SI KWELI Bodaboda na Bajaj zapigwa marufuku kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia Aprili 21, 2022

SI KWELI Bodaboda na Bajaj zapigwa marufuku kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia Aprili 21, 2022

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania imewatangazia kuanzia kesho Alhamisi bodaboda na bajaji zote hazitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji hilo.

1657981846184.png
 
Tunachokijua
Baada ya kudaiwa bodaboda na Bajaji za biashara zimezuiwa kuingia Mjini Jijini Dar es Salaam, mamlaka zimekanusha zuio hilo na kuelezea kuna vituo 9 vimetengwa maalum kwa vyombo hivyo, mchakato ukishirikisha viongozi wa Bodaboda, TARURA, Jiji, Polisi na LATRA.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng`wilabuzu Ndatwa Ludigija amesema kuwa utaratibu wa vituo hivyo utawapa urahisi wa kushusha na kupakia abiria na siyo vituo holela kama ilivyokuwa awali.

Aidha, Msemaji wa Shirikisho la Vyama vya Madereva Pikipiki Mkoa wa Dar, Tito Lazaro amesema:

“Utaratibu huo utapunguza uhalifu kwa kuwa kuna wasimamizi, mavazi maalum ya madereva, madereva watawasilisha nyaraka za utambulisho.

Vituo hivyo ni Nasra Tower (Kariakoo), Sabasaba (Msimbazi), JK Park (Mnazi Mmoja), Fire, Mindu & Maliki (Upanda), Suwata (Kariakoo), Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mnazi Mmoja na Kongo (Kariakoo).”
Back
Top Bottom