Bodaboda na Bajaji msijione mmesaidiwa kwa faini kuweni makini eshimuni sheria za barabarani

Bodaboda na Bajaji msijione mmesaidiwa kwa faini kuweni makini eshimuni sheria za barabarani

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Niseme tu kwamba hawa bodaboda na Bajaji nimewaona wakiwa na furaha kedekede bila ya kujua kuwa pamoja na kupunguza faini lazima watii sheria za barabarani na kuhakikisha vyombo vyao vya moto viko sawa na havina itilafu ambayo huenda vikasababisha trafiki wakawakamata.

Sikatai wafurahie ila wajue na niwakumbushe yafuatayo:
1. Bodaboda wengi na waendesha bajaji mikoani wengi hawana Lesseni.
2. Boda boda wengi na waendesha bajaji wengi vyombo vyao havina stika, Bima na havijalipia mapato.
3. Bodaboda wengi wanaendesha bila Helmet.
4. Bodaboda wengi na Bajaji wanaendesha vyombo ambavyo matairi yameisha, Bajaji vioo ni vibovu.
5. Bodaboda na Bajaji wengine hawana hata kadi za vyombo vyao na wengine namba zaa chasis zina tofautiana na zilizopo kwenye kadi.
6. Bodaboda na Bajaji wengi sheria za barabarani ni kama ngeni sana kwao kuzitii ni ngumu sana.

Niseme tu kwamba pamoja na kuwa faini zimepungua sasa wajipange kuwa anaweza akakutwa na makosa 4 hadi 5 na pesa hizo atalazimishwa kulipa na hapa ndio watabaini kuwa elfu 10 sio msaada, waliachwa sana ila sasa hivi wajipange.

Siwaogopeshi ila wazingatie kurekebisha makosa tajwa hapo kuwa hawanayo hii itawasaidia wafurahie faini ya elfu 10 na wa furahie kazi isiyo na misukosuko.
 
Back
Top Bottom