Makosa hayakufanywa na yeye.

Kuna mambo inabidi tufikirie na kuyaepuka.

Dogo huenda anatumikia dhambi ya wazazi wake.

Bibilia inatueleza Mungu hupatiliza Kizazi cha wana wa maovu hadi kizazicha Nne.

Huyo dogo huenda Babu yake au Baba yake alishiriki mambo maovu ya kuua, kutesa na au kupoteza watoto wa wengine.

Sasa kama Ilivyo Karma hilo hutokea ili wazazi nao waumie kama walivyowafanyia wengine.
Kwa sasa neno karma linatumika sana hata pale pasipostahili. Kwani motive ya kufanyiwa hivyo haiwezi kuwa ni kuchukua pikipiki yake? Lawama sasa mnazihamishia kwa babu na baba yake!
 
Back
Top Bottom