Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
Mtwara- Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda mkoani Mtwara wamepata elimu kuhusu matumizi ya mfumo wa e-Ardhi, unaowawezesha wananchi kusajili na kurasimisha viwanja vyao ili kupata umiliki unaotambulika kisheria.
Elimu hiyo imetolewa na Kamishna Msaidizi wa Ardhi (Utawala wa Ardhi), Bi. Hellena Philip, baada ya kuwatembelea katika vituo vyao na kuwahimiza madereva hao kutumia mfumo wa e-Ardhi kusajili taarifa za ardhi zao na kuziwasilisha kwa ajili ya hatua za umilikishaji kwa mujibu wa sheria.
Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kutumia teknolojia kurahisisha upatikanaji wa huduma za ardhi, kuongeza ufanisi na kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi zao kwa usalama zaidi.
Kliniki ya Ardhi Kidijiti inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 25 Septemba, 2026 na Mhe. Dr Leonard Akwilapo Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambapo baada ya uzinduzi huo, Kliniki ya Ardhi Kidijiti itafanyika nchi nzima.
#eArdhi #ArdhiKidijiti #Mtwara #HudumaZaArdhi #Serikali